UPENDELEO WA KUPITISHA MAGARI KATIKA TAA ZA MAGOMENI MAPIPA
Ndugu Balozi wa nani hii, sasa imekuwa ni muda mrefu (zaidi ya wiki 4) tokea ndugu zetu wa usalama barabarani wamweke mwanausalama huyu pale Mapipa mataa.
Badala ya mwanatraffic huyu kurahisisha kazi ya kupitisha magari amekuwa na upendeleo dhahiri kwa magari yanayotokea Kinondoni na Ilala. Mara nyingi utakuta anapitisha magari ya pande hizo kwa kurudia safari tatu mpaka nne kabla ya kupitisha magari yanayotokea Ubungo.
Na hata anapopitisha magari kutokea Ubungo atapitisha magari manne na kupiga stop. Foleni siku hizi saa moja kasorobo inaanzia Urafiki sielewi baada ya muda hapo inakuwaje. Sasa imekuwa ni kawaida kwa wafanyakazi wanaotokea Ubungo kuingia kazi saa mbili na nusu mpaka saa tatu na kuendele.
Hali hii imechangia magari mengi kupita njia za pembeni (Mikumi na Magomeni Tanesco) ili wakaingilie barabara ya Morocco wapate urahisi wa kupitishwa na traffic.
Tunaoumia ni wale tunaotumia usafiri wa daladala maana kutoka Ubungo mpaka Mapipa tunatumia zaidi ya saa mojana nusu. Jambo la kushangaza ni kuwa tukishapita Mapipa mataa tunachukua kati ya dakika 15 na 20 mpaka Posta mpya au dakika 10 mpaka Kariakoo kwa hiyo Jangwani hakuna foleni kubwa.
Tunaomba utuwasilishie kilio chetu kwa wanohusika wamtupie huyu mwanatraffic jicho au wambadilishe kituo.
Mdau Willy
Habari ya Matrafiki kufanya kazi kwa upendeleo imezidi
ReplyDeleteJunction ya Kinondoni na Bagamoyo road,pale Salender bridge yupo Trafiki anaitwa SAMWELI,
ameziki kugandisha magari yatokayo kinondoni.
huyo tayari maandalizi yamefanyika apewe kipigo cha nguvu muda simrefu.
so huyo wa magomeni leteni jina na picha tumuandalie disiplin yake.
Viongozi wao ndo wanawapa vichwa vya kufanya kazi kwa upendeleo.
Yule wa mwanzo alikuwa anapendelea sana magari toka Ubungo kiasi kwamba sis wa ilala na Kinondoni tulikuwa tunakaa sana mpaka dakika 20 wakati upande wetu hauna magari kabisa, huyu wa sasa amejaribu kubalansi anawapendelea wa ubungo lakini bila kutuumiza sisi, binadamu hamridhiki mnataka mpite nyinyi zaidi wakati mnakotoka kuna magari mengi. Bora zibaki taa tuone sasa
ReplyDeleteYaani ni kweli kaka Willy naona kama kun amakusudi ya trafiki kutukomoa tunaokwenda katikati ya jiji asubuhi,huo wa mapipa ni mfano mmoja sisi wa barabara ya Ali Hassana Mwinyi siku hizi tunakoma yaani foleni inaanzia pale mataa ya ubalozi(karibu na salender)hadi mwenge!yule trafiki wa pale anaruhusu magari yanayotokea kinondoni tu ila haya yanayotokea mwenge na mikocheni anayabania kama wiki ya tatu sasa hako kamchezi kanaendelea naona kama kuna makusudi kweli kwani ukivuka hapo huko mbele hadi unaingia city centre hakuna foleni na unaweza kutembea hadi 80km/hr!inauma kwa kweli ukifika njia panda ya kuelekea agakhani hspl ndio utakuta hao trafiki wamejipanga gwaride wanawahimiza madereva waongoze mwendo!!!!yaani mi hadi huwa nacheka badala ya kwenda kukaa kipita shoto cha kawe kwenye msongamano wao wanakuja kujijaza mjini ambako magari yanakwenda kwa kasi.
ReplyDeletekwani traffic signals zimekufa? kwa lugha ya kitaalamu, huyo polisi ni 'incident' by himself.
ReplyDeleteHiyo ni moja ya mambo yanayoonyesha leaders in our motherland dont know what they are doing.
Nafikiri tunahitaji sasa CCU=chama cha ukombozi manake mapinduzi kimetupindua kwelikweli
yaani kwa kweli napeta nimuunge mkono ndugu yangu hapo....
ReplyDeleteOf late, najikuta natumia zaidi ya saa moja na nusu kufika mjini kutoka Ubungo!!! yule askari anafanya komesha kiaina!!! leo nimefika pale kwenye mataa ya mapipa nikasimashwa...wakati mimi nilikuwa gari ya nne kutoka ile ya kwanza iliyoruhusiwa... kwa maana hiyo alipitisha matatu halafu akapiga mkono wa kusimama!!! kwa kweli anatuharibia siku na kazi pia.... sasa kweli ni haki mtu uanze kutoka nyumbani saa kumi na mbili kasoro wakati nakaa chuo tu hapo!!!?? kwa kweli kaka Michu tusaidie... tunazidi kwazika watumiaji wa barabara ya Morogoro...
Mimi nashauri ukifika magomeni mapipa....ni afadhali ushuke utembee maana it will take less time kuliko kuganda kwenye foleni au wewe unaonaje?
ReplyDeleteTumo ktk karne ya 21, karne ya sayansi ya teknolojia. Teknolojia ya kisasa ya na thabiti ya kuongoza magari ipo. Kodi tunalipa. Jiji halikosi pesa ya kuweka teknolojia mpya, bali wanachokosa ni vipaumbele. Hayo ya askari (binadamu) kuongoza magari kwenye makutano ni ya karne ya 20. Ni aibu kujivunia uchumi wa soko huria (ubepari) ambao umeongeza idadi ya magari hali huku tukiendelea kutumia barabara na taa za kuongezea magari za Mwalimu (yaani ujamaa). Hili ndilo tatizo. tatizo si askari huyo au hao!!!! Bongo tumekwama!!!!!
ReplyDeleteanon wa feb 1 at 04:10:00 I like that CCU lett it come now now.
ReplyDelete