Naitwa Iddy Tendega ni mtanzania na mkaazi wa Kinondoni B.
Tarehe 25 mwezi wa kwanza mwaka 2009 bwana Elias aliyekuwa mfanyakazi katika kampuni ya longhorn Publishers Tanzania Limited alinipa taarifa kuwa kuna nafasi katika position ya sells representative.
Tarehe hiyo hiyo 25 niliandika barua ya kuomba kazi na kuiwasilisha kwa bwana Geofrey gituki ambaye ni country manegal wa Longhorn.Baada ya kuisoma aliniita kwenye usaili na siku hiyohiyo aliniuliza kama niko tayari kuanza kazi nikamjibu kuwa niko tayari.
Nilianza kazi kwa makubaliano kuwa atanilipa mshahara wa shilingi laki mbili kila mwezi na posho ya shilingi elfu kumi kilasiku(maana nilikuwa nikizunguka kwenye shule mbalimbali na bookshop hapa dar na nje ya dar).
Alinipa id no LP/C/7 POSITION EDUCATION SELLS REP, nilifanikiwa kupata oda kwenye baadhi ya bookshop na shule na kwa kipindi cha wiki moja ya kwanza boss alikuwa akinitimizia malipo kama tulivyokubaliana.
mambo yaligeuka mwezi wa pili kwani mwanzoni mwa mwezi boss aliniita na kuniambia kuwa nijikopeshe pesa ili inisaidie katika kazi yangu kwani hakuwa na bajeti ya kutosha hivyo atanilipa baada ya kupata pesa kutoka headquotor Kenya.Nilikubali na kuendelea na kazi kwa mafanikio kwani nilikuwa nikipata oda za kutosha.mwezi wa tatu nilimuaga boss na kumwambia nataka nikajaribu kutafuta masoko ya vitabu vyetu mikoa ya Iringa na Mbeya.
Niliondoka nikijitegemea kwa kila kitu kwani bado boss wangu alidai hajapata pesa kutoka makao makuu.Nilifanikiwa kutembelea shule za Iringa kama star internation school,ipogolo pr schoo na nyingine nyingi pamoja na bookshop za lutengano investment,maliyabababookshop na nyinginezo.
Kisha nikaenda Mbeya ambako pia nilizulu shule nyingi na bookshop kama Panache bookshop.huko kote nilipata oda na kurudi dar ili kuchukua mzigo na kupeleka kwa walengwa.Niliporudi dar na kutoa ripot kwa boss,alisema mzigo atapeleka mwenyewe mimi sikuwa na wasiwasi nilijua kamisheni yangu atanipa kama tulivyokubaliana.
Kitu kilichonistua ni kuwa baada ya boss kurudi nilimuuliza kuhusu malipo kwa mujibu wa oda alizopeleka lakini alisema hawezi kunilipa kwani yeye ndio aliyepeleka.Nilipatwa na mshtuko nakudai haki zangu za mwanzo boss alisema hawezi kunilipa chochote kwani nina deni la shilingi laki mbili ambazo nilimkopesha mteja vitabu.
Nilipoendelea kumuasa anilipe alinijia juu na kuninyang'anya simu yangu ya lain mbili na fedha elfu ishilini akidai anafidia deni.
Nilichanganyikiwa kabisa na kwenda kuomba msaada wa kisheria Human legal kinondoni na kufungua JALADA # 09/696 ELEMENT UNIT.
Baada ya kuwasilisha dokment zote mwanasheria aliniomba nimpe muda apitie na kuahidi kunisaidia.Bahati mbaya ilikuwa ni karibu na rikizo za wafanyakazi wa human legal hivyo ilinipasa kusubili mpaka likizo itakapokwisha.
Baada ya likizo kuisha nilienda kwa mwanasheria na kumuuliza mwenendo wa madai yangu lakini alinijibu kuwa sheria za masuala ya kazi zimebadilika hivyo kulingana na mabadiliko hayo ni vigumu mimi kushinda kesi hiyo.namnukuu"no way you can win this case it is better to leav"
Nimeamua kuandika ili kuomba msaada kwa taasisi zinazoshugulika na haki za binadamu ili mimi nitendewe haki zangu.

