Askofu wa Kanisa la KKKT Dayosisi kuu ya Magharibi, Elisa Bubelwa akikata utepe kuashiria uzinduzi wa uchangiaji wa harambee kwa njia ya SMS Dar es salaam jana kwa ajili ya kuchangia uanzishwaji wa chuo kikuu cha Joshua Kibira university College(JOKUCO) mkoani Kagera
Na Ripota wetu
KANISA la Kilutheri Dayosisi ya Magharibi mjini Bukoba,limewataka watanzania kuchangia gharama za uanzishwaji wa chuo kikuu mjini humo kitakachofahamika kwama Joshua Kibira University College (JoKUCo).
Mwenyekiti wa kamati ya uwanzishwaji wa chuo hicho,Bw.Moses Kagya alisema chuo hicho kitagharimu sh.bilioni 1.3 ili kukamilika na kuanza kutumika.

Bw.Kagya alisema kuwa kuwa wananchi watachangia fedha kwa njia ya ujumbe mfupi (SMS) ambapo mchangiaji atatakiwa kutuma ujumbe wenye neno 'Mchango' na kutuma kwenda namba 15787.
Alisema ujumbe huo utagharimu sh.350 ambapo namba za simu za wachangiaji zitaingizwa katika droo itakayochezwa kila alhamisi pale Mlimani City katika duka la The Game na washindi watazawadiwa zawadi mbalimbali.
Aliongeza kuwa Chuo hicho kinatarajiwa kuanza kuchukua wanafunzi wa mwaka wa kwanza Oktoba mwaka huu na kitafundisha masomo ya Ualimu,Biashara na Teknolojia (IT).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. KAKA AHSANTE KWA KUTUPA HABARI ZA JOKUCO.
    NAOMBA UFANYE MASAHIHISHO YA MAMBO YAFUATAYO:-
    1. JINA LA ASKOFU NI ELISA BUBERWA
    2. JINA LA DAYOSISI NI KASKAZINI MAGHARIBI
    3. JINA LA CHUO NI JOSIAH .......
    KILA LA KHERI

    ReplyDelete
  2. Anony wa 13 MAR 08:09:00 Umeshafanya marekebisho wewe mwenyewe, asante kwa ,marekebisho
    Thanks

    ReplyDelete
  3. Hii inakuwa vipi sasa!!? Josiah Kibira ndio nani?! Na kwanini chuo kipewe jina lake, na michango tuchange sisi? Yeye mwenye jina atatoa ngapi katika hiyo gharama ya Billioni 1.3? Kama wote tunachanga sawa, basi natoa hoja kuwa JINA LA CHUO LIBADILISHWE NA KUITWA "THE UNIVERSITY OF TANZANIA, KAGERA." Asanteni ndugu wananchi

    ReplyDelete
  4. Asante kagera kwa maendeleo hayo, Mungu atujalie wote tushiriki kuchangia

    ReplyDelete
  5. THIS IS WONDERFUL, NAOMBA INFORMATION ZAIDI ILI KAMA SITAWEZA KU-TEXT NIWEZE KUTUMA MCHANGO WANGU KWA BARUA AU BANK. HIZI NDIZO NEWS TUNATAKA KUZISIKIA ESPECIALLY TULIOKO MBALI NA NYUMBANI NA NDIZO PROJECT WE WILL LIKE TO HELP FOR THE FUTURE OF OUR KIDS AND THE REGION ITSELF, MAENDELEO NDIYO YANAVYOANZA, VERY GOOD KKKT-MAGHARIBI.

    ReplyDelete
  6. Hawa waadishi wa miembeni....edit story kabla ya kuiandika. Ni Elisa Buberwa na Josiah Kibira University College

    ReplyDelete
  7. Wadau samahani, nna swali!
    hivi Mkoa wa kagera unavyuo vikuu vingapi?
    Mdau-Sumbawanga, Rukwa.

    ReplyDelete
  8. Mi nafikiri wangekifupisha na kuwa JKU.."Josiah Kibira University". Sometimes the name of the place helps to advertise itself.... My two cents

    Hivi kwa wale wenye contact za Bkb, Bukoba University iliishia wapi?? any updates

    ReplyDelete
  9. UNIVERSITY OF BUKOOBA HAITOOSHI BWAANAA, WAITU!!!!!

    ReplyDelete
  10. NAOMBA KUMJIBU ANAYELIZA KUHUSU CHUO KIKUU CHA BUKOBA.
    KAMA ULICHANGIA POLE SANA, FEDHA ILIISHIA MIKONONI MWA WENYE NGUVU MAJENGO NDIYO HAYO YAMETOLEWA KWA AJILI YA CHUO KIKUU HURIA.
    TUNAJITAHIDI SANA KUMUOMBA MUNGU ILI HILI JAMBO LIFANIKIWE NA KWA JINA LA YESU LITAFANIKIWA ILI TUSIJE KUTOA HISTORIA YA KUCHANGISHA PESA NA KUISHIA MIKONONI MWA WACHACHE. JoCUKO INAENDELEA VIZURI SANA UKAGUZI TOKA TCU UMEKAMILIKA TUNASUBIRI JIBU BILA SHAKA LITAKUWA POA. TUNAENDELEA KUWAOMBA KUCHANGIA.

    PIA KUNA ALIYEULIZA KIBIRA AMECHANGIA NGAPI...?
    HAIJALISHI CHUO KUPEWA JINA LAKE ISIPOKUWA NI KUENZI JINA LAKE KAMA WENGINE WENGI.

    MDAU

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...