Kaka
Mimi ni mshabiki (Fan) wa mtangazaji mahiri wa RTD (TBC) Swedi Mwinyi hasa kwenye matangazo ya mpira na mengineyo pia.
Nilikuwa nafuatilia matangazo yake hata wakati alipokuwa na Radio DW Ujerumani. Mara ya mwisho kumsikia ni kama miaka 2 iliyopita kwenye runinga ya TBC1 akishiriki kwenye matangazo ya mpira.
Sijamsikia tena kwa kipindi kirefu sana. Wadau mna habari zake? Amepata nyadhifa za juu zilizomfaya aache fani yake ya Utangazaji?
Naomba kuwasilisha swali.

Mdau

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. kweli huyu kaka yuko wapi siku hizi? katika watangazaji mahiri kwa kweli huyu aikuwa ni mmoja wapo. nami ningependa kujua aliko kwa sasa kaka michuzi tusaidie tujue

    ReplyDelete
  2. Ndugu yangu Swedi Mwinyi alipigwa kitu kinaitwa "zengwe" pale TBC na sasa yupo mtaani anazeeka na kipaji chake. Hii ndio bingo!!!

    ReplyDelete
  3. Hivi karibuni nilimwona maeneo ya Sea View, pale mbele ya Court Yard Hotel kwenye taxi nikiwa kwenye foleni. Na nimemwona kama mara mbili hivi. Maybe kijiwe chake kimehamia pale..nenda ukamuulizie pale ndugu waweza ukampata...

    ReplyDelete
  4. Wacha masihara hizi habari ni zakweli au uzushi? Mimi nilifikiri yupo Japani kachukua nafasi ya Amedi Kipozi. Wabongo kweli noma

    ReplyDelete
  5. Zengwe kama la Muro nini japo halikusikika ktk vyombo vya habari?!!!

    ReplyDelete
  6. JAMAA ALIHARIBU SIKU ALIPOKUWA AKIFANYA KIPINDI NA MASHEHE SIKU AMBAYO BUSH ALIKUWA ANAKUJA TANZANIA SASA YEYE AKASHIRIKI KUUNGA HOJA ZA MASHEHE ZA KUPINGA UJAJI WA BUSH NA WAKATI YEYE ANAFANYIA KAZI CHOMBO CHA SERIKALI NA ANATAKIWA KUISAIDIA SERIKALI... INGEKUWA ITV ANGEFUKUZWA SASA HUMU ANAMINYWA TU KIMTINDO!... HABARI NDIO HIYO NA HIVYO NDIVYO TUNAVYOISHI NDANI YA TBC!

    ReplyDelete
  7. Inauma sana, watu wanapewa uongozi TBC halafu wanaachia vipaji na vifaa kama Sued Mwinyi, Juma Nkamia, Baruhan Muhuza, Rose Reuben, na wengine kibao vinapotea. Lakini Poa nikipata Nauli nitakwenda kumueleza Mjomba kuwa huku mambo si shwari.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...