Meneja mkuu wa Global Publishers Abdallah Mrisho akimzawadia mpiga drums mahiri wa Twanga Pepeta, Martin Kibosho, zawadi ya kuwa mfanyakazi bora wa mwezi wa bendi hiyo kwa upande wa wapiga ala kwenye mnuso maalumu ulioenda sambamba na onesho la kila jumatano la bendi hiyo katika ukumbi wa Club Billicanas jijini Dar usiku huu. Shoto ni Mkurugenzi wa African Stars Entertainment Da'Asha Baraka na kulia ni RichardBig Brother II aliyekuwa MC Ankal akimzawadia Salehe Kupaza zawadi ya mfanyakazi bora wa mwezi wa Twanga Pepeta kwa upande wa waimbaji huku Da'Asha Baraka akishuhudia usiku huu katika Club Billicanas jijini Dar

Steve Kanumba The Great akimkabidhi zawadi ya mfanyakazi bora wa mwezi wa Twanga Pepeta upande wa wanenguaji, Amina Sharapova, huku Da'Asha Baraka na MC Richard Big Brother wakishuhudia usiku huu
Ankal akishangilia wakati Da'Asha Baraka akitaja sababu zilizomfanya Saleh Kupaza achaguliwe kuwa mfanyakazi bora wa Twanga Pepeta upande wa waimbaji. Kupaza keshatunga nyimbo kibao na mwezi huu kaangusha tungo nnyingine
Mkurugenzi wa African Stars Entertainment (ASET) Da'Asha Baraka akitoa hotuba
Club Billicanas ilifurika kama kawaida yake
Da'Asha Baraka akiwa na Steven Kanumba the great (shoto) na Ray The Greatest
Richard Big Brother pamoja na kuwa MC pia
kampuni yake ndiyo iliyopata tenda ya kurekodi tukio hilo
kabla na baada ya zawadi Twanga walipepeta kisigino hadi lyamba
Kalala jr na Aisha Madinda wakiongoza safu katika kutoa burudani murua










Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. OOHH men.. Get some real shirts, your armpits must be burning with those reflectors.

    ReplyDelete
  2. ni nchi gani hapa duniani ambayo ni miongoni mwa mataifa maskini sana 15 ambayo wananchi wake wanapenda starehe sana kuliko kazi na wanapenda kutumia msemo wa twende tukapoteze muda kijiweni au sehemusehemu,na wanapenda ngono sana na matokeo yake inashambuliwa na maambukizi ya HIV kwa kasi sana kwa njia ya ngono! na wakiwa na wananchi wa mataifa mengine wanajisikia wanyonge na wadhaifu kwakuwa wengi wao hawajui kuongea kiingereza kwa ufasaha,na sio hilo tu bali nimazoea ya kuzimikia mataifa mengine,na mabinti wa nchi hiyo akikutana na mtu wa taifa jingine tu basi anaoza hadi mwisho hata bila kujua nini kinachoweza mpata mbeleni na anategemea kuwa umaskiniwake ndiyo utapata ufumbuzi hapo. jibu sahihi nitatoa zawadi.

    ReplyDelete
  3. Huyo Aisha mbegu madinda amejaaliwa upaja. Hapa udenda unanitoka utafikiri nimeona ukwaju!

    ReplyDelete
  4. Jamani kuuliza si ujinga, pamoja na kuishi Dar kwa miaka 3 sikuwahi kwenda Billcanas naomba mnielekeze mahali ilipo make natarajia kutia timu Dar mwezi april.

    ReplyDelete
  5. Ooh! Yes I like this....Kanumba THE GREAT na Ray THE GREATEST. You made my day ankal.

    ReplyDelete
  6. Nyakatakule Unyilisya EchaloMarch 11, 2010

    ASET HONGERENI SANA KWA KUFIKIRIA NA KUWAMOTISHA WATUMISHI WENU NA PIA KWA KUWAHUSISHA WASANII WENGINE WA BONGO KATIKA KUWATUNUKU.

    Hata hivyo niwape ushauri wa bure kama ifuatavyo:-

    1. Uzoefu unanituma kusema kuwa hamtaweza kutoa zawadi za UHAKIKA kila mwezi, kila mwaka, kila karne. Kama mnafikiri mnaweza haya endeleeni nionekane kuwa muongo na mwenye wivu!

    2. Zawadi za namna hii (kind of Hygiene Factors) zinaweza zikaongeza tija au zikadidimiza tija kwa kasi ya ajabu.
    Hivyo hakikisheni kuwa vigezo vya utoaji hizo zawadi vinafahamika kwa watumishi wote kwa maandishi na mfumo wa kupima utendaji uwe huru, wa haki na unaojulikana kwa wote. Yaani ni akina nani wanatoa alama na hatimaye kuamua kuwa mchapakazi bora ni nani na utaratibu wa zawadi ni ujulikane. Na je tunu zinakuwa zinafafana au ni Da Asha atakavyoona inafaa.

