Katibu mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mshariki Balozi Juma Mwapachu akiongea na waandishi wa habari kuhusu mkutano wa Reli kwa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki utakaofanyika jijini Dar kuanzia kesho, dhima kuu ikiwa ni Uendelezaji wa mfumo wa usafiri wa reli kwa lengo la kudumisha ushirikiano, kurahisisha usambazaji wa bidhaa na kukuza uchumi za Jumuiya ya Afrika Masharikai na zile za SADC na COMESA.

Katibu Mkuu, Wizara ya Miundombinu Injinia Omar Chambo (kulia)akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es salaam kuhusu uimarishaji wa miundombinu ya reli katika Jumuiya ya Afrika Mashariki hasa ujenzi wa reli mpya kutoka Dar es salaam - Tanzania mpaka Kigali - Rwanda ambayo pia itaiunganisha nchi ya Burundi. Kushoto ni Katibu Mkuu, Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Stergomena Tax.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Reli ya kati wameshindwa kuimudu, wanataka wakimbilie reli ya afrika mashariki. Toka tanzania tumepatapango uhuru hakuna hata kiongozi mmoja mwenye mipango madhubuti ya kundeleza nchi.
    The leaders should seat down and analyze what do we need? and what we have to do? vinginevyo tanzania itaendelea kuwa kichwa cha mwenda wazimu siku zote.

    Mdau China

    ReplyDelete
  2. DUH HII SASA KASHESHE. RELI YETU YA KATI INATUSHINDA KUIENDESHA, HALAFU WAKUBWA WANAFIKIRIA KWENDA KULETA MAKUU MENGINE.
    YANGU MACHO.

    ReplyDelete
  3. Ndege ya ATCL yapata hitilafu angani

    Na Muhibu Said

    9th March 2010B

    Ndege ya Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), juzi ilikwamisha safari ya maofisa kadhaa waandamizi wa serikali waliokuwa wakienda mkoani Tabora kuhudhuria kilele cha maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani.

    Ndege hiyo iliondoka jijini Dar es Salaam juzi ikiwa imewachukua maofisa hao wa serikali, lakini ililazimika kurudi njiani baada ya kupata matatizo ya kiufundi wakati ikiwa angani.

    Baadhi ya maofisa hao wa serikali (majina tunayo) waliozungumza na Nipashe jana, walithibitisha ndege hiyo kupatwa na hitilafu wakati ikiwa angani na hivyo, kulazimika kukatisha safari na kurejea jijini Dar es Salaam.

    Hata hivyo, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa ATC, William Haji, alipoulizwa jana na Nipashe alisema tatizo lililoisibu ndege hiyo halikuwa kubwa kama linavyokuzwa.

    “Kama kungekuwapo na hitilafu ningejua, lakini kama lilikuwapo, ni mambo ya kurekebishika tu,” alisema Haji.

    Alisema kilichotokea kwa ndege hiyo, ni kuchelewa muda wa kwenda mkoani Kigoma, ambao mwisho wake ni saa 9:00 alasiri, jambo ambalo lililazimisha safari hiyo kusitishwa kwa vile kuna tatizo la taa za uwanjani.

    Hata hivyo, alisema siku hiyo hiyo, ndege hiyo ilikwenda mkoani Mwanza, kwa kuwa uwanja wake una taa na jana ilikwenda Kigoma na kuongeza kuwa mzigo wa gharama za kuwahifadhi abiria waliokwama kusafiri, ulibebwa na shirika.

    Maadhimisho hayo, ambayo kilele chake kilihitimishwa katika uwanja wa mpira wa Ali Hassan Mwinyi, mkoani humo, yaliyohutubiwa na Rais Jakaya Kikwete.


    CHANZO: NIPASHE

    ReplyDelete
  4. Tullow says profits have been hit by falling oil prices

    Exploration and production firm Tullow oil says profits for 2009 were down 93% but it has made oil discoveries and upgraded prospects in Ghana and Uganda.

    Pre-tax profits for the year ending in December 2009 were £20m ($30m), against £299m the year before.

    Tullow said it was hit by lower oil and gas prices, and sterling's weakness.

    Chief executive Aidan Heavey said the results "reflect a period of financial transition", and that Tullow was planning up to 30 new wells in 2010.

    Deals imminent

    Tullow's assets are mainly undeveloped oil fields and land held for exploration.

    More data on this share price
    They estimate their prospects in Ghana, including a new find at Tweneboa, equate to 4.5 billion barrels of oil.

    And they hope to see the first oil from the $3.1bn (£2.1bn) Ghanaian Jubilee field by the end of this year.

    In Uganda, Tullow say they have identified over 800 million barrels of oil, and highlighted a major 300 million barrel discovery at their Jobi-Rii field.

    Tullow said French oil firm Total , as well as Chinese state-owned China National Offshore Oil Corporation, will partner it to develop the Ugandan Lake Albert Rift Basin fields that it was formerly developing with Heritage Oil.

    In a statement Tullow it expected the transactions "to be signed in coming weeks".

    And they hope to see commercial oil production from Uganda from 2011.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...