Nahodha (Commodore) wa Yacht Club, Commodore Spiros Manolouis (kushoto) akitoa zawadi kwa Niels Sulzer, mmoja wa watoto walioshinda mashindano ya Vodacom Closing Regatta 2010 yaliyofanyika Yacht Club, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Yalidhaminiwa na Vodacom. Nahodha (Commodore) wa Yacht Club, Commodore Spiros Manolouis (kushoto) akitoa zawadi kwa David Scott mmoja wa washindi katika mashindano ya Vodacom Closing Regatta 2010 yaliyofanyika Yacht Club, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Yalidhaminiwa na Vodacom
Taswira za chini zinaonesha waendesha mashua wakichuana vikali ili kumpata mshindi katika mashindano ya Vodacom Closing Regatta 2010 yaliyofanyika Yacht Club, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Yalidhaminiwa na Vodacom.






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Hawa Voda baadala wadhamini ligi za mitaani ili waibue vipaji mbalimbali tena ndo kuna wateja wengi kuliko huko kwa hao wadosi wa mashua, maana kwanza wanamshiko, sitaki kuendelea.

    Mdau wa michezo ya kila aina kasoro Mashua!

    ReplyDelete
  2. Hivi wadau mnaelewa kuwa Yatch club wanalimit waswahili kwa kuweka kiwango kikubwa cha membership, yaani kuna wa ubaguzi wa aina fulani ukienda kumejaa wazungu, wametenga hiyo beach kwa ajili ya wazungu tuu. Kaka Michu hebu jaribu kwenda,utatolewa geitini tena wakikuona mswahili wanakwambia bei ya hapa huiwezi wewe nenda Slip way.

    ReplyDelete
  3. eheee pale yatch club ukiwa mswahili mlinzi anaanza kukutazama kwa jicho la chuki kama vile umekuja kuharibu starehe za waheshimiwa wake..utasikia `we memba? kama sio memba ondoka haraka! au utasikia hakuna kazi hapa..sijui wanadhani waswahili wote wanaenda kwa ajili ya kutafuta kazi za uhudumu,upishi au ulinzi,..lakini inabidi kuanzisha ya kwetu tuiite WITCH CLUB ngalawa na mitumbwi si ipo jamani,mamalishe wapo,vinywaji vyetu vya asili kama kindi,dengerua,pingu vipo kwa nini tubaguliwe na sisi tuna vyetu....

    ReplyDelete
  4. VODACOM ACHENI UTAPELI WA KUTOA SMS TANO ZA BURE KISHA MTEJA ATUMIAPO HIZO SMS MNAKATA SALIO LA MTEJA. PIA MTEJA AINGIAPO KWENYE CHEKA TIME HUWEZA AKAPOTEZA PESA YAKE BILA SALIO KUONEKANA KISHA MNAJIFANYA MMEGUNDUA TATIZO NA KUAHIDI KUMFIDIA LAKINI HAMTIMIZI AHADI, MJUE KUCHUKUA PESA YA MTEJA BILA SABABU ZA MSINGI NI KOSA.

    ReplyDelete
  5. Yatch club ndio ya wakoloni waliobaki tz

    ReplyDelete
  6. Nilijua tuu!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...