baada ya kutonywa juu ya dhahama katika PPF Tower, Globu ya Jamii leo imetembelea jengo hilo mtaa wa Ohio jijini Dar na kukuta mambo nimswano kabisa, lifti zote zilikuwa zinadunda kama kawa na maji pamoja na viyoyozi vyote vilikuwa vikifanya kazi. Ikagundulika kuwa kumbe kulikuwa na tatizo kama inavyooneshwa kwenye hilo tangazao hapo juu. chini ni wadau kwenye lifi ambazo zote zilikuwa fiti. kumbe kuna wadau walifanya uzembe....



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. safi sana tunaona Glob ya jamii inafanya kazi.

    ReplyDelete
  2. Tafadhali Wahusika wameleke kiinglish kozi aliyeandika tangazo hilo.
    Si ni bora angeandika kiswahili tu.!!

    ReplyDelete
  3. anona wa 2 hapo juu hebu toneshe hayo makosa ya kiingereza.

    pia usisahau kukimbilia kukosoa lugha ni ishara ya kukosa hoja.

    ReplyDelete
  4. Blogu ya jamii, msitumike ki-marketing kusafisha wafanyabiashara wazembe ambao hawatoi huduma vizuri na zikilalamikiwa kwenye vyombo vya habari wanakimbia kutafuta vi-excuse na kujisafisha. Matatizo kama watumiji wa jengo hilo walivyosema hayakuanza leo, ni kwamba tu hayakuwahi kuanikwa kwenye vyombo vya habari kama hivi sasa. Watafute kwa kina cha matatizo yanayojirudia rudia ya lifti kuharibika mara kwa mara, uhaba wa maji maliwatoni, uwepo wa wadudu n,k na wayatafutie ufumbuzi wa kudumu, sio kujitetea kwenye vyombo vya habari kama hivi.

    ReplyDelete
  5. Ankal asante kwa kutujuza mambo mbalimbali,ila umechapia kidogo maana PPF House iko mtaa wa Samora na ile ya pale Ohio ni PPF Tower,inatokea kibinaadam kukosea lakini ila wengine tulishtuka sna na nilitaka mpigia ndugu yangu mmoja yuko PPF House na anafanya kazi ghorofa ya 9,lakini kabla sijafanya hivyo ndo nikagundua sio kule.

    Asante kwa kuendeleza libeneke.

    mdau.

    ReplyDelete
  6. Duh jamani kila siku hizo water tap zinaachwa tu au umeshapigwa mchanga wa macho maana hilo jengo lina matatizo kila siku...

    ReplyDelete
  7. PPF House liko barabara ya Samora.PPF Tower liko Ohio,umetuchanganya tuweke sawa ni jengo lipi unalilisema?

    ReplyDelete
  8. yaani hicho kiingereza ni aibu tupu,si waandike kiswahili tuu au watafute watu wanaoweza kuandika vizuri wawasaidie

    ReplyDelete
  9. TENAT ALIPOFUNGUA BOMBA NA KUONA KUWA HAKUNA MAJI, BASI AKAONDOKA ZAKE BILA KULIFUNGA...KWA HIYO MAJI YALIPOKUJA USIKU WA MANANE, BOMBA LILIKUWA WAZI NA MAJI YAKAELEKEA HUKO KWENYE ELEVATOR....MOJAWAPO YA KAZI YA MLINZI NI KUPITA PITA KWENYE KILA FLOOR NA KUANGALIA USALAMA, INCLUDING MABOMBA YALIYOACHWA WAZI NA TAA AMBAZO HAZIJAZIMWA.....BONGO TAMBARARE KAMA KAWA

    ReplyDelete
  10. Kilo ahsate kwa kuchangia ila kwa taarifa yako mabomba yaliyoachwa wazi ni ya jikoni na huwa wahudumu hao wanafunga kwa funguo maana huwa wanahifadhi vitu wanavyodhani kuwa ni vya thamani. Nilichotaka kusema ni kuwa kwa mtu aliye-responsible with his/her own action hatakiwi kuambiwa kuwa ukifungua bomba na kukuta maji hayatoki funga. Hii inaonyesha ni jinsi gani baadhi wa wapangaji wa jengo hili walivyo na ufinyu wa akili na kufikiria matokeo yake inatugharimu kupanda mpaka ghorofa ya 17 kwa ngazi. Wakati mwingine siwalaumu sana maana inawezekana kabisa ni wakaazi wa tabata au mbagala ambao hawajawahi kuona maji yanatoka kwenye bomba hata siku moja.

    ReplyDelete
  11. thegodfatherMarch 19, 2010

    We Hail Michuzi our Saviour.

    ReplyDelete
  12. Wewe unayempinga aliyekosoa Kiingereza huna hoja pia. Wabongo mmezoea kila kitu ubabaishaji tu ikiwemo lugha. Ukiwa mtaani kwenu tumia lugha unavyotaka lakini kwenye mawasiliano tumia lugha sahihi. Kama umeamua kutumia kiingereza tumia sahihi. Kifupi katika kiingereza hakuna kitu kinaitwa lift bali Elevator.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...