KAMPUNI YA KIMATAIFA YA UHUSIANO,
INATAFUTA AFISA HABARI (PR EXECUTIVE) .
SIFA :
*AWE NA SHAHADA AU STASHAHADA KUTOKA CHUO KINACHOTAMBULIWA NA SERIKALI.

*AWE NA UZOEFU USIOPUNGUA MIAKA MIWILI
AWE NA UMRI USIOZIDI MIAKA 30.

*AWE NA UWEZO WA KUZUNGUMZA NA KUANDIKA KWA UFASAHA LUGHA ZA KISWAHILI NA KIINGEREZA

*ANAYEJIHESHIMU

KAMA UNA SIFA HIZO,
PIGA SIMU NAMBARI
O767 882250

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Kampuni, kama imetoholewa kutoka neno "Company = an organization which sells goods or services in order to make money"

    Hivi kampuni kama hii "KAMPUNI YA KIMATAIFA YA UHUSIANO" itakuwa inajihusha na biashara gani?

    ReplyDelete
  2. hadi leo bongo kuna age discrimination??? lol..mtaishia kudiscriminate wakati nchi nyingine zinasonga mbele...bongo tambarareeee.

    ReplyDelete
  3. Umri usizi miaka 30..!! Halafu Watanzania wakijiminya huku nje kupata maisha mnawaona sio wazalendo..!!

    Ole wenu nyie mnafanya ubaguzi Tanzania.

    ReplyDelete
  4. Age Discrimination

    ReplyDelete
  5. MDAU UMESHASEMA KAMPUNI NI CHOMBO KINACHOUZA BIDHAA AU HUDUMA SASA UNAULIZA NINI, GOODS OR SERVICES, SASA HII KAMPUNI INAUZA HUDUMA=SERVICES SHULE JAMAA NI MUHIMU.

    ReplyDelete
  6. Ngoja mimi nijibane humu humu. Nimesota kujisomesha kadegree na kamasta kangu nilikua nahamu sana ya kurudi bongo lakini kama ndio mambo ya kuambiwa umri usizidi miaka 30 namimi by the time nachukua nondo yangu nitakua na umri wa miaka 30 na siku tano.....owiiiii sirudi ng'oooooo

    Wenzenu wanasema ujuzi unauza nyie mnang'ang'ania umri sijui hivi, umri sijui vile akija mtu mwenye qualifications zote na umri umezidi mtamchukua asie na lolote just because yupo kwenye umri unaoutaka....Poleni na fikira zenu za kikoloni poor third world.

    ReplyDelete
  7. Kazi ipo, mtu unaanza shule na miaka 6 (waliobahatika), unapiga kitabu hadi form four ushaguza 18, unakwenda form five and six miaka miwili tayari ushakata 22. unaingia university unajikuta una 25, unajisukuma kupata masters tayari una 26, unarudi nyumbani kutafuta kazi cv kila mahali hadi unapata kibarua una miaka 27/28 utapata wapi experience ya miaka mitatu halafu wakati huo huo unapewa age limit ya kuomba kazi kuwa miaka 30?

    Hii ni age descrimination, kuna nchi tele duniani siku hizi mwajiri hata haruhusiwi kuuliza suali la umri kwa muombaji kazi ili kuepusha ubaguzi wa umri.

    umuhimu wa ajira ni work experience na ujuzi sio umri.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...