Ni Bonge la picha linaloanzia kijijini, Hisan Muya “Tino” anacheza kama kijana fukara akiwa amekomea kidato cha sita na kushindwa kuendelea na elimu ya juu kutokana na uwezo duni wa wazazi wake (Mzee Magari na Mama Kawele).
Uwezo wake duni pia unamfanya asikubaliwe kumuoa kipenzi chake cha muda mrefu Rose Ndauka ambaye anatoka familia yenye uwezo. Wazazi wa Rose Ndauka Mzee Olotu na Dotnata wanaamua kumuoza Rose kwa mtoto kutoka familia ya kitajiri Mohamed Nurdin “Chekibudi” Rose bila hiyari yake anaolewa na kwenda kuishi nyumbani kwa kina Chekibudi ambako huko anakutana na vituko vya wifi Aunt Ezekiel, mama mkwe Bi Hindu na shemeji Basupa. Mwana dada kutoka fani ya Bongo Fleva Queen Darleen nae anafunika vilivyo ndani ya filamu hii na kuwa kiungo muhimu katika kuwakutanisha tena Tino na Rose Ndauka.
Safari hii Tino akiwa mtu mwenye uwezo anapambana kumrejesha Rose katika himaya yake huku Chekibudi nae akisimama kidete kuhakikisha ndoa yake haitetereki. Ndani ya filamu hii iliyojaa simulizi za mapenzi yanatokea matukio kadhaa ya kisiasa na kisasi pamoja na watu kuporomoka na kupanda kimaisha huku wengine wakiishia kwenye mikono ya sheria.
Cha kuvutia zaidi ndani ya Cut Off ni kwamba maadili yamezingatiwa ipasavyo, ni filamu ambayo unaweza kuitazama mwanzo hadi mwisho ukiwa na wanao au mkweo bila adha ya lugha chafu au matukio yaliyo kithiri kimapenzi.
Filamu imeandaliwa na Screen Masters huku production ikifanywa na Sofia Production, Imetungwa na Hisan Muya “Tino” na kuongozwa na Issa Mussa “Cloud”. Sehemu kubwa ya filamu ya Cut Off imechezewa Boko Mbweni na Mbezi Beach Dar es Salaam. Mkurugenzi wa Screen Masters Said Mdoe amesema Cut Off ipo jikoni katika hatua za mwisho kabisa na inatarajiwa kuingia madukani muda si mrefu.
Mdoe ameongeza kuwa Cut Off ni filamu ambayo imejaza mastaa wengi pengine kuliko filam nyingine yoyote ile hapa Bongo. Miongoni mwa sura zitakazoonekana katika Cut Off ni pamoja na Mzee Yusuf, Cloud, Big Matovola, Nyoshi El Saadat, Nurdin Canavaro, Banza Stone, Mwinjuma Muumin, Juma Mbizo, Isha Ramadhan “Mashauzi” , Juma Pondamali na wengine kibao.
Yep, tunataka kuwe na watengeneza movie utitiri tu Bongo ili kuweka sawa soko kwa ujumla pamoja na ushindani. BIG UP
ReplyDeletesame old stories ..nothing new.copy and paste ..movie gani inatengenezwa mwezi mmoja..!
ReplyDeletestory ndio zile zile, kijana wa kifukara baadae anakuwa tajiri, kwenye movie za kibongo hamba reality kwamba fukara anakufa fukara always lazima atajirike, badilisheni story,kuweni creative, iso lazima kama wewe ndio unaicheza hiyo movie na kutunga pia utunge,watafute wakongwe na story wawatungie kama wakina mzee mfaume na wengineo.
ReplyDeleteukiachna na kijana wa kifukara basi ikibadilishwa sana ni kugombea demu, story ni moja ila zinabadilishwa majina tu. wabongo bwana ovyooooooo, hebu angalieni ile movie ya TSOTSI(kumradhi naweza nikawa nimekosea jina ila nimeeleweka) mlishawahi kujiuliza kwanini hii movie ya ki south ilishindanishwa kwenye tuzo za OSCAR?(sio ile ya kisani cha oscar ya mtaani ya kanumba)
mnajitahidi kiasi chake!lakini mnabahitisha sana! tafuteni profile za wasanii wenzenu wakubwa duniani muwaone walikopitia wengi hawakubahtisha! wamekwenda vyou vya sanaa na wanahuakika wanachikifanya! mfano waliotengeneza hii filamu wote wameokotana tu! Ushauli:(1) Nendeni shule zipo nyingi SOUTH AFRICA kuna college kibao za sanaa nendeni huko mkajifuze au BAGAMOYO basi mkishindwa
ReplyDelete(2)Tafuteni watahalamu wa mavazi wawashauli, mfano nikitazama hiyo picha hapo juu kuna makosa kibao!
WELL DONE GUY'S!!!!
ReplyDeletehaya ndo mambo yenyewe tunayotaka kupata kutoka kwa wa TZ, tumechoka na filamu za Nje zisizo na mafundisho na mwelekeo wa jamii ya TZ, mtaleta ushindani wa maendeleo.
kazi nzr sanaaaa!
Hakuna mpya hapo. Story ni zile zile..
ReplyDeleteTunaisubiri sana hii.
ReplyDeleteHongereni kwa hatua mliyofikia.
WASANII WETU WANFANYA KAZI NZURI SANA.
ReplyDeleteLAKINI KWANINI MAJINA YA PICHA NI YA KIINGEREZA?!!!
