Makamu wa Rais Dk Ali Mohamed Shein, Balozi Mwanaidi Sinare Majoor, wakiwa katika picha ya Pamoja na Rais wa Chama cha Touch Foundation Lowell Bryan na Mkwewe katika hoteli ya Marriot usiku wa kuamkia leo jijini London. Chama ambacho kinakusanya michango kwa ajili ya kuimarisha miundombini ya Hospitali ya Bugando jijini Mwanza, Chuo cha Udaktari cha hapo Bugando na Udhamini wa wanafunzi wanaosomea udaktari chuoni Bugando. Makamu wa Rais Dk Ali MOhamed Shein akizungumza na Mzee Rajan ambaye ndiye alikuwa mhisani Mkuu wa chakula cha jioni kilichaandaliwa katika hotel ya Marriot hapa London kwa lengo la kukusanya fedha za kuimarisha mindombinu ya Hospitali ya bugando pamoja na chuo cha Udaktari cha Bugando jijini Mwanza. Makamu wa Rais Dk Ali Mohamed Shein na Balozi Mwanaidi Sinare Maajar wakizungumza na mmoja wa waalikwa walioshiriki katika hafla hiyo usiku wa kuamkia leo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. HUYU BABA MUNGU AMPE NGUVU PIA ASIJAALIWE KUWA NA STORI CHAFU KATIKA HII NCHI. KWANI ANAJITUMA NI MNYENYEKEVU HAPENDI MAKUU SIJUI KAMA NI MAONI YANGU FINYU ILA NINACHOSEMA MUNGU AMPE NGUVU TU.

    By Mdau

    ReplyDelete
  2. Mr. Vice u look so good!!!

    ReplyDelete
  3. Wadau, wale waliojaaliwa uwezo lazima tuchangie sekta za elimu na afya. Nilipokuwa nasoma ughaibuni kitu nilichogundua ni kuwa watu wenye uwezo husaidia sana sekta za elimu na afya ama kupitia "trusts" au "foundationa" au hata ujenzi wa miundombinu zinazohitajika na scholarship. Hii inahakikisha kuwa huduma inajengwa na ufisadi unapunguka. Kama alivyosema JFK "Ask not what your country can do for you, but ask what you can do for your country". Utamaduni huu unafaa kukuzwa. Ed.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...