Bi. Ever Klaue-Machangu

Msimamizi mkongwe wa matangazo ya idhaa ya kiswahili ya DW mjini Bonn Bi Ever Klaue-Machangu, leo amestaafu rasmi kazi, baada ya kuitumikia DW kwa muda wa miaka 28.

Bi Ever ambaye hapo kabla aliwahi kuwa pia mtangazaji wa idhaa ya kiswahili ya DW wakati huo ikiitwa sauti ya Ujerumani mjini Cologne, ni mwenyeji wa mkoa wa Kilimanjaro.

Akizungumza na Globu ya Jamii kwa simu moja kwa moja kutokea Bonn, Bibi Ever Klaue-Machangu, amesema anajisikia fahari kubwa kuweza kuchangia kupanua lugha ya kiswahili, kwa kufanyakazi idhaa ya kiswahili ya DW kwa miaka yote hiyo.

Sherehe kabambe ya kumuaga imeandaliwa kesho Ijumaa, kwa mapochopocho na muziki ambapo madj watakuwa watangazaji wakongwe katika idhaa ya kiswahili, kama vile Ramadhani Ali´Manju wa spoti, Oummielkher, Othman Miradji´Alhadji´, Abdul Mtullya´Konko´ na Mohamed Abdul-Rahman´Eddy´

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Silvano MachanguMarch 26, 2010

    God bless you Mama. Real umetumika miaka mingi DW but you have never forget home. Welcome back home we misses u alot.

    ReplyDelete
  2. Huyu ndo yule mama mwenye sauti flani hvi nzito lakini tamu wa DW?

    ReplyDelete
  3. Hongera sana. Umekuwa mfano wa kuigwa. nakutakia kila la kheri katika maisha mapya na tunategemea mchango wako kwa Taifa hili japo umestaafu. Mungu akubariki sana.

    ReplyDelete
  4. Kyachiya mndumi ya uyana wana wa mka wakoyone mphiri cho inu kipfa samu chi kitarasa pfo ma yekepusa pfo mpfo Makyitsinde.
    -----------------------------------
    Kutoka katika papachi za moyo wangu nimeamua kumpongeza mama yetu kutoka kule Mkolowony jirani kabisa na shule ya msingi Mrieny kwa lugha ya Kichagga ili ajisikie yupo nyumbani.Naomba samahani kwa wale ambao si wadau wa Kichagga cha Vunjo.Kwa kuwa katika lugha ya Kiswahili hakuna fungu la maneno wa sentensi ya kuonyesha hisia za shukrani kutoka katika papachi za moyo zaidi ya kusema asante,nami nasema asante na hongera sana kwa mama Ever Klaue-Machangu.
    -----------------------------------
    Mdau na mtetezi wa Kiswahili
    Dar es salaam,Tanzania.
    ---------------------------------
    Email:mcraynjau@gmail.com
    -----------------------------------

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...