Tingatinga likishindilia sehemu za uwanja wa Sheikh Amri Abeid leo


Picha na habari:Woinde Shizza,Arusha

Wakati ligi daraja la kwanza inatarajia kuanza kutimua vumbi jumamosi hii Marchi 13 katika uwanja wa kumbukumbu ya Sherk Amri Abeid jijini hapa. Uwanja huo kwa sasa umefungwa kwa muda kwa ajili ya marekebisho.

Ripota huyu alifika katika uwanja huo leo na kujionea umefungwa huku mafundi wakiendelea na ukarabati mdogo mdogo ukiwemo wa kupaka rangi kwenye magoli pamoja na kufyeka majani ambayo yalikuwa yameota.

Mbali na hayo pia moramu ilikuwa ikimwaga na kushindiliwa uwanjani hapo ikiwa ni shamra shamra za kuweka uwanja katika hali nzuri ya kuweza kuchezewa ligi daraja la kwanza.

Mmeneja wa uwanja huu Bw. Abeid Mashaka Gwabi alisema kuwa kiwanja hiki kimekuwa kikitumika kwa muda mrefu bila mapumziko hivyo wameamua kukipumzisha kwa muda kwa ajili ya ligi.

“unajua uwanja huu umechezewa mfululizo ikiwemo ligi ya wilaya ,kombe la mazingira na michezo mingine mingi hivyo kwa muda wa wiki hii moja itatosha kabisa kupumzika kidogo”alisema Gwabi.

Alisema kuwa wanauhakika kabisa kwa ukarabati ambao wameufanya kwa muda wa wiki hii moja unatosha kabisa kuurekebisha na ligi kuchezwa bila tatizo lolote.

Hadi sasa baadhi ya timu ambazo zitashiriki ligi daraja la kwanza zimesha wasili mjini hapa ikiwemo timu ya JKT Ruvu pamoja na Polisi ya Dodoma ambayo imetia kambi mkoani Kilimanjaro.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. KWA MASIKITIKO MAKUBWA NAANDIKA NIKIWALAUMU SANA WADAU NA WADHAMINI WA SOKA LA BONGO KUISAHAU LIGI DARAJA LA KWANZA NA KUIKUMBATIA LIGI KUU NA TAIFA STARS.LIGI DARAJA YA KWANZA NDIYO KISIMA CHA WACHEZAJI WATAKAOINGIA LIGI KUU NA TAIFA STARS LAKINI UWEKEZAJI NA PROMOSHENI HAPA NI ZIRO KABISA.SASA WADAU NA WADHAMINI WA SOKA LA BONGO BADILIKENI KABISA NA MTOE MCHANGO WENU WA HALI MALI KWENYE LIGI HII.VITUO VYA REDIO NA TELEVISHENI NENDENI ARUSHA NA MTULETEE MATANGAZO YA LIGI HIYO KWA MANUFAA YA TAIFA. TAFADHALI,TAFADHALI,TAFADHALI SANA TFF AMKENI NA MTOE MSUKUMO UFAAO KWENYE LIGI DARAJA LA KWANZA ILI TUWEZE KUJENGA TUIBUE VIPAJI VYA KUTOSHA KWA AJILI YA LIGI KUU NA TAIFA STARS.

    ReplyDelete
  2. Mdau unayewalaumu wadhamini kwa kuisahau ligi daraja la kwanza umesahau kwamba wadhamini wanafanya biashara? Wazo lako la kuhamasisha vyombo vyetu vya habari kutuonyesha kinachoendelea kwenye ligi hiyo ndilo litakalopeleka wadhamini kwenye hayo mashindano. Kama kuna uwezekano wa wengi kuyaona wadhamini watapigana vikumbo kutafuta kuonekana. Ndivyo biashara iendavyo.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...