Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani
nchini afande Mohamed Mpinga akiongea na wanahabari eneo la tukio leo
umati mkubwa ukishuhudia matokeo ya ajali hii mbaya iliyotokea Kibamba leo ambapo watu wapatao 11 walipoteza maisha hapo hapo
mmoja wa walionusurika akiondolewa sehemu ya tukio miili ya waliopoteza maisha ikiondolewa. kwa kweli inatia uchungu na kuzua maswali kifanyike nini ajali zipungue kama si kutkomea kabisa na wasio na hatia wasipoteze uhai namna hii

mwili ukiondolewa kwenye daladala

daladala likiondolewa kwa winchi
daladala likiondolewa
majonzi na simamanzi wakati daladala likiondolewa mtaroni
Watu 10 wanasemekana wamefariki hapo hapo baada ya tenji la mafuta kuligonga na kisha kuliburuza mratoni na kulilalia daladala katika ajali ilitokea Kibamba watu kumi papo hapo. Picha na Francis Dande wa Globu ya Jamii
Picha na habari na
Francis Dande wa Globu ya Jamii

Ajali mbaya ya barabarani imetokea leo alfajirri wakati Lori la mafuta lilipoigonga gari ndogo ya abiri na kuuwa watu 11 hapo hapo katika barabara ya Morogoro eneo la Kibamba CCM Wilaya ya Kinondoni.

Kwa mujibu wa mashuhuda walioshuhudia ajali hiyo walisema kuwa, ilitokea majira ya saa 10:30 alfajiri wa leo wakati lori hilo likitokea Dar es Salaam kuelekea mikoa jirani na kuligonga kisha kuliburuza kwa umbali mrefu kabla ya kulilalia kwa juu na kusababisha vifo hivyo vya watu hao 11.
Kamanda wa Kikosi cha Usalama barabarani Mohamed Mpinga alifika eneo la tukio na kuthibitisha kutokea kwa ajali hiyo majira hayo ya saa 10:30 eneo hilo la Kibamba CCM wilayani Kinondoni.

Amesema ajali hiyo ilihusisha gari la abiria lenye namba za usajili T615 AJW aina ya Hiace ambayo dereva wake hakuweza kufahamika iliyokuwa ikitokea Kibamba kuelekea katikati ya jiji na Lori(lililobeba mafuta) T182 ABP aina ya Iveco mali ya Mahamud Mohamed likiendeshwa na Kudura Adamu.

Kamanda Mpinga alisema hadi sasa ni maiti wanne ndio wametambuliwa majina yao kuwa ni pamoja na Abuu Twalibu Twaibu mfanyakazi wa Bandari, Shukuru Hussein kondakta wa Hiace hiyo, Ester Christino, Faraja Issa na Zainabu Ali ambaye alikuwa mjamzito akielekea hospitali kwa ajili ya kujifungua.

Hata hivyo, alisema miili ya marehemu hao imehifadhiwa katia hospitali tatu tofauti. Amesema mili ya watu wawili imehifadhiwa katika hospitali ya Tumbi, wanne wamehifadhiwa katika hospitali ya Mwananyamala ambao ni Abdalah Twalib, Zaina Ali, Faraja Issa na mmoja amaye hajatambulika.

Kamanda Kapinga alisema wengine

watano wamehifadhiwa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

Kamanda Mpinga alisema lori hilo lilokuwa limebeba mafuta ya taa lilikuwa likitokea Dar es Salaam kuelekea Isaka, Kahama, Mkoani shinyanga.

Kamanda Mpinga alisema ajali hiyo ilitokana na uzembe wa dereva wa lori la mafuta baada ya kutaka kulipita gari lingine huku akiwa kwenye mwendo kasi na kuligonga gari hilo dogo la abiria lilokuwa na abiria hao 11 ikiwa
ni pamoja na dereva na kondakta wake katika basi hilo dogo

Mpinga alisema kutokana na mazingira ya ajali hiyo kuwa mbaya kwa lori hilo lenye uzito wa tani 30 kulilalia gari dogo na kulisaga kabisa na kuonekana kama chapati limefanya uokoaji kuwa mgumu hata baada ya magari matatu ya breakdown kujaribu kuliinua lori hilo.

Alisema zoezi hilo la kuliondoa lori hilo kwenye eneo la ajali lilifanikiwa baada ya kuomba msada wa Kampuni ya Effco inayomilikiwa na Elimlingi Mtui huku wakisaidiana na waokoaji wengine walioopoa miili hiyo, wakisaidiana na askari wa Kikosi na Ukoaji na zimamoto, Msalaba Mwekundu na wananchi.

Kamanda Mpinga alisema bado serikali inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na uhaba wa vyombo vya uokoaji kama ilivyojitokeza leo. Hata hivyo, alisema anatambua kuwa eneo hilo ni la hatari kutokana na kuwa na mteremko mkali na mlima.

