Kampuni ya African Barrick Gold (ABG) leo imetangaza kwamba ajali ya kuporomoka kwa mwamba iliyotokea katika mgodi wake wa Bulyanhulu mnamo Machi 16 2010 imesababisha vifo vya wafanyakazi wake watatu.
Wafanyakazi waliopoteza maisha kutokana na ajali hiyo ni Bw. Dickson Kadelema (36), aliyeajiriwa mnamo mwaka 2003 na alikuwa akifanya kazi kama dereva wa mashine ijulikanayo kwa jina la Jumbo, Bw. Vedastus Wilfred Tandise (33), mchimbaji ambaye alijiunga na mgodi wa Bulyanhulu mnamo mwaka 2008 pamoja na Bw. Joel Mathew Nicholas (34), ambaye pia alikuwa mchimbaji tangu mwaka 2007.
Kikosi cha Uokoaji cha Mgodi huo kilipelekwa katika eneo la tukio mara tu baada ya tukio hilo kutokea Machi 16 na kilikuwa kikifanya kazi masaa yote katika jitihada za kuwaokoa wachimbaji hao. Kwa bahati mbaya jitihada za uokoaji hazikufanikiwa.
Shughuli za uchimbaji zilisimamishwa ili kupisha shughuli za utafutaji na uokoaji wa majeruhi. Shughuli za uchimbaji zitaendelea kusimamishwa kwa muda wa siku moja (Machi 18) ya maombolezo kama ishara ya heshima kwa waliopoteza maisha.
Eneo la tukio litafungwa mpaka hapo uchunguzi utakapokamilika na sababu ya ajali kujilikana na hatua kuchukuliwa.
Maneno katu hayawezi kuelezea huzuni kubwa tuliyonayo kwa kuwapoteza wafanyakazi wenzetu. Tuko pamoja na familia na marafiki zao katika fikra na maombi; na tunatoa heshima katika kuwakumbuka,” alisema Bw. Dave Anthony, Afisa Uendeshaji Mkuu, ABG.
Timu ya wachunguzi waandamizi wa Barrick imekwishapelekwa ili kuanza uchunguzi kamili na wa kina wa ajali hiyo. ABG inazingatia sana usalama wa kila mfanyakazi wake na itaendelea kuliweka mbele suala la usalama katika migodi yake.
Barrick nchini Tanzania haijapata ajali yoyote ya kusababisha kifo tangu mwaka 2006 na mgodi wa Bulyanhulu ulitunukiwa Tuzo ya Kitaifa ya ubora katika Mfumo wa Usalama na Afya iliyotolewa na Mamlaka ya Usalama na Afya Kazini, Tanzania, mnamo mwaka 2009.
Kwa taarifa zaidi
PR & Communications Manager
African Barrick Gold
+255 (22) 216 4229
+255 767 308 600

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 14 mpaka sasa

  1. Bwana ametoa na Bwana ametwaa, jina lake lihimidiwe. Mungu awapumzishe pema ndugu zetu, Amina.

    ReplyDelete
  2. Frankly speaking, Hawa Barrick wamekuwa wakitolea ufafanuzi kuwa uokoaji ulianza constant toka tukio lilipotokea. Hii inafanya watu tuamini kuwa waliofukiwa ni watu 300 na 297 wameokolowa na watatu wamefariki.

    Lakini si hivyo ni watu watatu tu walionaswa sasa uokoaji gani huo unaofanyika more 24 hours kwa watu watatu tu?. Hawa jamaa Hakuna walichofanya zaidi ya Publicity tu, hawana kikosi chochote Imara cha kupambana na Maafa na wote huu ni usanii mtupu.

