
NA MWANDISHI MAALUM
NEW YORK-Wajumbe wa Kikao cha Kazi cha Baraza Kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa,wameishauri Tanzania kupitia upya makadirio ya ujenzi wa mahali pa kuhifadhia nyaraka , kumbukumbu na masalia ya shughuli zote za Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari (ICTR).
NEW YORK-Wajumbe wa Kikao cha Kazi cha Baraza Kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa,wameishauri Tanzania kupitia upya makadirio ya ujenzi wa mahali pa kuhifadhia nyaraka , kumbukumbu na masalia ya shughuli zote za Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari (ICTR).
Wajumbe hao wametoa ushauri huo, mara baada ya Tanzania kupitia Mwakilishi wake katika Umoja wa Mataifa, Balozi Augustine Mahiga, kutetea kwa nguvu zote haki ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya kuhifadhi nyaraka hizo na yote yatokanayo na Makahama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari.
Katika ushauri wao, ambao umetolewa kwa nia njema, baadhi ya wajumbe hao wameeleza kushtushwa kwao na gharama kubwa zilizowasilishwa na Tanzania. Gharama ambazo inasemekana ni mara nne zaidi ya zile zilizowasilishwa na nchi jirani.
“Mhe. Balozi tumeyapokea maelezo yako, na tunashukuru sana kwa namna ulivyojenga hoja na kujieleza, kwa kweli tumeridhika, lakini hili la gharama ambalo tumelisoma katika taarifa nyingine, linatuacha na maswali. Ni matumaini yetu kwamba serikali yako itakuwa inalifanyia kazi hili, na tunashauri kwa kweli mfanye hivyo na kutuletea taarifa zaidi.
Akitoa utetezi wake mbale Kikao hicho. Balozi amesema Tanzania inayo nia, utayari na sifa zote za kulitekeleza jukumu hilo.
Balozi Mahiga ambaye alialikwa mbele ya Kikao hicho, kilichofanyika siku ya jumanne, ambapo alitakiwa kuwaeleza wajumbe ni kwa nini anadhani Tanzania ina sifa na inakidhi hadhi ya kuwa mhifadhi wa nyaraka na kumbukumbu na shughuli zote za ICTR baada ya mahakama hiyo kumaliza muda wake.
Katika utetezi wake uliodumu kwa dakita kumi na tano. Ambao ulianza kwa kuelezea historia nzima iliyozaa kuanzishwa kwa Mahakama hiyo. Balozi Mahiga amesema, tangu kuanzishwa kwa Mahakama hiyo, Tanzania imefanya kazi na kutoa ushirikiano mkubwa kuanzia Baraza Kuu la Usalama, Umoja wa Mataifa hadi katika Mahakama yenyewe , watendaji na shughuli zima za utafutaji wa haki.
“ Kwa miaka 16 mfulululizo, serikali ya Tanzania kuanzia mwanzo wa maandalizi ya makahama hiyo, mpaka ilipoanza kazi na hadi sasa, imejitolea kwa hali na mali, kwa kuweka mazingira mazuri ambayo siyo tu yameiwezesha mahakama hiyo kutekeleza jukumu lake la kutoa haki. Lakini pia imefanya kazi zake katika mazingira ya utulivu, usalama na amani ” akasema Mahiga.
Na Kuongeza “ siyo tu kwamba Tanzania ilikidhi vigezo vyote vya kimataifa vya kuanzishwa na hatimaye kuendeshwa kwa Mahakama hiyo, lakini pia ilitimiza wajibu wake wa kimataifa kupitia makubaliano iliyoingia na Umoja wa Mataifa, Baraza Kuu la Usalama pamoja na Mahakama yenyewe.
Anasema Mahiga.
Anasema Mahiga.
Kubaki kwa nyaraka , kumbukumbu na mchakato mzima wa ICTR katika ardhi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania licha ya faida zake nyingine nyingi kama vile utafiti, kutumika kama hadidu za rejea, na kivutio cha kihistoria.
Kubaki kwake ni heshima kubwa kwa Tanzania, itakuwa ni kuheshimu na kutambua mchango mkubwa wa Tanzania ambayo imeutoa kwa ICTR, UN, Baraza Kuu la Usalama na katika mchakato mzima wa utafutaji wa haki .
Kubaki kwake ni heshima kubwa kwa Tanzania, itakuwa ni kuheshimu na kutambua mchango mkubwa wa Tanzania ambayo imeutoa kwa ICTR, UN, Baraza Kuu la Usalama na katika mchakato mzima wa utafutaji wa haki .
