Mmatumbi mwenzetu Mohamed Iddi a.k.a Moody Spen (pichani kulia) anatuwakilisha na kuitangaza nchi kwa njia ya sarakasi na vichekesho kwa mafanikio makubwa huko Ujerumani na visiwa vya spen na Green Canary Las Palmas akiwa na kikundi kiitwacho Lanzate Entertainment na kampuni zingine zinazoshughulika na burudani hiyo. Anasema kajifunza mengi huko na anajiandaa kuja kugawa ujuzi kwa wabongo wenzie hapa nyumbani

Akiwa hapa nyumbani Moody amewahi kupitia vikundi mbalimbali ikiwa ni pamoja na cha Muungano Cultural Troupe chini ya Norbert Chenda, DDC Kibisa chini ya Mama Salma Moshi na pia alipita kundi la Makutano chini ya marehemu Mzee Ghazabu kabla hajaajiliwa na shirika la Bima kama muanzilishi wa sarakasi upande wa Bima Modern Taarab ambapo wakati mwingine kundi la TATUNANE lilikuwa likichukua sarakasi hiyo kwenye maonesho hoteli za New Africa na Bahari Beach.


moody na wenzie wakiwa na mtazamaji jukwaani
Moody akifanya vichekesho na wenzie
Moody na staili ya kichwa kwa kichwa
kukurukakara...







Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Pesa inaweza kukufanya mjinga...zile sehemu zote za kutisha wamempa yeye.

    Mdau
    London

    ReplyDelete
  2. Mtoto wa Coast, pata 5 nakufagilia. Naona wapangaji wamehama kichwani mwa huyo mpiga boooksi wa Londoni. Fikra zake zinayumbe kiaina hivi. Inabidi tumpepee uuf uuf! labda wapangaji watarudi.

    Mdau, Algeria

    ReplyDelete
  3. Huyo jamaa ni mahiri ndio sababu akapewa sehemu zote zinazohitaji ujuzi na uzoefu ni si kwamba kwa sababu mzaramo basi panda juu ukaanguke,we mdau wa london kazi yako ni nini? inaonekana unapewa kazi za hatari kutokana na kuwa na uelewa mdogo,sijui unafanya `odd jobs` ndio maana kazi za sanaa unaziona za hatari,endelea kukaa uwani ukukwangua masufuria tu huko london!
    MZAZI.

    ReplyDelete
  4. Mtoto wa CoastMarch 25, 2010

    Mdau Algeria,
    Tuko pamoja tuendelee kuelimisha vijana wanaoleta uhalo wa kauli humu ndani.
    Nami nakurudishia 5 ndugu yangu!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...