    Sijui kama pia mtathaminisha zaidi ufanisi(Efficiency) au matokeo (output/outcome) anayosababisha mtumishi.
    Mfano Dancer anaweza kuwa anacheza kwa kutumia nguvu nyingiiii na kujirusha sana chini lakini bado hafurahishi kabisa hadhira.

    Au mimi nikatunga nyimbo 10 za kawaidaaa wakati mwenzangu anaibuka na moja tu ambayo mashahiri yake yanawanyanyua watu kwenye viti! Hapo sasa ni vipi?

    3. Hili mnaweza kuona kuwa halina maana lakini niliseme.
    Hapo Bilz wateja wanalipa kiingilio kuja kupata burudani ya muziki. Kitendo cha kuchukuwa muda wao ili ugawe zawadi na kutoa maelezo na kustage mastaa wa Bongo kinahitaji ridhaa yao. Je itapatikanaje hiyo ridhaa ya wote.

    Hivyo nashauri kuwa:

    1. Zawadi zitolewe kila baada ya miezi 3 (Quarterly). Hii itatoa nafasi ya kutosha kwa Kamati au Mfumo unaohusika kuangalia nidhamu, bidii, ubunifu na ufanisi wa watumishi kabla ya kutoa zawadi.

    2. Tukio la kuwazawadia watumishi wenu liwe kando kabisa na mnapokuwa katika shughuli. Yaani iwe ni hafla / kutaniko la kuwatunuku watumishi bora wa Twanga Pepeta wakiwa mapumzikoni. Iwe ni siku yeyote ya wiki kama mtakavyoona inafaa. Kwa kifupi wanatakiwa wawe mapumzikoni na ikiwezekana wakitumbuizwa na wengine.

    Licha ya kukwepa lawama za wateja wasiofurahia 'kuchukuliwa muda wao' kuna sababu nyingine za Saikolojia ya kazi ambazo sitakuwa na muda wa kufafanua hapa isipokuwa kama mtapenda mnaweza kuwasiliana nami nikawashauri.

    Pamoja na ushauri wote narudia kuwapongezeni kwa nguvu zote. Na kila mara nikiwa hapo Dar mimi huwa ni wenu damu maana;
    "Twanga Pepeta niliipenda mwenyeweee, hata popote nikwënda nayooo!!

    ReplyDelete
  7. da hayo mashati ya kina kanumba na ray sooo inabidi watembee na fire extng moto unaweza ukawaka ghafla

    ReplyDelete
  8. Mzee wa Bwawa la Maini..Tungependa kuona clip ya tukio hilo..Hususani wanatwanga wakisigina..Sisi tupo mbali..

    ReplyDelete
  9. doh! mashati ya kanumba na ray yamenikumbusha udogoni baba aliponinunulia shati la aina hiyo wakati ule tuliyaita "Suku Suku" Kanumba na Ray oyeeeeeeee!kwa kunikumbusha utotoni

    ReplyDelete
  10. Zawadi kila mwezi kwa watu wote hao ni kuengezeana uchafu nyumbani. Zawadi zitakua cheap shit tu.

    kam manataka kuwanufaisha wafanyakazi wenu at least mngempa mfanyakazi bora mmoja kila mwezi na iwe zawadi ya maana itakayomsaidia maishani kwake....



    najua ankal hawa ni sponsor wako usije ukabania heri uambiewe ukweli kuliko....

    ReplyDelete
  11. Ni mimi tena na zawadi ziwe kama kumsposor mtu masomo ya jioni chuo chochote hata short courses, computer, hata trip ya mfanyakazi na familia yake kwenda mahali kupumzika etc etc...wakijaga kuzeeka waweze hata kufanya mambo mengine ya maana au kukumbuka kuwa walikwenda sehemu ya maana....zawadi kama hizi zitawafanya wafanyakazi kuchapa kazi zaidi.

    Huku kwangu mfanyakazi bora unapata hela ya maana, disney trip, big screen Tv etc etc

    ReplyDelete
  12. ha ha haaa nafwaaa we mdau uliyesema ati mashati ya suku suku nimejikojolea laivu kwa kucheka yaani nimeangua cheko na machozi juu blogu ya jamii oyeeeeeee

    ReplyDelete
  13. Eeee! huyu Nyakutakule amerudi, alipotea sana. Naona anafaa maana huwa ana mawazo ya busara.

    Uncle nawe uanzishe zawadi kwa wadau wanaotoa michango ya maana kama hao. Hata Tshirt yako ya michuzi blogu itawafaa kama kumbukumbu

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...