“ Yote yatokanayo na mahakama hii yanatakiwa kubaki katika Ardhi ya Tanzania, ardhi ya Afrika na kumilikiwa na kutunzwa na waafrika wenyewe. Na hii itakuwa ni heshma kubwa sana kwa si kwa Tanzania bali kwa Afrika na waafrika” akasisitiza Balozi.
Akiwasilisha hoja zaidi, Balozi Mahiga anaeleza wazi kwamba, nyaraka zote za Mahakama hiyo zinataarifa muhimu sana na nyeti zinazohusiana na mashahidi. Mashahidi ambao Tanzania ilitoa mchango mkubwa sana katika kupatikana kwao.
Na kwa sababu hiyo, anasema , ikiwa nyaraka hizo hazitadhibitiwa na kutunzwa ipasavyo zinaweza kuhatarisha maisha ya mashahidi na familia zao.
Akaeleza pia kwamba kipindi chote cha uhai wa Mahakama hiyo, ICTR imeweza kuzihifadhi nyaraka hizo na taarifa muhimu katika aridhi ya Tanzania kwa usiri mkubwa na usalama wa hali ya juu. Si usalama wa nyaraka peke yake bali pia usalama wa watendaji wa mahakama, washtakiwa , wahanga na mashahidi.
Akafafanua zaidi kwa kusema, katika miaka yote hiyo, Serikali ya Tanzania, imetoa ulinzi wa kutosha kwa matabaka mbalimbali ya mashahidi, imewezesha kufika kwao katika mahakama hiyo na kuhakikisha kwamba wanaendelea kulindwa hata baada ya kutoa ushahidi wao wakiwa ndani ya ardhi ya Tanzania.
Hayo yote na mengine mengi ambayo Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeyafanya na inaendelea kuyafanya. ni dhahiri kwamba Tanzania inatabirika na inaaminika kupewa jukumu hilo.
Akasema kuendelea kubaki nchini Tanzania kwa nyaraka na mabaki yote yanayohusiana na Makama hiyo. Utakuwa ukumbusho tosha kwa wale wote watakaotaka kujihusisha na mauaji ya halaiki, vitendo vya kikatili dhidi ya binadamu na makosa ya kivita.
“Kwa Tanzania kuwa muhifadhi wa kumbumbuku za ICTR pia itakuwa ni kielelezo cha kwamba , kukamilika kwa shughuli za Mahakama hiyo hakumaanishi kuwa sasa Umoja wa Mataifa, Baraza Kuu la Usalama na Jumuia ya Kimataifa haitawashughulika tena wahalifu”.
Nchi ambazo hadi sasa zimebaki katika kinyanganyiro cha kuwania haki ya uhifadhi wa kumbukumbu za Mahakama hiyo baada ya nyingine kujitoa ni Tanzania na Kenya.
hii ndiyo taaabu ya watanzania, 10% zinatupeleka pabaya.
ReplyDeletesafi sana mh.Dr.Mahiga hata mimi nimefurahishwa sana na utetezi wako, ila rekebisha swala la ghalama ili yote tuliyofanya yakaonekana kuwa sifuri.
ReplyDeleteMdau toka KAZAKHASTAN-ASIA
Kenya natumai wamebid kupitia mapungufuu yetu kama ya bei na kujipangaa..
ReplyDeleteTunastahili heshima ya kuwa mhifadhi wa nyaraka hizoo.
Ningeomba waliotoa taarifa za mapendekezo hayo wathibitishe takwimu zao za kifisadi hizo na wawajibike,walidhani yataishia kwa mbumbumbu zao waliowazoea!!! Mambo ya aibu haya, Hovyo ovyo kila siku...!!! Amkeni mkemee uozo huu too much bwana tumechoka!!
ReplyDeleteHakuna Cha Kustahili...
ReplyDeleteWahusika warekebishe gharama kama walivyoshauriwa, kwa wale wanaojua Projects Accounting hilo sio jambo geni wala gumu kulifanya. Tanzania imekuwa ikihifadhi nyaraka hizi kwa miaka yote 16, hivyo majengo, makabati, ulinzi n.k tayari vipo in place....sasa inakuwaje gharama walizotoa zinazidi majirani zetu.
Either hao majirani ni wasanii au Tanzania inaleta usanii. Kwa mujibu wa UN ianonyesha Tanzania ndio haiaminiwi...i wonder why..!!!
NI KWELI TANZANIA INASTAHILI;LAKINI JE INASTAHILI?JIBU LA SWALI HILO LIPO MIKONONI MWA WANAZUONI WETU WA BAJETI NA MICHANGANUO WATUONYESHE USTAHILI WETU.HISTORIA HAITAKUBALI HIFADHI IWE NJE TANZANIA;HUU NI URITHI WETU.
ReplyDelete