    Mungu awale pema wahanga wa uzembe

    ReplyDelete
  3. wewe anon no2 hapo juu, mimi sipo katika eneo la tukio ila napenda kuzungumzia jambo moja ufahamu kwamba inapotokea ajali,kwa kuwaokoa waliokumbwa na janga wakiwa hai huwa inategemea factors nyingi kama ifuatavyo:-
    1.aina ya majeraha waliyoyapata mara tu ktk tukio, yanaweza kuwa ni majerahaya ambayo hata kama ungetumia dakika 2 kuwatoa katika tukio bado huwezi kuokoa uhai wao.
    2.muda walipopata majeraha hadi muda wa kuwafikia na kuwapa msaada wa kidaktari,hii itagemea mahali pa ajali kufikika,ugumu au urahisi wa kufukua vifusi huku ukizingatia tahadhari za kutosababisha majeraha zaidi kwa waathirika,vifaa unavyotumia ktk mazingira husika n.k
    3.kama wamefikiwa na kutolewa wakiwa bado hai na majeraha pia inategemea uwezo wa kivifaa walionao watoa huduma,wanaweza kuwa na nia,na uwezo lakini vifaa vya hospitalini visiwepo vinavyokidhi kutoa huduma hitajika kwa aina ya majeraha.
    hivyo basi,nivyema tunapozungumzia swala la binadamu mwenzetu kupoteza uhai,tusiishie tu kulaumu,bali ia tuangalie na halihalisi inayozunguka tukio zima.
    sikuzote kuzuia ni bora,na kama kwasababu zisizoweza kuzuilika jambo limetoke,basi chamsingi ni kukubali kilichotokea.

    ReplyDelete
  4. "Barrick nchini Tanzania haijapata ajali yoyote ya kusababisha kifo tangu mwaka 2006 na mgodi wa Bulyanhulu ulitunukiwa Tuzo ya Kitaifa ya ubora katika Mfumo wa Usalama na Afya iliyotolewa na Mamlaka ya Usalama na Afya Kazini, Tanzania, mnamo mwaka 2009"

    JE NUKUU HII ILIKUWA INA MAANA YEYOTE CHANYA?


    Elewa kuwa Vifo vinaweza kusababishwa na machimbo ya madini kwa madhara ya uvutaji hewa chafu au hata kazi ngumu ambapo wahanga wanaweza kukutwa na maradhi hadi vifo polepole baada ya muda mrefu. Na hii hutokea pia kama ajali maana haikusudiwi.

    Kama mmetuniukiwa Tuzo je kuna uhusiano gani na kutoa taarifa za vifo leo? Usiwe kama ulikuwa unajibu tuhuma fulani hapa bila kujijua!

    Barrick tupo tayari kuwasaidia namna ya kutoa kauli zisizo na utata kwa ajili ya PR yenu.

    ReplyDelete
  5. We Anon wa Wed Mar 17, 10:10:00 PM

    Acha theory zako za kwenye Chibuku/Chicha, kama hukuwepo ya nini kudandia mambo usiyoyajua. Hawa barrick wamekuwa Defensive sana katika kutoa habari yote ya ajali hii. Jana walituambia wamesikia sauti za watu chini ya mgodi wakasema bado wazima. Ukweli ni kwamba hawa Barrick wanachofanya hapa ni sawa na kupingwa ngumi ya pua na Panya ukabaki unatoka damu halafu panya kakimbia. Hawa jamaa hawana Kikosi Imara cha uokoaji ni usanii mtupu. Hebu fungua link hapo chini usikilize habari kabla ya kurukia usiyoyajua. (Mimi Anon wa 2 hapo juu)

    http://www.bbc.co.uk/mediaselector/check/swahili/meta/tx/swahili_1530?size=au&bgc=003399&lang=sw&nbram=1&nbwm=1

