Mazishi ya Kiongozi wa Wapiganaji Prof. Karim Hiji aliyezikwa makaburo ya Njiro jana. Picha hizi ni wakati wa sherehe za kuuaga mwili wa marehemu kwenye viwanja vya General Tyre zilizokusanya maelfu ya watu kutoka Arusha na kwingineko nchini na hata Malawi, Kenya na Rwanda.

Famili ya Marehemu Prof. Hirji. Katikati ni mkewe akiwa na watoto wawili wa kiume na mmoja wa kike na shemeji yake Firoz (nyuma).

Waliokaa kuomboleza kutoka kushoto Mr. Tesha, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege, Mbunge Seleli na Mr. Michael Shirima, Mwenyekiti wa Precionair.

Baadhi ya waombolezaji waliofurika viawanjani hapo.

Baadhi ya viongozi wa Arusha Wazee Sports Club ambayo marehemu alikuwa mwanachama. Kutoka kushoto Mzee Kasori, Mzee Danford Mpumilwa (mwenyekiti) na Mzee Mike Taylor.

Mwenyekiti mwanzilishi wa Arusha Press Club Danford Mpumilwa akiuaga mwili wa marehemu Prof. Hirji ambaye wakati wa uhai wake alikuwa Mlezi mwanzilishi wa Club hiyo kongwe na
ya kwanza ya waandishi wa Habari mikoani. Picha zote na Ripota wa Globu ya Jamii, Arusha
Mzee Danford Mpumilwa na wazee wenzio wa Club ya Wazee nawapeni pole sana kutokana na msiba wa mzee Hirji. I am sure wengi wetu tutamiss jokes zake ambazo zilikuwa zinatupatia uhai kila jumapili tunapokuwa tunacheza mpira pale General Tyre au siku nyingine tukiwa pale AICC club kijenge tukitia stori. Poleni sana. Hata hivyo mwenzetu katangulia kama wazee wenzetu wengine waliotangulia kama akina Geho na wengineo. Kifo ni sehemu ya mchakato wa maisha. Kifo siyo laana wala balaa. Tumshukuru Mungu wetu aliye hai. Amen
ReplyDeletePoleni sana wafiwa!
ReplyDeletePoleni wafiwa. May he rest in eternal peace.
ReplyDelete