Habari yako Unkali,
Nashukuru kwa hii habari uliyo weka hapo na e-mail address yako. Sasa naomba jina langu usilitumie popote itakapo hitajika ila naomba nikutaarifu kuwa kanisa la Wasabato (S.D.A) watakuwa na tukio kuuubwa (BIBLIA INAYO ZUNGUSHWA DUNIA YOTE) litakalo anzia leo mida ya saa 5 hivi pale airport ambapo Kanisa la S.D.A limeamua kuikumbusha Dunia kurudi kutumia biblia kama muongozo pekee wakuwaongoza katika kumfaham Mungu wa mbinguni na maelekezo yake ya namna binada anavyo takiwa aishi hivyo kanisa limeamua kuizungusha BIBLIA DUNIA YOOTE na leo hiyo satano itakuwa inaingia Tanzania sijui itakuwa inatokea nchi gani lakini hii ni ratiba halisi wala sio ya wasiwasi. Program hiyo hapo airpot kwa Julius Kambarage Nyerere itafuatiwa na maandamano ambayo yataanzia hapo airport hadi Kanisa la Wasabato la Magomeni hapo Mwembechai. Na kesho kwa Dar na Pwani ndio itakuwa siku yao ambapo watakusanyika Wasabato woooote kutoka makanisa yoooote ya kisabato ya Dar na Pwani kuanzia saa 2:00 asubuhi pale uwanja wa taifa wa zamani (Uhuru) na itakuwa ni program itakayo enda hadi saa 11 jioni. Baada ya hiyo kesho tukio hilo litaenda mikoa mingine itakayo chaguliwa kabla BIBLIA HIYO haijaendelea na safari kwenda nchi zingine. Kaka nitakushukuru saaana kama matukio haya nitayaona kwenye globu yetu hii inayo tuhabarisha vilivyo.
Asante na siku njema.

Safari hii hamtaki kwenda nje ya nchi bure, bila passport wala visa!!
ReplyDeletemtoa maoni wa kwanza,jifunze kuheshimu dini za wengine,sio wasabato wote walikuwa kwenye ishu ile,wale ni wasabato masalia na wala kanisa haliwatambui!
ReplyDeletetutakuwa pamoja kesho katika ibada
Bwana awabariki
Mdau
Magomeni SDA
Jambo la maana kukumbushana maadili an miongozo ya kiroho...Mungu awabariki kwa mpango huo. Mimi binafsi nasubiri habari na picha kwa shauku kubwa. Natamani pia ningeweza kutathmini matokeo ya ujumbe huu duniani. Jambo linalinifuraisha kuliko yote katika mpango huu ni kwamba hamtangazi dini... mnatangaza BIBLIA... Asanteni sana.
ReplyDeleteWale hawakuwa wasabato, maana kama sherehe hiyo ya biblia ilivyo (kutukumbusha usomaji wa biblia). Biblia inasomeka kumheshimu MUNGU na pia kuziheshimu mamlaka ambazo Mungu ametupatia. Kutumia Passport ni moja kati ya sheria zilizowekwa na mamlaka ambazo Mungu amesema tuziheshimu pia.
ReplyDeleteWale walisingizia usabato tu. Wasabato utawaona Leo!!
Ni jambo kubwa ila shetani atawafunga macho wengi wasione! Ni kuwaombea tu..... Ni moja kati ya mikakati ya kumaliza kazi tuliyopewa ya kuhubiri biblia ulimwenguni kote.
ReplyDeleteHA ha ha Thanx Judith Wambura (Mrs Habash)
ReplyDeleteahsanteni wasabato,mi naungana na mtoa maoni hapo kwamba jambo kubwa hapa si udini bali ni kukumbushana juu ya matumizi ya kitabu kitakatifu Biblia ili hatimaye sote tufike mbinguni siku ile parapanda itakapolia. pia wale hawakuwa wasabato bali kikundi cha watu wanaopotosha maandiko na ndo maana aibu iliwafika
ReplyDeleteAmen.. Na Mungu Awatangulie kwa kila litakalofanyika katika siku hiyo..
ReplyDeleteCheckingo's Family
Wow! Mimi kama muamini mpya katika kanisa hili na hapo mwanzo nilikuwa Mkatoliki, Natoa ushuhuda kuwa "HAKUNA JAMBO ZURI NA LENYE FARAJA SANA MAISHANI KAMA KUMJUA MUNGU NA KUMTAFAKARI KATIKA KWELI NA KATIKA ROHO. NI FARAJA KUU MNO!" Hivyo nawahimiza watu wajitokeze hata kama sio wasabato wakasikilize, Hakika hutatoka kama ulivyokuja ifikapo saa 11 jioni hiyo kesho. Mbarikiwe sana wote; (Waandaaji, wasikilizaji na Wahubiri watakaohusika).
ReplyDeletethats great,tunawaunga wasabato kwa kazi nzuri kama hiyo.biblia ni taa pekee inayounganisha wakristu wote duniani
ReplyDeleteMungu atutangulie mbele.Biblia itasomwa ulimwenguni kote.natamani ningekuwepo huko na mimi ningejumuika wa wasabato wenzangu. ila najua mbele za Mungu tuko pamoja na nimejumuika nanyi kiroho.
ReplyDeleteMaranatha!!