    ReplyDelete
  6. Kwanza kabisa natoa pole kwa ndugu, jamaa, wafanyakazi wa BGM na marafiki wa karibu wa waliofariki kwa ajali hiyo.
    Ule mgodi mimi naujua vinzuri sana kuanzia juu mpaka chini na nimefanya kazi Underground kabla sijaja huku UGAIBUNI. Ajari ya namna hiyo ikitoke sio swala la kuaza kulaumiana katika swala la uokoaji. Mwamba unaweza kuanguka lakini usiwaangukie ukawa umeanguka karibu na hao watu lakini ukaziba sehemu ya waliyoingilia na hapo kunajinsi ya uokoaji na ikitoke mwamba ukawaangukia watu hilo linakuwa jambo jingine. Kwani upigaji baruti ndo swala la haraka sana kutoa kifusi hicho kwani kifusi hicho huwa sio mchanga ni mawe na upigaji wa baruti ni hatari pia kwani kwa haraka huwezi jua watu hao wapo eneo lipi. Kwahiyo swala la uokoaji kuchukua muda mwingi mimi sipingani nao inategemea na ugumu wa eneo na ukumbwa wa kifusi hicho na usalama kwa waokoaji.
    Nakumbuka wakati nafika nilisimuliwa kwamba kuna mwamba uliwahi kuangukia mashine bahati nzuri mashine ilikuwa inafanya kazi eneo lile kwa rimoti. waokoaji walipofika mashine ilikuwa bado ikisikika ikiunguruma na ilikuwa haijaangukiwa na mwamba ila mwamba umeziba tu eneo la kuingilia na uokoaji wake ulikuwa mgumu sana ambapo waliamua ku Back fill eleo lile na kufukia mashine palepale kutokana na sababu za usalama zaidi na kuhama eneo la uchimbaji.
    Kwahiyo nachoweza kusema ni kwamba tusilaumu swala la uokoaji ila tuungane kuomboleza vifo vya ndugu zetu wapendwa na tuwaachie wataalamu wachunguze zaidi ili kuimarisha usalama zaidi kwa kutotokea tena tatizo kama hilo.
    MUNGU azilaze roho za marehemu mahali pema peponi
    AMINA

    ReplyDelete
  7. we anon no.2 inaelekea una hasira za mkizi tu,lakini inabidi ujifunze kupima mambo kabla hujaanza kuhukumu kwa kauli zako maishani. alichokizungumza huyo x-worker wa barrick ndicho nilichosema na nichamsingi sana. tatizo watu wengine mko desparate na kwahasira mnaamua kuwahukumu tu wengine kwa kilajambo bila hata kusubiri kupata ukweli wa jambo husika. ingekuwa basi ni kirahisi kama unavyofikiri maswala ya uokoaji,naamini hata tukio la sept 11 2001 nchini marekani hakuna ambaye angepoteza maisha mle ndani ya kifusi,maana marekani ndilo taifa ambalo kwa hapa duniani lina uwezo mkubwa na kwa harakaharaka kwajinsi ninavyoona mtizamo wako,basi visingepaswa kutokea vifo huko katika vifusi maana wangetumia sijui teknolojia gani kuwaondoa ndani ya sekunde kadhaa,lakini tukio la uokoaji lilichukuwa muda mrefu,na wengi walipoteza maisha hata baada ya muda flani kupita huku wakisubiri kuokolewa.
    tukio la pili ni lakuzama meli nchini urusi NYAMBIZI YA KURSKY ,kama unakumbuka pia pamoja na juhudi zote hadi kushirikana na ufaransa na marekani lakini bado watu walipoteza maisha.
    hivyo kwa mtu mwenye upeo wa kufikiri,huwa anapima mambo kutokana na halihalisi na mazingira ya tukio.
    kusikika sauti chini,hakumaanishi kwamba nirahisi kufika huko na kuwaokoa,au kuwafikishia basi angalau hewa na chakula waendelee ku survive hadi upatikane ufumbuzi.
    sikulaumu maana wewe huo ndiyo upeo wako unapoishia,mzee wa kulaumu,but put in their shoes first. siajabu hata wewe kuna mambo ya kawaida tu katika maisha ambayo kwa mazingira flani yanakufanya uwe hapo ulipo na pengie hukupenda kuwa ktk hali flani unayolazimika wakati mwingine kuwemo,je nawewe wengine wakulaumu kwakuwa uko katika hali uliyomo?. nimimi anon no3.

