Ni wakati wa Ibada ya Kusimikwa kwa daraja la Uaskofu Mkuu, Monsignor Novatus Rugambwa mjini Vatican. Monsignor Rugambwa ataiwakilisha serikali ya Vatican Nchini Angola na Sao Tome na Principe. Kwa picha Zaidi tembelea libeneke la Jumuiya ya Watanzania Roma.
www.watanzania-roma.blogspot.com Monsignor Rugambwa muda mfupi kabla ya kusimikwa
Monsignor Novatus Rugambwa akisimikwa
kuwa Askofu Mkuu wa Angola na Sao Tome na Principe

Jana Jioni alhamis 18 March, kwenye kanisa Kuu la Mtakatifu Petro(Saint Peters)Mwadhama Kardinali Tarcisio Bertone ambaye ni Katibu wa Vatican, kwa niaba ya Baba Mtakatifu ametoa madaraja ya Uaskofu mkuu kwa watumishi watatu wa Kanisa Takatifu katoriki.

Kwanza kabisa kwa Mtanzania Monsignor Novatus Rugambwa ambaye ni Askofu Mteule wa Tagaria ambaye pia ni Nunzio Mteule (Mwakilishi wa Vatican) nchini Angola na Sao Tome' na Principe. Wapili ni Monsignor Pietro Piopo askofu Mteule wa Torcello na mteule Nunzio wa Cameroun na Guinea na Watatu ni Monsignor Eugene Martin Nugent Askofu mteule wa Domnach Sechnaill na ambaye ameteuliwa kuwa Nunzio wa Madagascar, Mauritus na Shelisheli.

Ibada hii takatifu iliudhuriwa pia na Askofu wa Bukoba Monsignor Nestorius Timanywa. Jumuiya ya Watanzania Rome inaungana na watanzania duniani kote kumpa hongera na kumtakia mafanikio mema Baba Askofu mteule na Nunzio Apostolico Novatus Rugambwa kwenye Wadhifa huu mpya.





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Waihuyuka waitu "Hongera Bwana"
    observer

    ReplyDelete
  2. Hongera Rugambwa kwa kupata wadhifa huo mkubwa,

    Wadau naomba mnisaidie maana ya maneno haya
    Monsignor,Nunzio,Nunzio apostolico,kardinali

    ReplyDelete
  3. Nakupongeza kwa wadhifa huu uliopata ni mtanzania wa kwanza kuwa na cheo hicho ,hongera Baba Rugamabwa,halafu naomba nisahihishe waandishi wa habari hii na hata wa magazeti,ni hivi Uaskofu siyo DARAJA ni kusimikwa uaskofu,DARAJA ni UPADRE PEKE YAKE,ndiyo maana unaweza kuvuliwa uaskofu lakini huwezi kunyang'anywa DARAJA la upadre,ningependa waandishi wa habari kabla ya kuandika habari ,hasa zinazohusu kanisa katoliki ni vyema mkawasiliana na watu wanaojua ukatoliki au wahusika kama mapandre au katibu wa Askofu au msemaji wa jimbo
    Asanteni

    ReplyDelete
  4. Asante ndugu yangu Fracis Said ni hivi maana ya hayo maneno au hivyo vyeo wasiliana na katibu wa jimbo ulilopo au kama hauko jimboni wasiliana na padre wa parokia atakufamisha kwa uzuri sana au sehemu yoyote yenye watawa wa kanisa katoliki
    Asante ndugu yangu mpendwa kwa maswali yako ya kutaka kuelimishwa
    MUNGU AKUBARIKI

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...