Mpinga alieleza masikitiko yake kwa baadhi ya madereva wasiojali kwani pamoja na kuwekwa matuta wamekuwa wakidaharau na kujaribu kwenda kasi na kukiuka kanuni sheria za usalama barabarani. Dereva wa Lori inasemekana alitoroka na msako umeanzishwa kumsaka.






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 45 mpaka sasa

  1. TANROADS AAMKENI HIO MIFEREJI MIREFU PEMBENI MWA BARABARA YA MOROGORO INAHITAJI VIZUIZI. HIVI NYIE WAHANDISI MMENDA SHULE GANI JAMANI........KILA SIKU TUNALALAMIKIA HIO MIFEREJI MIPANA NA MIREFU LAKINI HAMUSIKII. INABIDI MUWAJIBIKE. NILIPOSEMA TANZANIA TUNAMATATIZO MENGI HATA HATUJUI TUANZIE WAPI NAONA SASA MNANIELEWA.
    NDIO TUNAELEWA KUWA MLISAIDIWA NA WADANIMAK KUSANIFU NA KUJENGA HIO BARABARA. NI JUKUMU LENU KUHAKIKISHA ZINAFIKIA KIWANGO CHA USALAMA WALAU WA WATUMIAJI WA MAGARI.
    POLENI FAMILIA ZILIZOPOTELEWA NA WAPENDWA.

    ReplyDelete
  2. kweli binadamu ni kama Maua,Mungu awape mwangaza wa milele,lkn huu udhembe lazima utafutiwe ufumbuzi makini mapema inavyowezekana kupunguza vifo visivyo vya lazima.
    i)Jesh la polisi:Usimamizi madhubuti ktk ukaguzi wa Magari na utoaji wa leseni za udereva na Magari.
    ii)Madereva:Umakini ktk uendeshaji,angalia huyo alivyoua wenzake.Tujifunze na tujirekebishe.
    iii)Serikali:Itunge sheria kali kwa wale wote watakaobainika kuwa chanzo cha ajali kama hizi,ikiwa ni pamoja na kifungo cha maisha maana hii haina tofauti na uuaji.

    ReplyDelete
  3. jamani mungu azilaze roho zao mahali pama peponi...

    Jamani hawa wenye malori wangetafutiwa tu njia yao ya kupita leo kama hivyo imetokea ajali hiyo na hata kwa jioni nakuwa usumbufu sana kwa sie wakazi wa maeneo ya kimara na hwa madereva wa malori ni wajeuri wasio hata na huruma kwa magari madogo watafutiwe tu njia yao ya kupita

    ReplyDelete
  4. jamani inasikitisha sana ni ajali mbaya sana.poleni sana wafiwa.mungu ziweke roho za marehemu mahali pema peponi,amen.bwana ametoa bwana ametwaa jina la bwana libarikiwe

    ReplyDelete
  5. Ajalihiyo imenifanya nijiulize. Hivi kiburi na jeuri ambayo mara kwa mara huwa inaonyeshwa na madereva na makonda wa daladala dhidi ya abiria na hasa wanafunzi je huwa wanakumbuka kuwa kutokana na kazi yao hiyo mauti huwa yanakuwa hayakombali nao? Na kwamba wanatakiwa kuonyesha upendo kwa binadamu wenzao na wasimuudhi Mola? Sijui yalikuwa ni mazingira gani waliokuwemo wakatiwa ajali hiyo

    ReplyDelete
  6. jamani njamani serikali wapo wapi watu wanpoteza maisha kizembe hivi kila siku kwenye hii barabara tuu kwanini malori yasitengewe barabara yao ya kuingia mjini mpaka yajichanganye na magari madogo? ni nini jamani serikali

    ReplyDelete
  7. Hiace imepondekapondeka kama kitumbua na kupona hapo ni miujiza.

    Mungu Awalaze marehemu mahali pema. Inasikitisha!

    ReplyDelete
  8. WANASIASA PUNGUZENI MATUMIZI YENU MAKUBWA YA KODI ZA WANANCHI ILI MAPATO YA SERIKALI YABORESHE HUDUMA ZA KIJAMII.MNATAKA MABILIONI KWENYE UCHAGUZI WAKATI SHULE ZOTE NI CHAKAVU BILA MADAWATI WALA NYUMBA ZA WALIMU.BARABARA ZETU ZIMEZIDIWA NA MAGARI NA KUNA UHITAJI MKUBWA WA BARABARA ZA KUINGIA NA KUTOKA JIJINI DAR ES SALAAM.JE ILE BARABARA YA NYERERE HAIWEZI KUBORESHWA ZAIDI HADI MLANDIZI ILI MSONGAMANO WA UBUNGO NA KIMARA UPUNGUE?

    ReplyDelete
  9. Serikali, amka sasa. Watu tunateketea. Badilisha sheria. Weka sheria kali. Sheria za faini ya TZS 20,000 hazina maana tena. Kazi ya serikali yoyote iliyo makini ni kulinda raia wake. Kila siku mnasema sheria zimepitwa na wakati, kwani haziwezi kubadilishwa? Sheria zilitungwa na binadamu hizo, binadamu huyo huyo ana uwezo wa kuzibadilisha. Za Mwenyezi Mungu tu ndio hazibadilishwi.

