Kampuni ya 4Layers (T) Ltd, Tuition Management Solution inaazisha mpango maalum wakuwawezesha wanafunzi katika ngazi zote kupata nafasi ya kusoma ndani ya nchi bila kujali, jenda, rangi, kipaji, wala alama za juu za masomo, ujulikanao kwa jina la NITASOMA Scholarships for NON and Merit Students.

4Layers (T) Ltd ni miongoni mwa kampuni chache nchini ambayo inajihusisha na utoaji wa huduma hususani katika maswala ya Elimu.

mpango huu umeanza rasmi leo tarehe 15.03.2010 , huduma ambazo kampuni hii itatoa ni scholarship kwa mashule na vyuo taasisi zote za elimu ya juu kwa ujumla vilivyopo nchini, pili ni pamoja na kutoa ushauri wa kitaalam kwa wanafunzi juu ya kuchagua masomo kwa shule za sekondari pia kuelimishwa jinsi kujiunga na mashule au vyuo na vitengo mbalimbali vya elimu na ufundi, mafunzo katika kuandika barua ya kuomba kazi , muongozo kamili katika kuboresha elimu kwa ujumla huduma hii itawalenga wanafunzi kuanzia shule za sekondari, vyuo vya elimu ya juu na vyuo vikuu.

NITASOMA Annual Career day ni siku ambayo wanafunzi watakutana na wataalam maarufu nchini ana kwa ana na kujadiliana kuhusu ubora, umuhimu hata matatizo ya ufanisi katika sekta hizo mbalimbali. Kwa kipindi cha mwaka tunatarajia kusomesha bure wanafunizi 6 kwa muda wote wa masomo na kutoa zawadi za Laptop 12, vitabu vya masomo au vifaa vya masomo kwa wanafunzi 12, simu ya mkononi 1 kwa wiki zawadi hizi ni kwa wanafunzi wale watakaoshinda kupitia bahati nasibu maalum.

Wanafunzi watakaofaidika na mpango huu ni wale tu watakao tuma ujumbe mfupi wa simu NITASOMA SEC au NITASOMA HIGH kwa shule za sekondari au NITASOMA UNI kwa vyuo vikuu kwenda kwenye namba 15767 na ataingia katika mchakato huo kwa gharama ya shilingi ya kitanzania 500 tu.

Zawadi hizo zitatolewa kwa awamu yaani laptop moja kwa kila mwezi. Simu ya mkononi kila wiki na vitabu kila mwezi tukizingatia masharti na vigezo.

Napenda kukumbusha tena mpango huu wajamii utasaidia kuwapa nafasi wale walioshindwa kwenda kusoma ndani na nje ya nchi kupitia nafasi za serikali na kwa wanafunzi walioshindwa kuendelea kusoma kutokana na gharama za masomo. Pia mpango huu utasaidia wanafunzi walioshindwa kupata nafasi ya kusoma kutokana na ushindani wa alam au nafasi maalum na wanafunzi wengine.

Kuhusiana na utaratibu wamalipo, 4 Layers (T) Ltd Tuition Management solutions kama kampuni itafanya malipo moja kwa moja katika shule au chuo husika na mwanafunzi atakayepewa ada ya masomo (Tuition fees)fedha za vitabu mkononi.
Naomba kumalizia kwa kumbusha tu mfumo huu utapunguza idadi ya wanafunzi wanao soma kupitia Bodi ya Mikopo kwani wengi wao huwa wanashindwa kulipa mkopo baada ya muda wa kusoma au hatakushindwa kukamilisha vigezo vya kupata mikopo hio.
Mshindi wa kwanza wa NITASOMA Scholarship kwa zawadi ya simu ya mkononi tarehe anatarajiwa kupatikana 22.03.2010 yaani jumatatu ijayo.

www.nitasoma.com





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...