www.watanzania-roma.blogspot.com
Monsignor Rugambwa muda mfupi kabla ya kusimikwa
Monsignor Novatus Rugambwa akisimikwa
kuwa Askofu Mkuu wa Angola na Sao Tome na Principe
Jana Jioni alhamis 18 March, kwenye kanisa Kuu la Mtakatifu Petro(Saint Peters)Mwadhama Kardinali Tarcisio Bertone ambaye ni Katibu wa Vatican, kwa niaba ya Baba Mtakatifu ametoa madaraja ya Uaskofu mkuu kwa watumishi watatu wa Kanisa Takatifu katoriki.
Kwanza kabisa kwa Mtanzania Monsignor Novatus Rugambwa ambaye ni Askofu Mteule wa Tagaria ambaye pia ni Nunzio Mteule (Mwakilishi wa Vatican) nchini Angola na Sao Tome' na Principe. Wapili ni Monsignor Pietro Piopo askofu Mteule wa Torcello na mteule Nunzio wa Cameroun na Guinea na Watatu ni Monsignor Eugene Martin Nugent Askofu mteule wa Domnach Sechnaill na ambaye ameteuliwa kuwa Nunzio wa Madagascar, Mauritus na Shelisheli.
Ibada hii takatifu iliudhuriwa pia na Askofu wa Bukoba Monsignor Nestorius Timanywa. Jumuiya ya Watanzania Rome inaungana na watanzania duniani kote kumpa hongera na kumtakia mafanikio mema Baba Askofu mteule na Nunzio Apostolico Novatus Rugambwa kwenye Wadhifa huu mpya.

Waihuyuka waitu "Hongera Bwana"
ReplyDeleteobserver
Hongera Rugambwa kwa kupata wadhifa huo mkubwa,
ReplyDeleteWadau naomba mnisaidie maana ya maneno haya
Monsignor,Nunzio,Nunzio apostolico,kardinali
Nakupongeza kwa wadhifa huu uliopata ni mtanzania wa kwanza kuwa na cheo hicho ,hongera Baba Rugamabwa,halafu naomba nisahihishe waandishi wa habari hii na hata wa magazeti,ni hivi Uaskofu siyo DARAJA ni kusimikwa uaskofu,DARAJA ni UPADRE PEKE YAKE,ndiyo maana unaweza kuvuliwa uaskofu lakini huwezi kunyang'anywa DARAJA la upadre,ningependa waandishi wa habari kabla ya kuandika habari ,hasa zinazohusu kanisa katoliki ni vyema mkawasiliana na watu wanaojua ukatoliki au wahusika kama mapandre au katibu wa Askofu au msemaji wa jimbo
ReplyDeleteAsanteni
Asante ndugu yangu Fracis Said ni hivi maana ya hayo maneno au hivyo vyeo wasiliana na katibu wa jimbo ulilopo au kama hauko jimboni wasiliana na padre wa parokia atakufamisha kwa uzuri sana au sehemu yoyote yenye watawa wa kanisa katoliki
ReplyDeleteAsante ndugu yangu mpendwa kwa maswali yako ya kutaka kuelimishwa
MUNGU AKUBARIKI