Mkurugenzi Mwandamizi wa ghazeti la Jamboleo Ben Kisaka (katikati)akiongea na Mkurugenzi wa Masoko wa Vodacom Tanzania Ephraim Mafuru(kushoto) na Mkurugenzi wa maswala ya uhusiano Mwamvita Makamba(kulia) katika ofisi za ghazeti hilo ambapo mtandao huo unaendelea kutembelea vyombo vya habari na kufikisha ujumbe wake wa kushusha gharama ya kuongea kwa shilingi 1 kwa sekunde siku nzima kwa wateja wa Vodacom.
Mkurugenzi wa Kitengo cha Uhusiano cha Vodacom Foundation, Mwamvita Makamba (wa pili kushoto), akimuonesha tangazo la punguzo la gharama za huduma kwa wateja la 'habari ndiyo hiyo', Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Kampuni ya Jambo Concepts Limited, Juma Pinto wakati uongozi wa Vodacom ulioongozwa na Mkurugenzi wa Masoko, Ephraim Mafuru (wa tano kushoto), ulipotembelea jana ofisi za kampuni hiyo inayochapisha jarida la Jambo Brand Tanz ania na gazeti la Jambo Leo zilizopo Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni Meneja Masoko wa Jambo Concepts, Suleiman Rutakinikwa na Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Benny Kisaka. Kulia ni Meneja Mawasiliano wa Vodacom, Nector Pendaeli - Foya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Jambo Concepts.Mkurugenzi wa Kampuni ya Jambo Concepts Limited, Benny Kisaka (kushoto), akiwaelezea viongozi wa Vodacom Tanzania, kuhusu utayarishaji wa Jarida maalum la Jambo Brand Tanzania, litakalokuwa na habari za kuitangaza Tanzania, litakalosambazwa wakati wa fainali za Kombe la Dunia, nchini Afrika Kusini baadaye mwaka huu. Viongozi hao walioongozwa na Mkurugenzi wa Masoko, Ephraem Mafuru (wa pili kulia) na Mkurugenzi wa Kitengo cha Uhusiano cha Vodacom Foundation, Mwamvita Makamba (kulia) walitembelea ofisi za kampuni hiyo, Dar es Salaam jana, kwa ajili ya kutangaza punguzo la huduma kwa wateja ya 'habari ndiyo hii' ambapo sasa itakuwa shilingi moja kwa sekunde kwa saa 24. Wa tatu kulia ni Mkurugenzi wa Bodi ya Jambo Concepts inayochapisha pia gazeti la Jambo Leo, Juma Pinto. Picha na mdau Richard Mwaikenda

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. pinto naona bongo umesha fika sasa

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...