TUKITUMIA MAJINA YA KISWAHILI FILAMU ZETU HAZIUZIKI AU HAZIPENDWI?!
WATU WA MASOKO WATUSAIDIE KUHUSU HILI!
AU WASANII WANALENGA SOKO LA WANAOONGEA KIINGEREZA ZAIDI NA SIO WAZALENDO WANAOZUNGUMZA KISWAHILI
ni kweli mdau wa tatu hapo juu ile movie ya tsotsi imechezwa na kina kanumba wa south lakini iko juu sana huwezi linganisha na maigizo ya bongo mtu anatengeneza movie 3 kwa mwezi tatizo wanaiga sana wanaijeria badala watoke kitofauti halafu ukiwaambia ukweli wanakuja juu na kuita watu mahater hasa hao mashabiki wao huko ni kudumazana tuu na wanajiona wanajua saana hata hivyo vyuo vinavyotoa mafunzo wanaona havina maana kwa vile ati wao ni mastar wapiiii hatujaona movie bado sanaa
ReplyDeletenime mind sana jamaa huyu chekibudi, je ameowa jamani kaka michuzi hebu nitafutiye contact zake kama hajaoa please.
ReplyDeletemdau los angeles u.s.a
Wee mtoa maoni wa U.S sijui hata kama upo U.S kweli,UNANIKUMBUSHA HSPO ZSMSSNI DEMU AKIWA MWEUPE TU; SI NYODO HIZO:
ReplyDeletemi hata Qeen Darling Nimeshindwa kumtambua kutokana na mapoda aliyo jisiliba usoni,
WEUPE SIYO UZURI JAMANI STAY BLACK STAY BEUTY;
TUNGENI FILAMU ZENYE MAADILI YA KIAFRIKA SIYO HIZI COPY AND PASTE; SASA SIBORA NIANGALIE MOVIE YA HOLLYWOOD KULIKO HUO UCHAFU WENU:
angalia na vitambi vyao, halafu wanajiita ma star na kujifananisha wao na wa Hollywood, hebu waangalieni wakina brad Pitt kama wanavitambi. msanii wa bongo hata akitoa wallpaper huwezi kununua na kwenda kutundika hicho kitambi ukutani, wabongo bwana, eti kumjua mwenyehela mpaka awe na kitambi. yaani wananiudhi mpaka basi.
ReplyDeleteanon 02:25 AM umenchekesha sanaaaaaa, hehehehe..KWELI huwezi kununua kitambi ukatundike ukutani bwana.
ReplyDeletekwani lazima ununue???
ReplyDeleteCUT OFF ndio maana yake nini????? Kuweka majina ya mastaa wengi ndio nini au ndio iweje????
ReplyDeleteJamani kazi ziko nyingi na sio lazima wote mtengeneze filamu.
hi ankal!
ReplyDeletepls ask the guys: What is PARAPHRASING? and does it help to tanzanian culture?
NONDO
nimecheka adi basi!!na hivi naumwa kichwa mbona kimepona?
ReplyDeleteila jamani,badilisheni izo majina ya kiinglish na stori zisifanane
pluliiizzz
kwanini mna vitambi nyie watoto?
ReplyDeletewasanii mbadilike. mnaigiza vitu vya kufikirika sana yan no reality.
ReplyDeletemnafanya watoto wanaongalia hzo movie kufikiri hayo ndo maisha wakat si maisha halisi hayo mnaigiza. try to be more realistic with tanzanian life. msigize stail za maisha ya watu wachache sana nchini.watanzania wengi ni masikini hawawez kujifunza kitu hapo. kiukwel movie za kibongo zinaboa sana...unakuta kwenye movie mtu anamuuliza mwenzie jina wakati ameshamuita jina lake...au movie zingine zinatumia lugha ya stor jinsi mtu alivyofanya zaman halaf anaonyeshwa akiwa mzee na mazingira ni yaleyale bila hata kubadili kuendana na ilivyokua...mnafanya kama mnaigiza jukwaan jaman...jipangeni...
PARAPHRASING means to repeat something writen or spoken using different words and shorter form that makes the original meaning cleared, we know wat its means my friend we are not dummy
ReplyDeleteNawapongeza ndugu zangu kwa jitihada za mwanzo lakini kusema ukweli bado tuko nyuma katika utengenezaji wa filamu zenye quality achilia mbali theme za kuvutia.
ReplyDeleteHivi mmeshaona zile tafsiri za kiingereza wanazoandika kama subtitles! Jamani, sijawahi kuona kiingereza kibovu kama kile. Sijui wanakuwa wanalenga watu gani wazisome!(Watanzania wanaosikia Kiswahili au.....?) Ile inaonesha kukosa umakini katika uandaaji, kwani sidhani kama hamna watanzania wenye uwezo wa kutoa tafsiri sahihi..
kwa kweli hawa ni vijana wadogo na inashangaza VITAMBI vyao vikubwa kulingana na umri wao , mimi kama mdau najitolea waje katika gym ya iko kariakoo mtaa wa GOGO nitawasaidia kuwalipia kama pesa ni tatizo kwao , kwani ni aibu hata kuwafamahisha rafiki zangu walioko nje kwamba hawa ndio Masta wa TZ , acheni kujibweteka jamani , mkipata visenti tu VITAMBI MWAAAAAA !!!! mikanda haifungi !!!
ReplyDeleteebu kavaeni mashati funika hizo mimba za panya
ReplyDelete