assalam alaykum jamia,
nimepata shauku kubwa ya kusoma riwaya za kiswahili hasa zenye kutaa'lak na mazingira ya kale, na hasa za mafanani wa Kizanzibari ili kuweza kuudurusu utamaduni wa Mzanzibari. tafadhali unaweza kunisaidia wapi naweza kupata/kununua vitabu hivi, au vyovyote kati ya hivi:

Said Ahmed Mohamed
Babu Alipofufuka
Amezidi
Tata za Asumini
Kitumbua Kimengia Mchanga
Pungwa
Kiza katika Nuru
Kina cha Maisha (nadhani ni mashairi)
Utengano
Si Shetani si Wazimu
Asali Chungu
Dunia Mti Mkavu
Dunia Yao

Muhamed Said Abdulla (Bwana Msa)
Mzimu wa Watu wa Kale
Kisima cha Giningi
Duniani Kuna Watu
Siri ya Sifuri
Mke mmoja Waume watatu
Mwana wa Yungi Hulewa
Kosa la Bwana MSA

Shafi Adam Shafi
Kasri ya Mwinyi Fuad
Kuli
Haini
Vuta N'kuvute

Muhamed Said Muhamed
Kiu
Nyota ya Rehema

natanguliza shukrani zangu kwa msaada wako.
--------------
Hamad Hamad
Copenhagen

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Sheikh unataka kufungua darasa la kiswahili huko?
    Saleh Washington DC

    ReplyDelete
  2. Vichache kati ya hivyo ulivyovioroshesha utavipata University of Dar es Salaam Bookshop, kwa hiyo kama vipi tafuta mtu akununulie kisha akutumie.

    ReplyDelete
  3. dah mdau umenigusa???umenipa changamoto nitafute pia

    naanza pasaka hii!!
    uwiii lugha yetu adhimu sana

    ReplyDelete
  4. Wadau, nami naingia kwenye msururu,
    mwenye angalau kuwa na copy zifuatazo: ani sms on 0784236990
    Muhamed Said Abdulla (Bwana Msa)
    Mzimu wa Watu wa Kale
    Kisima cha Giningi
    Duniani Kuna Watu
    Siri ya Sifuri
    Kosa la Bwana MSA

    Muhamed Said Muhamed
    Nyota ya Rehema
    Na moja "Chaguo la Maua"

    ReplyDelete
  5. Hongera sana mdau wa lugha ya Kiswahili kwa tamaa yako njema kudumisha utamaduni wa mswahili.

    ReplyDelete
  6. Mussa MussaMarch 27, 2010

    na mimi pa nataka kuungana nawe ukifanikiwa au nikifanikiwa tushtuwane; email address yangu mussamussa@hotmail.com

    ReplyDelete
  7. Wadau kama mnataka vitabu tafadhari tuadikie hapa sisi ni shirika lisilo la kiserikali tunashughulika na mambo ya usomaji kama unataka vitabu visafirishwe mpaka huko kwako baadhi tunavyo hapa
    unaweza tutembelea website yetu hapa
    www.soma.or.tz/ +255754093768
    hapa kuna kila kitu na contact address kama unahitaji kuwasiliana na sisi
    Natanguliza shukrani
    Joachim Homvye

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...