Ankal, kwanza nakupongeza kwa kuwa
mmoja katika watu waliopata shahada
ya shukran kutoka Serengeti.

Leo Ankal nakutumia picha hii ambayo ni shimo lililopo katika bandari yetu
ya Dar-es-Salaam, eneo la kupandia abiria kuelekea Zanzibar na Pemba.

Shimo hili limechimbwa kunako mwezi wa saba mwaka jana yaani 2009 kwa nia ya kutengeneza njia ya kupitisha maji ya mvua yanayotoka mjini kuelekea baharini. Njia hiyo ilikuwepo ila kutokana na uchakavu wa miondu mbinu ikawa wakati mvua kubwa inanyesha, maji yanajaa bandarini badala ya kwenda baharini.
Kwa nia nzuri kabisa Mamlaka ya Bandari (TPA) iliamua kuchimba eneo hilo na kuerekebisha.

Kama nilivyoeleza hapo juu shimo likachimbwa mwezi wa saba mwaka jana na
kama unavyoona, mpaka leo hii bado liko wazi. Huko chini kumetengenezwa, yaani wameshaweka mabomba ya udongo maarufu kama kalavati, lakini cha kusikitisha ni kuwa maji bado yanapenya pembeni mwa hilo kalavati na kufanya kufunika kwa shimo hilo kuwa kitendawili.

Ni hatari kwa abiria wanaotumia sehemu hii ya bandari na aibu kuwa kazi ndogo kama hii inachukua zaidi ya miezi sita. Cha kufurahisha zaidi ni kuwa mafundi na vibarua wanakuja kila siku wanasogeza mawe au mchanga au kokoto au wanafika tu na kuteremka chini kwenye baji na kulala mpaka saa nane au tisa wanatoka na kuondoka. Siku imeingia.

Je huu si ufisadi?
Au tuuiteje?
Mdau wa Libeneke
la nanihii

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Tunasubiri msaada kutoka kwa Wafadhili, Japan, Scandinavia....

    ReplyDelete
  2. Kweli wahusika hawapo serious kabisa!

    Nawashauri waunde tume, kazi kwisha.

    ReplyDelete
  3. Kwa mujibu wa kauli ya Waziri wa Mazingira, Shirika la mazingira la UN limeishatoa mamilioni ya kuweka jiji la dar katika hali ya usafi - tusubiri pengine na hilo shimo litanufaika na msaada/deni hilo. Bongo tambalale (sio tambarare)!!!! Ninakubaliana na mdau aliyesema kuwa nchi imeishauzwa, acha kila mbongo afanye atakalo!!!

    ReplyDelete
  4. wee mdau #1 acha masihala

    sasa wewe unaerekebisha lugha?kiswahili kigumu ndugu

    ili shimo litafukiwa adi mtu aanguke umo tu/yaani ajali itokee
    vp ile keep-left yetu ya pale bot?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...