Katibu wa Siasa na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Singida mjini Bw.Hassan Mazala akitoa hotuba kwa wana CCM Singida Mjini Jimboni kwa Mh.Mohammed Ghulam Dewji.
KATIBU wa Siasa na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Singida Mjini, Hassan Mazala amewaasa viongozi waandamizi wa Jimbo hilo kuepuka makundi na baadala yake waendeleze mshikamano ilikuendeleza mshikamano na kupata ushindi wa kishindo katika uchaguzi ujao.

Akizungumza katika maojiano maalum juu ya hali ya kisiasa jimboni humo, jana jijini Dar es Salaam , lisema kuwa mpaka sasa Viongozi wameweza kutekeleza ilani ya Chama kwa asilimia kubwa na kuendeleza matumaini kwa wananchi, viongozi hao ni Rais, Mbunge na Madiwani katika Halimashauri hiyo ya Manispaa ya Singida.

“Viongozi wote waliochaguliwa mwaka 2005 kupitia CCM, wameweza kutekeleza Ilani kwa asilimia kubwa, zikiwemo ahada zao binafsi. hivyo nawaomba Viongozi na wana CCM tuendeleze mshikamano tulio kuwa nao” alisema Mazala.

Mazala aliendelea kusema kuwa, kwa kipindi cha kuelekea uchaguzi mkuu, vuiongozi wa wa juu wa Chama ambao ndiyo wanaokuwa na dhamana ya kupendekleza viongozi kuingia katika michakato mbalimbali, aliwaasa kuachana na makundi pamoja na chuki ambapo kama wataepuka hali hiyo Chama kitaendelea kuimalika.

“Unaweza kumshagua kiongozi kwa kutumia ulaghai, lakini je anaweza kutekeleza ilani ya Chama kwa vitendo?, hivyo kama viongozi wanajukumu la kuangalia hilo kwa undani na wala wasiangalie wapi kuna maslai binafsi” alimalizia Mazala.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Bwa' Michu habari za CCM zimeanza kutawala globu. Ina maana vyama vingine havina habari au ndio mwelekeo mpya wa globu katika 'hiki kipindi kibaya'?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...