Naomba msaada wa ufafanuzi wa
Jambo Hili nimepokea mail asubuhi hii
kuhusu mada hiyo hapo chini
Mdau Rajupal
Matumizi ya ARVs kukuzia kuku??
Kwa mujibu wa matokeo ya uchunguzi wa kitabibu, baadhi ya kuku wa kufugwa wanaoingia sokoni wamekuzwa kwa kutumia ‘utundu’ wenye hatari wa baadhi ya wafugaji wasio waaminifu kwa kulisha mifugo hiyo dawa za ARV ambazo huwafanya kuku hao kuonekana wakubwa na wanene kwa muda mfupi.
Uchunguzi huo unakwenda mbele zaidi na kubainisha kwamba, tabia za dawa hizo ambazo ni kujenga mwili na kuimarisha kinga ya magonjwa kwa mwathirika wa Virusi vya Ukimwi, ndiyo inayompata mlaji wa kuku hao.
Inadaiwa kuwa, kuku hao wanapokula chakula kilichochanganywa na dawa hizo, huweza kutumia siku kumi na mbili hadi kumi na nne kutoka kuwa vifaranga hadi utayari wa kuingizwa kwenye soko la walaji.
Ili kukamilisha uchunguzi huo, Amani lilituma makachero wake maeneo ya Kibamba, nje kidogo ya Jiji la Dar ambapo ndipo kwenye viwanda vya kuzalisha kuku wa ‘sampuli’ hiyo.
Kwa mujibu wa kijana mmoja ‘profesheno’ wa kutunza kuku katika moja ya nyumba maarufu kwa uzalishaji maeneo hayo, ambaye hakutaka jina lake lichorwe kwenye ‘pepa’ hii, alikiri kuwepo kwa ishu hiyo, lakini alibainisha kuwa hajui bosi wake anapochukulia vidonge hivyo vya ARV’S.
MADHARA:Kwa mujibu wa Daktari mmoja wa Hospitali ya Taifa Muhimbi ambaye aliomba hifadhi ya jina lake, mtu anayependa kula kuku waliokuzwa kwa kutumia ARV na yeye huanza kunenepa kupita kawaida, lakini uzito unaweza kuwa tofauti na unene ‘boya’.
Mtabibu huyo aliongeza kuwa, watoto wengi wanaozaliwa siku hizo ambao wazazi wao wamekuwa watumiaji wazuri wa kuku, hukua haraka kiasi kwamba, mtoto wa miaka 18 huonekana kama ana miaka 27.
Aidha, alidai kuwa, wengi ambao kuku hao wamekuwa chakula chao kikuu, hufika mahali wanakuwa ‘legelege’ katika utendaji wa kazi wa kila siku tofauti na zamani huku sehemu kubwa ya chakula hicho ikiangamiza ‘pati’ ya subira na uvumilivu na mlaji kuwa na hasira.
Dalili nyingine ni mtu kuhisi muda wake wa kuchoka unakuwa mfupi akilinganisha na zamani na wakati mwingine hali ya kuhisi kusinzia humtawala hata kama anafanya kazi
SASA UNATAKA MSAADA GANI?????? - ni nini usichokielewa hapo
ReplyDeleteSTUPID!!!!
ReplyDeleteARV'S are controlled drugs na hazipatikani kama njugu za mitaani.
This is a poor piece of literature inayofikiri wasomaji are just as stupid
NOTE:utawapa kuku wangapi hizo drugs economically hata kama unaziiba hospitali ili uweze kufuga kibiashara?
STUPID!!!
You're more than a stupid!!!
ReplyDeleteMbona its easy kupata majibu? Kwani bongo hakuna maabara ya kufanya test za hao kuku wanaoshukiwa. Iam telling you viwango sijui au kampuni iliyo responsible kuhakikisha nyama zinazouzwa hazina madawa yanayohatarisha miili ya binaadamu ipo wapi. Inatakiwa wafanye suprise ukaguzi na kutest kuku kwenye masoko na atakayekamatwa apewe adhabu kali ili iwe fundisho kwa wengine. Bongo watu wanakula na vyakula na kusurvive kwa kudra ya mungu. FDA ya bongo hivi inafanya kazi kweli sijui ndiyo inaitwa viwango or something. BONGO TAMBARARE MWEEEE!
