Kutoka kulia ni Mkurugenzi wa 4Layers (T) Ltd., Nashesha Mvungi, Mlezi Mama Esther Mkwizu, Mwenyekiti wa Tanzania Private Sector Foundations, Meneja Masoko 4 Layers (T) ltd Levis Paul na Mr Jackson Sinkolongo Sales and Marketing Manager Macmillan Bookstore.
Baadhi ya wanafunzi wawakilishi wa vyuo mbali mbali waliudhuria

Wawakilishi toka sehemu mbalimbali na wanahabari
Mkuu wa itifaki na MC Masoud Ali Kipanya akifafanua jambo wakati wa uzinduzi huo
RISALA YA MKURUGENZI WA KAMPUNI YA 4LAYERS NASHE MVUNGI
Mama mleziwa NITASOMA Scholarship scheme mheshimiwa mama Esther Mkwizu, wageni waalikwa toka Wizara ya Elimu, Tanzania Commision of Universities, The Gaming Board of Tanzania, Push Mobile, Goethe Institute, Macmillan, Ndugu zangu waandishi wa habari, ndugu wanafunzi wa wakilishi wa vyuo mbalimbali wageni waalikwa mabibi na mabwana.

Kwa niaba ya uongozi wote wa kampuni ya 4layers (T) Ltd, napenda kuwashukuruni sana kwa kujumuika nasi siku hii muhimu sana kwetu sisi kama kampuni. Siku ya uzinduzi wa huduma maalum kwa jamii NITASOMA.

Kampuni ya 4Layers (T) Ltd, Tuition Management Solution inaazisha mpango maalum wakuwawezesha wanafunzi katika ngazi zote kupata nafasi ya kusoma ndani ya nchi bila kujali, jenda, rangi, kipaji, wala alama za juu za masomo, ujulikanao kwaj ina la NITASOMA Scholarships for both NON and Merit Students.

4Layers (T) Ltd ni miongoni mwa kampuni chache nchini ambayo inajihusisha na utoaji wa huduma hususani katika maswala ya Elimu.

Ndugu waandishi wa habari ,kwa wanafunzi walengwa mpango huu utaanza rasmi tarehe 15.03.2010 , huduma ambazo kampuni hii itatoa ni scholarship kwa mashule na vyuo taasisi zote za elimu ya juu kwa ujumla vilivyopo nchini, pili ni pamoja na kutoa ushauri wa kitaalam kwa wanafunzi juu ya kuchagua masomo kwa shule za sekondari pia kuelimishwa jinsi kujiunga na mashule au vyuo na vitengo mbalimbali vya elimu na ufundi, mafunzo katika kuandika barua ya kuomba kazi , muongozo kamili katika kuboresha elimu kwa ujumla huduma hii itawalenga wanafunzi kuanzia shule za sekondari, vyuo vya elimu ya juu na vyuo vikuu.

NITASOMA Annual Career day ni siku ambayo wanafunzi watakutana na wataalam maarufu nchini ana kwa ana na kujadiliana kuhusu ubora, umuhimu hata matatizo ya ufanisi katika sekta hizo mbalimbali.

Nimatarajio yetu pia katika siku za mbele ni kutoa udhamini katika shughuli mbalimbali za kielimu na vijana.

Nikiwa kama Mkurugenzi Mtendaji , napenda kufafanua kuwa kipindi cha mwaka tunatarajia kusomesha bure wanafunizi 6 kwa muda wote wa masomo na kutoa zawadi za Laptop 12, vitabu vya masomo au vifaa vya masomo kwa wanafunzi 12, simu ya mkononi 1 kwa wiki zawadi hizi ni kwa wanafunzi wale watakaoshinda kupitia bahati nasibu maalum.

Wanafunzi watakao kufaidika na mpango huu ni wale tu watakao tuma ujumbe mfupi wa simu NITASOMA SEC au NITASOMA HIGH kwa shule za sekondari au NITASOMA UNI kwa vyuo vikuu kwenda kwenye namba 15767 na ataingia katika mchakato huo kwa gharama ya shilingi ya kitanzania 500 tu.

Zawadi hizo zitatolewa kwa awamu yaani laptop moja kwa kila mwezi. Simu ya mkononi kila wiki na vitabu kila mwezi tukizingatia masharti na vigezo.

Napenda kukumbusha tena mpango huu wajamii utasaidia kuwapa nafasi wale walioshindwa kwenda kusoma ndani na nje ya nchi kupitia nafasi za serikali na kwa wanafunzi walioshindwa kuendelea kusoma kutokana na gharama za masomo. Pia mpango huu utasaidia wanafunzi walioshindwa kupata nafasi ya kusoma kutokana na ushindani wa alam au nafasi maalum na wanafunzi wengine.

Kuhusiana na utaratibu wamalipo, 4 Layers (T) Ltd Tuition Management solutions kama kampuni itafanya malipo moja kwa mojakatika shule au chuo husika haku na mwanafunzi atakayepewa ada ya masomo (Tuition fees)fedha za vitabu mkononi.

Naomba kumalizia kwa kumbusha tu mfumo huu utapunguza idadi ya wanafunzi wanao soma kupitia Bodi ya Mikopo kwani wengi wao huwa wanashindwa kulipa mkopo baada ya muda wa kusoma au hatakushindwa kukamilisha vigezo vya kupata mikopo hio.

Nimatarajio yetu kuchagua mshindi wa kwanza wa NITASOMA Scholarship kwa zawadi ya simu ya mkononi tarehe 22.03.2010 yaani jumatatu ijayo.

Asanteni kwa kunisikiliza.








Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. Thank you 4Layers but not thank you!! Hii company holding some important finacial information to the public i'm not happy for that.
    Kwasababu wanasema watasomesha 6 student bure per year ukipiga mahesabu ya harakaharaka total fees za students hao kwa Tsh haizidi 24million pia wanasema watatoa 12 laptop per ya year which means kila mwezi Laptop moja total cost za computer hizo ni kama milion 8 hivi. ukichunguza na kufanya Capital budgeting ya company hii IRR(kwa lugha ya Finance) utaona kuwa wanapata Faida kubwa kuliko wanafunzi maana kwa mahesabu ya haraka haraka utaona hizo text message watakazosendi kushindania hizo nafasi au kupata sponsorship ya company hiyo kwa njisi walivyoplan forecast yao kwakweli watapata pesa mamilion ya pesa halafu huduma watakayotoa hailingani na income received piga tu mahesabu ya minimum forecast lets say student 100,000 time 500 = 50mil na hii inarepeat for 12 month man! hawa jamaa nawasifu kwa huo mchezo mchafu wanaotaka kuucheza Jamani Wanafunzi Tz fumbueni macho!!!!! Sijui kama kwenye Press conference waliuliza pia how much Tax subsidies wanareceive from the TZ Gov????? maana mimi binafsi sitaki kufund wizi huu wa waziwazi WE derserve Answers from 4Layers CEO.Nakaribisha mjadala wa swala hili kwa wadau wote wenye machungu na nchi. Michuzi usibanie hii comments tafadhali Mdau USA

    ReplyDelete
  2. mdau usa kwahiyo ulitaka wafanyeje ili kupata hela za kulipia ada, zawadi, ofisi, wafanyakazi, nk?
    ebu wajuzi wa kiswahili, ni jenda au jinsia?

    ReplyDelete
  3. Mdau USA afadhali umeona hiyo. Na hapo ukiuliza tax huoni. Bongo yetu ukiwaambia watu wafungue macho hawaoni.

    Mimi attention imeingia nilivyoona majina mengi ya hao watu ni ya wapare. Nimejiuliza hii ni ile in-cooperate scam nini ambayo ipo huku USA ambayo imeshashtukiwa ila bongo yetu wakijashtuka wengi wametajirika...

    ReplyDelete
  4. Duh...najua ninachotaka kusema ni irrelevant lakini, ze Mr Ze Kipanya ze hair!! OMG! Ze nywele is ze hair so iz you comb or shave it all.

    Senk yu.

    ReplyDelete
  5. Mdau wa US umefanya critical analysis bomba na umethink outside the box! I wish wa TZ wengi wangekuwa na critical mind kama yako! Ukweli ni kwamba,
    1. hao wanafunzi watajisomesha wenyewe kupitia hizo gharama za sms watakazotuma na laptop watajinunulia wenyewe kwa hizo sms.
    2. Kwa hizo sms faida watagawana phone companies na hao 4 Layers,
    3. Walengwa ambao wengi wako vijijini na wanashindwa hata kujilipia Tshs.20,000/- kwa mwaka sec sch hawana uwezo wa kupata simu za kutuma sms. Watafaidi wale wale wenye visimu vya mkononi.
    4. Kama kampuni hii ina nia njema ya kusaidia watoto wa Tanzania, kwanini wasishirikiane na watendaji wa Mitaa, Vijiji na Kata kuwapata watoto wasio na uwezo lakini vichwa vinachaji wakawasomesha??
    Wiiiizi Mtupu!

    ReplyDelete
  6. mdau USA mimi nafikili huja think out of the box kama mwenyewe unavyosema... wewe umefikilia kama wanafunzi wakijitokeza wengi kama 100,000 kumbuka hiyo ni kampuni na tayari wameishatoa ahadi kwa hiyo hata wakiwa 1000 walio shiriki lazima wapatikane washindi nani sasa atalipa gharama hizo wakiwa wachache, nyinyi watu mlio nje kwanini mnakuwa wagumu wa kufikili na kufilia mambo mabaya tuuu, njoona wewe ufanye chako tukione sio kujifanya unajua kucritiseze wakati huna mchango wowote kwenye taifa

    Mdau sweden

    ReplyDelete
  7. Kweli hii ni biashara na haina nia yoyote ya kusaidia jamii. Ningetegemea kuwa walengwa wawe wanafunzi ambao bila msaada wasingesoma. Lakini ni wazi kuwa watu wanaohitaji zaidi msaada wa kulipia elimu wana nafasi ndogo sana ya kuupata. Ama waandaji hawakuufikiria vizuri mchakato wa kupata wanafunzi au ni biashara tu. Kama ni biashara sema ni biashara tujue moja. Sio mnatoa lugha za kuchanganya watu..

    ReplyDelete
  8. Wanafunzi 6 kwa mwaka wachache sana! Ingekuwa hamna kutuma sms hapo sawa.. sasa hii ni kama 'lotto' au bahati nasibu. Bisha?

    ReplyDelete
  9. Hii ni BAHATI NASIBU kwa kutaka kujifichia kwenye watoto wa shule. Serikali ndio ya kulaumiwa kwanini watoe kibali cha kuruhusu kampuni wizi kama hizi zinazotumia jina la KUSAIDIA JAMII ili waweze kujinufaisha...

    ReplyDelete
  10. Hawa jamaa ni waumini wa falsafa ya Kimakaveli "Ends justify the means"
    Kwa kifupi programu yao ina tokeo ADILIFU kupitia njia OVU.
    Badala ya kuchangia kupitia sms wangeanzisha mpambano wa kitaaluma kisha washindi ndio wanapata scholarship lakini sio utaratibu wa sandakalawe kwenye masuala ya taaluma. Go do your home work guys

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...