    ReplyDelete
  8. anon wa 17 march 08:59 00 pm mzee wa kuhukumu,napenda nikupe live example.kuna watu wa aina yako ambao kwamfano akisikia flani katuhumiwa kuuwa na ushahidi wa awali ukaonyesha alihusika basi akihukumiwa kifo unataka anyongwe papo hapo maana kahukumiwa na adhiibiwe kama muuwaji.
    sasa 30 yrs ago ilitokea tukio la ukweli nchini spain ambalo lilipelekea kufutwa hukumu ya kifo nchini humo.
    kuna kijana mmoja mwanafunzi alituhumiwa kuuwa,na ushahidi wa awali ukaonyesha kweli kanakwamba alihusika na akahukumiwa kifo.
    siku ya kunyonga kama ilivyopaswa kufanya alikalishwa kwenye kiti na kufungwa mikono kila mkono kwenye egemeo lakiti. kisha kuvishwa ringi kichwani ili kukifix kwenye sehemu ambapo kuna screw ndefu imeunganishwa kwenye pedal inazungushwa hadi inatoboa fuvu tokea kisogoni hadi kwenye paji,kisha ndipo mtuhumiwa hufa polepole kwa mateso ili kukomesha mauwaji.
    dogo alinyongwa kikatili hivyo,kama muuwaji,lakini baada ya miaka kadhaa kupita,ikagundulika siyo yeye aliye uwa bali mashahidi walikosea.
    sasa kwa kauli za kuhukumu harakaharaka hayo ndiyo matokeo.nahilo likasababisha wakajifunza na kuifuta hukumu ya kifo haitekelezwi huko spain.
    najuwa hakuna direct connection ktk tukio hili na maafa ya huko mgodini,ila nazungumzia reaction yako ya kuwalaumu barrick eti hawakuwaokoa. na nadhani ungekuwa hakimu sasahivi ungesha wa hold responsible barrick. subiri wachunguze kisha serikali itatoa tamko nini mkasa mzima!!
    siwatetei barrick lakini pia sikubaliani na kauli zako.

    ReplyDelete
  9. Hivi wanvyo-declare vifo ina maana hizo maiti zimepatikana au wameachia wafe taratibu.....maelezo mengi ila kuna missed point.....where are the dead bodies...inawezekana bado wako hai ndani ila kilichosimamishwa ni garama za kuwafikia!.....insurance cover ya hawa wafanyakazi wa "kifo-mkononi" ikoje?.....HIZI NDO HOJA ZA MSINGI badala ya kukimbilia kulia lia ooo rest in peace....rest in peace kitu gani mbele ya mazingira hatarishi kama hayo!....

    ReplyDelete
  10. Mungu awalaze marehemu mahali pema, pia asaidie ndugu na jamaa kuwana Imani kyk wakati huu mgumu. Mataraji pia watu wa barick watatengeneza miundo Omar kyk sehemu ya kazi, ili kuepuka matukio Kama Gaya baadae. Familia za wafiwa pia zinastahili kupewa fidia

    ReplyDelete
  11. Poleni wafiwa, wafanyakazi wa mgodi na mgodi.

    Lakini imekuwaje tena, taarifa tulizokuwa tunazisikia hadi jana ni kwamba waokoaji walikuwa wanaweza wanasikia kelele au sauti za wahanga. Wamekufa vipi?

    Basi hizo sauti hazikuwa za watu bali mashetani ya mgodini au?

    ReplyDelete
  12. PR ya kijinga sana hiyo kusema kuwa hawajawahi kupata ajali tangu 2006..waifute hiyo kauli la sivyo sisi ndugu wa marehemu tutawashtaki maana kama vile sisi ndio nuksi tumeleta hiyo ajali???

    ReplyDelete
  13. Ukiacha hili, mbona suala la uchafuzi wa mazingira limepewa kisogo. Kuna picha za waathirika kwenye mtandao, watuambie kwamba ni isolated cases au la!

    Kama hujui haya nenda: vijanafm (dot) com.

    Sitegemei hii comment 'kuona mwanga wa jua.'

    ReplyDelete
  14. Naungana na mdau aliyepata kufanya kazi Barrick kabla ya kutimkia ughaibuni. Ni mapema mno kuwahukumu Barrick. Ni kweli Barrick suala la usalama kazini wanalipa umuhimu. Wengine wanaweza kusema ni kwa sababu wanajali na wengine wanaweza kusema ni kwa sababu wakiwa na rekodi ya ajali nyinginyingi basi wanalazimika kulipia shirika lao hela nyingi katika bima ya ajali. But that's not the point. Barrick wanavyosema toka 2006 hajapata mtu ajali ya kupoteza maisha maana yake ni kuwa mara ya mwisho mtu au watu kupoteza maisha kazini ilikuwa 2005. Draw your own conclusions from that.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...