ReplyDeleteKwanza mbona Madhara yake sio mabaya sana hayatishi,mimi angesema unapata cancer au ni sumu unakufa hapo sawa,sasa ukiniambia mtoto wa miaka 18 huonekana kama ana miaka 27 huo ndio utafiti gan huyo Dr.atakua ni wa darasa la saba au watakua ni wakina Sheh Yahya.
ReplyDeleteNyie mnaosema stupid nyie ndio stupid wakubwa.
ReplyDeleteHuyo kaleta ili kuwa kama kuna mtu anaweza kufafanua hii aeleze, au kama kuna ukweli ndani yake basi tuelezwe.
Mnasema madhara sio mabaya...mtanenepa nyie mpaka mkome.
na mkisema control hazipatikani unajua ni watu wangapi wanaweza kuuza dawa? Na pia ni wangapi huku tunandugu walioathirika na tunazituma hizo dawa nyumbani kila siku kwa wingi tu.
Msitupie chini haya mambo. Hata kama si kweli labda kuna watu wanaoanza huo mchezo.Serikali inatakiwa kuamka kabla haijawa janga kwa nchi...
Hao walioandika kuwa alioandika ni stupid yeye ndiyo mjinga kabisa, hakusoma wale wenye viwanda waliotengeneza maziwa yaliowadhuru watu china walivyonyongwa. Waliopingana na maelezo yaliotolewa wanaonyesha ndiyo wafugaji wa hao kuku wenye kupewa ARV's. Hakuna kitu kisichopatikana katika mahospitali yetu hapa Tanzania ilimuradi uwe na ndugu, rafiki anafanya kazi huko au pesa yako? ARV's zina madhara mengi saana inabidi wafugaji wachunguzwe na kama itadhihirika wanatumia dawa zozote zenye madhara wapelekwe katika vyombo vya sheria kushtakiwa
ReplyDeleteIDIOTS kabisa!!!mbona vi-madhara vyote ni POSITIVE kwa apa kwetu???
ReplyDelete1. io ya madogo wa 18 yrs kuonekana wana age ya 27 itatufaa sana kwenye KILIMO KWANZA (tutakua harakaharaka)
2. io ya kusinziasinzia pia itatusaidia kuendana na ma-STRESSES ya maisha ya bongo(unakula zako vi-KUKU viwili unalala)
3.io effect ya kuleta HASIRA ndo nzuri sanaaa....unapiga zako vi-kuku ka vi-5 ivi apo ukikutana na FISADI barabarani wala hujiulizi mara mbilimbili ni KICHAPO tu!!
NAWASILISHA>
Hao wanaosema STUPID naona wamefilisika kiakili naona nao wameathirika na kuku wanaotumia ARV. Hapa serikali ifanye uchunguzi kupitia vyombo vyake. Lisemwalo lipo. Vinginevyo na hao mastupid wataathirika kama sio wao ni watoto wao.
ReplyDeleteMdau azliyeleta hii mada nampa big up. Hii ni kitu muhimu kuijadili hao wanaosema stupid tusiwajali. Hii tunaomba msaada wa wataalam. Selikari pia itoe tamko. Sasa bongo tunahitaji adhabu kama za wachina "hukumu za vifo" huku ni kuchezea afya za binadamu kwa tamaa za fedha.
ReplyDeleteKama Kuku wanapewa ARV's basi mbona imetulia sana tu maana, itawafaa sana wagonjwa na itakuwa ni dozi tosha. KINGA NI BORA KULIKO TIBA kula vijiKuku vilivyo na ARV na usiwe na wasi wasi wa kuvaa Kondom
ReplyDeletemdau wa kugawa DOZI
Jamani msifanye utani haya mambo yapo kabisa tena hadi mikoani hadi vijijini.
ReplyDeleteNilikuwa nikiishi Njombe miaka miwili ilopita, basi kuna siku nikaona kuku wanauzwa kwenye tenga ila ndo hao wanaoitwa wakisasa, nikanunua kuku kwa muonekano alikuwa mzuri tu.
Nilipo mchinja ile kuanza kumnyonyoa manyoya tena bila kumchelewesha akaanza kuoza kuanzia nyuma ashakumu si matusi (matakoni) na kutokea rangi nyeusi.
Nika amua kumtupa kwakuchimba shimo na kumfukia kabisa kwani nilihisi ni sumu kwa kiumbe atakaekula na kusahau 5,000/= yangu.
Wafugaji jamani mtunusuru walaji wa vyuku kwani mnaua hata ndugu zenu.