Waziri Mkuu wa Finland, Mhe. Matti Vanhanen ambaye aliwasili nchini kupitia Arusha siku ya Jumapili tarehe 14 Machi, 2010 kesho tarehe 16 Machi, 2010 anatarajiwa kuzindua chuo kilichoanzishwa kwa ushirikiano kati ya Serikali ya Finland na Tanzania kitakachojulikana kama “ Dar es salaam Institute for Sustainable Development”.

Chuo hicho kimeanzishwa kwa pamoja na nchi hizi mbili baada ya kumalizika kwa mchakato uliojulikana kama Helsink Process kati ya mwaka 2002 hadi 2008 ambao ulijikita katika masuala ya utandawazi na Demokrasia.
Waziri Mkuu wa huyo wa Finland ambaye atakuwepo nchini kwa ziara ya siku nne ataambatana na mwenyeji wake, Mhe. Mizengo Kayanza Peter Pinda katika uzinduzi huo.

Kabla ya uzinduzi huo, Mhe. Vanhanen atakuwa na mazungumzo na na mwenyeji wake na baadaye kuonana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete. Makao yake ya muda kwa sasa yuko katika eneo la Sasatel House, Coco Beach Dar es salaam.

Jana tarehe 15 Machi, 2010, Waziri Mkuu wa Finland alipata nafasi ya kutembelea eneo la Mbuga ya Wanyama ya Manyara na Hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro.

IMETOLEWA NA WIZARA YA
MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA
14 MACHI, 2010

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Michuzi Hongera kwa kutuletea hii habari,
    Tunashukuru sana na watu tuliokuwa tunaufahamu huu mchakato tunamkaribisha mgeni wetu hapa nyumbani...
    Swali la Kizushi...Hivi hawa Wizara ya Mambo ya Nje na ushirikiano wa Kimataifa" hawana hiki kitu inaichoitwa TOVUTI yaani WEBSITE?? Maana nimejaribu moja ilikuwa mfaic.go.tz holaaa hakuna kitu sasa wanawasilinaje huko nje na wanashirikianaje na wenzao wa dunia nyingine...
    Kama wameshindwa hata kuwa na TOVUTI basi waingie Ubia na Michuzi wapewe anuani ndani ya blog yake

    Mfano
    www.issamichuzi.blogspot.com/Mamboyanje
    It make sense maana Michuzi is very popular kuliko hata hiyo wizara....Ni maoni Binafsi tuu

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...