



Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
OOHH men.. Get some real shirts, your armpits must be burning with those reflectors.
ReplyDeleteni nchi gani hapa duniani ambayo ni miongoni mwa mataifa maskini sana 15 ambayo wananchi wake wanapenda starehe sana kuliko kazi na wanapenda kutumia msemo wa twende tukapoteze muda kijiweni au sehemusehemu,na wanapenda ngono sana na matokeo yake inashambuliwa na maambukizi ya HIV kwa kasi sana kwa njia ya ngono! na wakiwa na wananchi wa mataifa mengine wanajisikia wanyonge na wadhaifu kwakuwa wengi wao hawajui kuongea kiingereza kwa ufasaha,na sio hilo tu bali nimazoea ya kuzimikia mataifa mengine,na mabinti wa nchi hiyo akikutana na mtu wa taifa jingine tu basi anaoza hadi mwisho hata bila kujua nini kinachoweza mpata mbeleni na anategemea kuwa umaskiniwake ndiyo utapata ufumbuzi hapo. jibu sahihi nitatoa zawadi.
ReplyDeleteHuyo Aisha mbegu madinda amejaaliwa upaja. Hapa udenda unanitoka utafikiri nimeona ukwaju!
ReplyDeleteJamani kuuliza si ujinga, pamoja na kuishi Dar kwa miaka 3 sikuwahi kwenda Billcanas naomba mnielekeze mahali ilipo make natarajia kutia timu Dar mwezi april.
ReplyDeleteOoh! Yes I like this....Kanumba THE GREAT na Ray THE GREATEST. You made my day ankal.
ReplyDeleteASET HONGERENI SANA KWA KUFIKIRIA NA KUWAMOTISHA WATUMISHI WENU NA PIA KWA KUWAHUSISHA WASANII WENGINE WA BONGO KATIKA KUWATUNUKU.
ReplyDeleteHata hivyo niwape ushauri wa bure kama ifuatavyo:-
1. Uzoefu unanituma kusema kuwa hamtaweza kutoa zawadi za UHAKIKA kila mwezi, kila mwaka, kila karne. Kama mnafikiri mnaweza haya endeleeni nionekane kuwa muongo na mwenye wivu!
2. Zawadi za namna hii (kind of Hygiene Factors) zinaweza zikaongeza tija au zikadidimiza tija kwa kasi ya ajabu.
Hivyo hakikisheni kuwa vigezo vya utoaji hizo zawadi vinafahamika kwa watumishi wote kwa maandishi na mfumo wa kupima utendaji uwe huru, wa haki na unaojulikana kwa wote. Yaani ni akina nani wanatoa alama na hatimaye kuamua kuwa mchapakazi bora ni nani na utaratibu wa zawadi ni ujulikane. Na je tunu zinakuwa zinafafana au ni Da Asha atakavyoona inafaa.
Sijui kama pia mtathaminisha zaidi ufanisi(Efficiency) au matokeo (output/outcome) anayosababisha mtumishi.
Mfano Dancer anaweza kuwa anacheza kwa kutumia nguvu nyingiiii na kujirusha sana chini lakini bado hafurahishi kabisa hadhira.
Au mimi nikatunga nyimbo 10 za kawaidaaa wakati mwenzangu anaibuka na moja tu ambayo mashahiri yake yanawanyanyua watu kwenye viti! Hapo sasa ni vipi?
3. Hili mnaweza kuona kuwa halina maana lakini niliseme.
Hapo Bilz wateja wanalipa kiingilio kuja kupata burudani ya muziki. Kitendo cha kuchukuwa muda wao ili ugawe zawadi na kutoa maelezo na kustage mastaa wa Bongo kinahitaji ridhaa yao. Je itapatikanaje hiyo ridhaa ya wote.
Hivyo nashauri kuwa:
1. Zawadi zitolewe kila baada ya miezi 3 (Quarterly). Hii itatoa nafasi ya kutosha kwa Kamati au Mfumo unaohusika kuangalia nidhamu, bidii, ubunifu na ufanisi wa watumishi kabla ya kutoa zawadi.
2. Tukio la kuwazawadia watumishi wenu liwe kando kabisa na mnapokuwa katika shughuli. Yaani iwe ni hafla / kutaniko la kuwatunuku watumishi bora wa Twanga Pepeta wakiwa mapumzikoni. Iwe ni siku yeyote ya wiki kama mtakavyoona inafaa. Kwa kifupi wanatakiwa wawe mapumzikoni na ikiwezekana wakitumbuizwa na wengine.
Licha ya kukwepa lawama za wateja wasiofurahia 'kuchukuliwa muda wao' kuna sababu nyingine za Saikolojia ya kazi ambazo sitakuwa na muda wa kufafanua hapa isipokuwa kama mtapenda mnaweza kuwasiliana nami nikawashauri.
Pamoja na ushauri wote narudia kuwapongezeni kwa nguvu zote. Na kila mara nikiwa hapo Dar mimi huwa ni wenu damu maana;
"Twanga Pepeta niliipenda mwenyeweee, hata popote nikwënda nayooo!!
da hayo mashati ya kina kanumba na ray sooo inabidi watembee na fire extng moto unaweza ukawaka ghafla
ReplyDeleteMzee wa Bwawa la Maini..Tungependa kuona clip ya tukio hilo..Hususani wanatwanga wakisigina..Sisi tupo mbali..
ReplyDeletedoh! mashati ya kanumba na ray yamenikumbusha udogoni baba aliponinunulia shati la aina hiyo wakati ule tuliyaita "Suku Suku" Kanumba na Ray oyeeeeeeee!kwa kunikumbusha utotoni
ReplyDeleteZawadi kila mwezi kwa watu wote hao ni kuengezeana uchafu nyumbani. Zawadi zitakua cheap shit tu.
ReplyDeletekam manataka kuwanufaisha wafanyakazi wenu at least mngempa mfanyakazi bora mmoja kila mwezi na iwe zawadi ya maana itakayomsaidia maishani kwake....
najua ankal hawa ni sponsor wako usije ukabania heri uambiewe ukweli kuliko....
Ni mimi tena na zawadi ziwe kama kumsposor mtu masomo ya jioni chuo chochote hata short courses, computer, hata trip ya mfanyakazi na familia yake kwenda mahali kupumzika etc etc...wakijaga kuzeeka waweze hata kufanya mambo mengine ya maana au kukumbuka kuwa walikwenda sehemu ya maana....zawadi kama hizi zitawafanya wafanyakazi kuchapa kazi zaidi.
ReplyDeleteHuku kwangu mfanyakazi bora unapata hela ya maana, disney trip, big screen Tv etc etc
ha ha haaa nafwaaa we mdau uliyesema ati mashati ya suku suku nimejikojolea laivu kwa kucheka yaani nimeangua cheko na machozi juu blogu ya jamii oyeeeeeee
ReplyDeleteEeee! huyu Nyakutakule amerudi, alipotea sana. Naona anafaa maana huwa ana mawazo ya busara.
ReplyDeleteUncle nawe uanzishe zawadi kwa wadau wanaotoa michango ya maana kama hao. Hata Tshirt yako ya michuzi blogu itawafaa kama kumbukumbu