Ankal wasalaam aleykum.Naomba msaada tutani,jamani mi nataka kununa gari aina ya TOYOTA GAIA, naipenda sana hii gari ila kiukweli cfahamu kama ni gari nzuri au vipi i mean kwenye maswala ya spare na kila kitu. Naombeni maoni yenu na ushauri wenu wanalibenke ambao mnaexperience na TOYOTA GAIA.
Asanteni
MDAU


we nunua tu spear zipo tu mitandao kibao we hujui tuko enzi za utandawazi?/
ReplyDeletemdau hiyo gari ni nzuri sana , engene yake ni 3s ina maana inakula mafuta kidogo sana, inachukua abilia 7 ukiondoa dereva ina leather seat kwa kweli ni gari nzuri kwa familia, mimi ninayo nyeusi ya mwaka 98 na bado sijaisajili ila imelipiwa ushuru wote...kama unaitaka piga simu namba 0713 541786
ReplyDeletemdau, mimi nilinunua gaia 2yrs ago,Nilimwachia mtu, nimetoka nyumbani Juzi ile gari imekwisha kabisa, sasa sijui ni gari au mtumiaji. Nilijaribu kuikarabati inaingiliana spea za ndani na RAV4, lakini za nje(yaani body) hakuna, iligongwa taa za nyuma hadi leo sijata za kubadilisha. Imechakaa mfano wa mabaloon yanavyochakaa. Fanya utafiti zaidi kabla ya kuinunua.
ReplyDeleteHongera sana mdau kwa kutafuta msaada kutoka kwa wadau.Suala la spea ni la pili lakini la muhimu ni kuagiza gari kutoka kwa wauzaji hakika kule Japani.Iwapo utafuata vigezo vya utafutaji na uagizaji utaifaidi gari kwa wakati kabla ya kuanza kutafuta spea ambazo kwa ujumla wake zinapatikana.
ReplyDeleteKaribu sana kwa madokezo ya ziada.
-----------------------------------
R.E.Njau
Mdau wa shughuli za forodha
Dar es salaam,Tanzania.
raynjau@gmail.com
--------------------------------
Jamani ee, nami naomba niangalizie kwa jamaa. Nami pia naomba ushauri juu ya gari aina ya Toyota Platz (Yaris). Msaada please.
ReplyDeleteHuyu jamaa ameuliza ushauri wa ubora wa hii gari. Sasa inashangaza watu wengine baadala ya kumpa majibu sahihi wanaanza kuanza kumuuzia gari zao na wengine kutaka kumsaidia kuaagiza.
ReplyDeleteHii haimsaidii
Spea za magari haswa za ndani si tatizo sana. Magari huwa hayaaribiki sana. Na spea za magari huwa sinaingiliana katika aina mbalimbali za magari.
ReplyDeleteIla za nje(body) kama taa, handle za milango hizo huwa zinakuwa shida kupata especially kama magari machache ya aina hiyo hapo ulipo.
Kama unataka tu gari nunua aina ya gari ambao inajulikana na kutumika sana Tanzania. Usifanye majaribio na fedha zako.
Ila kama una fedha za kutosha unaweza kutest tu hii aina ya gari. Lakini inaonekana fedha za kutosha huna.
Be in the safe side.
Hiyo gari ni nzuri kabisa haina wasi wasi nina ndugu yangu anayo na iko poa tu. Kuhusu spare zipo kwani hiyo gari ni jamii ya TOYOTA ambazo zimetapakaa sana hapa kwentu tanzania kuliko gari nyingine yeyote. Na tena engine yake inaingiliana na gari nyingi kama RAV4,Ipsum,Spacio,starlet nk hivyo spare za gari nyingi za TOYOTA zinaweza kuingiliana. Hebu Jaribu pia kuuliza kwa mafundi gari kuhusu ishu ya spare upate ushuhuda.
ReplyDeletemdau usiwe na wasi mimi nimenunua gaia miaka miwili sasa sijapata shida yoyote kubwa, injini yake kama mdau mwingine alivyosema ni 3s yaani ni sawa na injini ya rav4 yangu ni cc 1885 nilinunua hapa hapa bongo kwenye yard.
ReplyDeletekuhusu spea usitie shaka sana as long as ni toyota na unaitumia bongo there are plenty of toyota spairs here, siri moja ujue gaia imetengenezwa kwa kumerge spea tofauti kutoka magari mengine ya toyota, mimi niliwahi kubadilisha tie rod end, rack hand wakati tunatafuta dukani fundi aligundua kumbe inaingiliana na carina,
yaani hizi spea za ndani usipate shida labda kama ni zile taa, lakini mimi siku za mwanzo nilivunja endiketa ya kulia ofkoz nilitumia muda kupata kwa sababu sikujua wapi pa kutafuta lakini eventually nilikuja nunua duka moja linaitwa shamas liko shauri moyo karibu na ofisi za raha leo wale jamaa waliniambia kuwa huwa wanaenda huko mara kwa mara japan kualeta vipuri dizaini hizo, mpaka sasa miaka miwili sijawahi kufanya any major mainteance kwenye injini zaidi ya service na vitu vidogo vidogo vinavyo wear out so ndugu yangu thats my experince thats a good car for family si unajua familia zetu za kibingo mi inanisevu kishenzi
Acha na mambo ya kununua gari maana ataongeza tu foleni ya magari barabarani.
ReplyDeleteACHANA NA MAMBO YA TOYOTA ZINARUDISHWA KIWANDANI NUNUA VW AU AINA NYENGINE. TOYOTA NYANYA
ReplyDeleteumenichekesha eti asinunue gari ataongeza foleni
ReplyDeleteKwa nini usinunue BOTI hujui dar es salaam wakati wa mvua ni mafuriko tuuuuuu!
ReplyDeleteZulu safi hiyo lakini mie naziona kama chache vile hapa town.Hafu iko chini kiaina kwenye matuta uwage mpole.We ongeza utafiti na hafu fikiria na long safaris hasa uendapo kijijini kufagia mananihii. But all in all choice is better comes from within. au we sio zulu...
ReplyDeleteYaris imetulia dogo ichukue tu usiogope kila kitu mswano...
ReplyDeleteyaris ipo bomba.....hata hii GAIA nayo ipo fresh...
ReplyDeletelakini ANGALIA ENGINE ISIJE IKAWA D4....hizo zinazingua kinoma kaka....
watu wengine bwana! eti huyu jamaa anaomba ushauri wa kununua gari kwenye libeneke. hivi akali umepwa ya nini? mambo mengine mna jitakia wenyewe, wewe umpewa akili uitumie sasa unaanza kuleta kuleta. mdau toka bujumbura
ReplyDelete