YOTE NILIYOANDIKA NI UKWELI NA MUNGU ANISAIDIE.

IDDY YAHAYA TENDEGA
Email:iddy20@yahoo.com
cell:+255719283959

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 14 mpaka sasa

  1. Nyangau akionea mwananchi, pole sana mzee ukishindwa mtafutie watu wamfanyizie mtaani

    ReplyDelete
  2. unajua watu wengine wanachezea sana wenzao,nahisi kutetemeka hapa njinapoandika msg hii maana kama angenitendea mimi hivyo sijui kama ningeweza kuvumilia,jamani serikali mko wapi na hizo sheria zilizobadilika je zinamruhusu mtu kufanya ujinga wa kudhulumu mtu na kuondoka bila ya kushitakiwa,mmmh tanzania sio nchi ya kuishi kabisa,wala sitaki kurudi walahi,na wewe muajiriwa umeona wapi kampuni inasema jikopeshe mwenyewe sh 10000 huoni hapa ni ujanja ujanja tu?

    ReplyDelete
  3. 1. Makubaliano yoyote ya mikataba yawe kwa maandishi. 2. Ukiwa ni sales representative sharti uwaeleza wateja wako kuwa wewe ndiye mwakilishi ulioiipatia dili kampuni na hivyo kama kuna ubishi wateja ndio watakuwa mashahidi wako. 3. Usiwaamini sana watu kupita kiasi, hususan baadhi ya jamaa zetu kutoka nchi jirani. 4. Endelea kugombea haki yako bila kujali huyo wakili aliyekukatisha tamaa.

    ReplyDelete
  4. HIYO SIO SOLUTION, MUANDIKIE RAIS KIKWETE, AU NENDA IKULU, WATU KAMA HAWA NI WAONEVU WANATAKIWA KUSHTAKIWA JAMA! NA SIO KUACHIA TU! FIGHT MPAKA MWISHO KAKA.

    ReplyDelete
  5. UKINYANG'ANYWA SIMU NA PESA UNATAKIWA UENDE POLISI KUFUNGUA MASHITAKA.

    ReplyDelete
  6. Najua umeonewa lakini ngumu kwako ushahidi wako ni wa kimazingira tu..itakua shida kumtia hatiani huyo bwana unless kama una documentations flani

    ReplyDelete
  7. The Nasty HR LadyMarch 18, 2010

    kama una mkataba wa maandishi au hata oral contract ( nayo inatambulika ) nitumie email nitakusaidia/ na kukuelekeza free of charge kudai haki yako, tatizo ni kuangalia kama bado uko within time kupeleka madai hapo CMA
    actually sheria za kazi ziko wazi kabisa
    email us at info.hrct@hrct.co.tz

    ReplyDelete
  8. Mshtakie Mungu.

    ReplyDelete
  9. Pole sana kaka,ushauri kwa wote ni Marufuku kujitolea kazi,acha kuvolunteer kazini,ujiukopeshe imetoka wapi?kama hakuna pesa hakuna kazi,vifaa chini.Mkataba muhimu sana baina ya muajiri na muajiriwa,wengi wanapoteza haki kwa kukosa mikataba,hata wenye mikataba haiko mizuri kwao,tuko desparate tunahitaji kazi hivyo uwa utangalii sana mambo haya ni hatari.

