Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda akiwa na Makamu wa Rais na Kaimu Rais wa Nigeria, Dk. Goodluck Jonathan (katikati) na kushoto ni Rais wa Sierra Leon, Ernest BaiKoroma wakisikiliza wimbo wa taifa wa Nigeria kabla ya kuanza kwa mkutano wa viongozi wakuu wa Afrika kuhusu Maendeleo ya Biashara na Usindikaji wa Mazao yaKilimo uliofanyika kwenye ukumb i wa hoteli ya Transcorp Hilton jijini Abuja
Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda akiteta na Rais wa IFAD, Dr. Kanayo Nwanze katika mkutano wa Viongozi wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Maendeleo ya Biashara na Usindikaji wa Mazao a Kilimo uliofanyika kwenye ukumbi wa hoteli ya Transcorp Hilton jijini Abuja
Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda, Waziri wa Viwanda Biashara na Masoko, Mary Nagu (kushoto) na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Seif Ali Iddi (kulia) wakitoka kwenye ukumbi wa mikutano wa hoteli ya Transcorp Hilton katika jiji la Abuja baa ya kufungwa kwa mkutano wa viongozi wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Maendeleo ya Biashara na usndikaji wa mazao ya kilimo Machi 10, 2010. Mheshimiwa Pinda alimwakilisha Rais Jakaya Kikwete katika mkutano huo.





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Ndiyo mkuu wa Wilaya !
    wakati hali ya uchumi dunia inajaribu kutoka kwenye mshikitiko ulio anza mwaka mmoja na nusu idadi ya wenye nazo inazidi kuongezeka ! ama kweli maneno ya biblia yanakamilika """aliye nacho ataongezewa zaidi bali yule asiye nacho atanyanganywa hata kile kidogo"""""" NAOMBA WAWEKEE LINK WADAU WAANGALIA MAMBO YANAVYOKWENDA(http://www.forbes.com/lists/2010/10/billionaires-2010_The-Worlds-Billionaires_Rank.html )
    Mdau wa Kanyigo!

    ReplyDelete
  2. Top Billionaire Cities.

    1.New York, N.Y.
    Number of billionaires: 60
    Wealthiest resident: Michael Bloomberg ($18 billion)
    Other notable billionaires: Ralph Lauren, Carl Icahn, Rupert Murdoch, Donald Trump, Mortimer Zuckerman)

    2.Moscow, Russia
    Number of billionaires: 50
    Wealthiest resident: Vladimir Lisin ($15.8 billion)
    Other notable billionaires: Roman Abramovich, Alisher Usmanov, Oleg Deripaska )
    No body could believe in the early of 80"s that Russia will be 2nd leading billionaires country in the world and this is not miracles but really fact may be is wind of change blow from east to west.....
    Mdau wa Kanyigo!

    ReplyDelete
  3. Mimi ni mdau wa utamaduni (kielelezo cha bongo zinavyofanya kazi) wa afrika na utandawazi pia. Mavazi ni sehemu muhimu sana ya utamaduni. Nikiri kuwa hakuna kitu kinaconipa raha kila nikiona viongozi waandamizi wa Nigeria wanavyovalia suti ya kinigeria wawapo katika hafla za matawi ya juu kama Dr Goodluck Jonathan anavyoonekana hapo. Hii ni sehemu ndogo, lakini inaweza kukueleza kwa nini Nigeria ni mojawapo ya mataifa yaliyoendelea sana Afrika kusini mwa jangwa la Sahara. Tanzania tayari tunayo suti ya Tanzania lakini katika hafla kama hii JK angetinga kama waziri wake mkuu anavyoonekana hapo juu - suti ya ulaya. Kisa? Eti nasi tuonakane 'tumeendelea!!!" au "tusije tukachekwa!!" Hicho nacho ni kielelezo wazi kwa nini tupo mahali tulipo: "tunakwenda na wakati!!!!"

    ReplyDelete
  4. Mdau thu Mar 11,05:00PM

    suti ya kitanzania na suti ya kinigeria zinafananaje? Nimejitahidi kumwangalia Pinda na dr ila nimeshindwa kuzitofautisha ipi ni ipi??!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...