    ReplyDelete
  10. kaka Idd Tengana,.

    ninaweza kukupa ushauri wa kisheria katika suala hilo, lakini taarifa zako muhimu hujatupatia, ambazo ni kama zifuatazo,

    a) je baada ya kukunyanganya simu na pesa hitma yake ilikua nini? alikwambia kakufukuza kazi au? i mean nini kiliendelea...maana umesema tu ukaenda kituo cha sheria lakini hujaeleza status ya mwajiri wako kazini ilikuaje?.i disclaim from liability for anything so stated.


    b) Umesema ulianza kazi 25/01/2009... ulimaanisha 2009 au 2010. naomba uwe wazi hapo.

    c) hujaeleza hilo deni la vitabu kama ulikua unadaiwa na mwajiri wako.

    pamoja na hayo kuna dondoo zifuatazo; zitakozochochea mwanga fulani katika shauri lako hilo, nazo no kama zifuatazo,

    1. JE ULIKUA NA MKATABA HALALI WA AJIRA?
    kifungu cha 14(2) Sheria ya kazi na mahusiono kazini ya mwaka, 2004 Wazi kwamba mkataba wa ajira unaweza kua aidha wa maandishi au wa mdomo. lakini kama unaajiriwa nje ya Jamuhuri ya muungano wa Tanzania sharti uwe na mkataba wa maandishi, si wa mdomo.ie;kama hukupatiwa mkataba ulikua na mkataba wa mdomo ambao una nguvu sawa na ,kataba wa maandishi; the weight of oral contract is as good as written contract.

    2. JE HADHI YAKO ILIKUA KAMA KIBARUA/MWAJIRIWA?

    ndugu, katika hili kuna mambo mengi hujafafanua?ulifanya kazi kwa muda gani? umesungumzia toka mwezi wa 1-3.lakini ili kujua kama ulikua kibarua au mwajiriwa..hili ni nuhimu katika stahili gani utapata.. kifungu cha 61 cha Labour Institution Act kinazungumzia suala hili. nitakufafanulia zaidi tukiwasiliana.



    3. JE MWAJIRI ALIKUA NA HAKI KUKUNYANGANYA SIMU NA PESA?

    katika suala hili, Kifungu cha 28(2), cha sheria ya ajira na mahusiano kazini, kinazungumzia makato halali ya ujira wako kulipoa upotevu /hasara ulioufanya.( japo hujafafanua zaidi) kama kweli ulikopesha vitabu au la...nikipata mwanga hapo ntafafanua.

    4. JE SHAURI LAKO LINA NGUVU YA KISHERIA?
    hili ni suala la mzingi sana, maana ulesema umeanza kazi toka 25/1/2009 na mgogoro ukajitokeza baada ya miezi 3 ambapo ni kama mwezi wa 4/2009. na leo ni 18/03/2010. kuna ukomo wa kisheria wa kupeleka mgogoro sehemu husika...je ulikua wapi toka 2009 mpaka leo 2010????

    sheria inatoa siku 30 kupeleka malalamiko yako kwenye tume ya uamuzi na usuluhishi>> sasa naona kama you are tie barred.

    nina mengi sema muda mchache,

    fmuna@Breakthru.com--nitumie dondoo zote nikusaidie kwa ushauri.

    ReplyDelete
  11. POLE KAKA, MFUNGIE SAFARI BAGAMOYO NDUGU YANGU.

    ReplyDelete
  12. Pole kaka.Hayo ni majambo ya mjini ila dawa yake huyo we muendee Pangani ukamshushe busha.

    ReplyDelete
  13. MTAFUTE UMPIGIE KELELE ZA MWIZI

    ReplyDelete
  14. pole sana kaka,, ungekuwa ulaya lazima ungekuwa na National Insurance,, its enough to establish that u have worked for him, for how many hrs and from when,, tena kama ajira ingekuwa ya mazabe na fine angelipizwa vile vile, ila according to the info na vitengo vya sheria alivotamka "the nasy HR Lady hapo juu,, think utapata haki zako sometimes mambo kama haya yanatufanya na elimu zetu tuogope kurudi home,, ah when is the government gonna make some changes in these areas,, hii ni story ya nne nasikia about boss ku treat watu vibaya, the first one was the lady who worked at the Kilimanjaro sijui ndo kempisky,, heheheh ingekuwa mie huyo bosi angejua kuwa "HIKI NI NINI NA NANI KALETA,," JASHO LA MTU HALILIWI,, MDAU UK...

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...