    ReplyDelete
  10. Wal-lwaaahi,kuanzia leo nikipanda dala dala, dareva akianza kuleta madoido tu, au mbwembe naomba kushuka hapo hapo.
    Potelea mbali kuchelewa au kulipa nauli mara mbili,
    Hii ajali naamini kwa asilimia zote kwa dereva wa kipanya alikua anatanua kama wanavyo sema wenyewe.
    Modereva viburi roho kolo koloni.

    ReplyDelete
  11. Roho za marehemu wapate rehema kwa Mungu wapumzike kwa amani, amina.
    Agp.

    ReplyDelete
  12. Maroli yatafutiwe njia zake, Serikali lioneni hili.

    Udhibiti wa madereva wa daladala hakuna si vyombo vya dola wala abiria wenyewe. Abiria wadhibiti wadereva wanaoendesha ovyo, roho hazina spea jamani. Mbona vibaka mnawachoma moto? kwani hawa si sawa nao tu.

    Poleni familia za wafiwa. Mungu awapumuzishe marehemu mahali pema. AMEN

    ReplyDelete
  13. My prayers and thoughts are with family members of those who have lost their lives. Amen. Nini kifanyike kupunguza hizi ajali za kijinga kama gari kutokuwa na break? The simple answer ni implementation ya sheria zilizopo kwenye makaratasi. Hakuna haja ya sheria mpya. Sheria zote nzuri zipo Tanzania kazi ni utekelezaji. Utekelezaji unakuwa mgumu kwa sababu ya rushwa, watu kuwa wababaishaji na kutokuwa responsible with what they should be responsible.

    ReplyDelete
  14. kutafutia malori njia zake sidhani kama ndo suluhisho la ajari hizi. Uendeshaji wa ovyo-ovyo ndiyo chanzo cha ajari zote hizi.

    ReplyDelete
  15. Poleni wafiwa.

    Hivi ni lini Watanzania tutakapoona kwamba ajali sio kitu cha kawaida na kuacha kusingizia 'kazi ya Mungu'?

    Kwa nini kila zikitokea ajali tunakurupukia mara gavana, mara teknolojia gani wakati asilimia kubwa ya ajali zinasababishwa na binadamu, wakiwemo madereva, kutozingatia kanuni za usalama?

    Tunataka kitokee nini ndio tuone kwamba tunahitajika kubadilika?

    Kwa nini tuna haraka sana tunapokuwa nyuma ya usukani wakati mambo mengine yote tunafanya polepole?

    Barabara za Dar watu wanaendesha tu kwenye taa nyekundu bila aibu. Hakuna anayefuata upande wake. Ukisimama kwenye taa nyekundu unapigiwa honi. Yote tunaona kawaida.

    Chuo cha Usafirishaji wanatoa mafunzo mazuri sana ya udereva. Iwekwe kanuni kwamba madereva wa magari ya abiria na ya mizigo lazima wapitie mafunzo pale. Kanuni ilazimishe madereva hawa kupata certification kwa kupata mafunzo ya kupigwa msasa mara kwa mara.

    ReplyDelete
  16. kuna habari nimezipata hivi punde kuwa kuna ajali nyingine imetokea hapo kibamba usiku huu ikihusisha malori mawili na kuna wananchi kadhaa wamepoteza maisha !

    ReplyDelete
  17. mimi binafsi nadhani tatizo ni speed na madereva wasiotakiwa kuwepo barabarani(walevi, bange na wasio kuwa na driving licence ambazo halali) nimekaa katika nchi ambazo zina magari zaidi ya Tanzania na sijawahi kuona ajari kama hizo zinazotokea kila siku Tanzania, na hiki tokea ujuwe itakuwa breaking news, Viongozi wanchi yetu wamesoma,wametembea nchi mbali mbali duniani na ninauhakika leo kuna kiongozi mwingine anaenda katika Tour ya kimataifa Europe, sasa mi swali langu, huwa wanaenda kujifunza nini,au kujaza nafasi tu?

    Sirikali inabidi iangalie usalama na ustawi wa wananchi wao,nadhani ni sisi ndio tunao wachaguwa na kwahivyo nadhani kama kuna DEMOCRACY nadhani sisi raia tuna nguvu yakuwaondoa... Amani

    ReplyDelete
  18. SAHIHISHO
    Kampuni EFFCO ambayo ilisaidia kuinua tanker kwa kutumia crane yake ya Tadano tani 35 inamilikiwa na kampuni ya Southern Africa Enterprise Development Fund (SAEDF) ya South Africa. Elimringi Mtui ni General Manager wa EFFCO.

    ReplyDelete
  19. MDAU WA KWANZA BRAVOOOO SANA UMENENA .....SASA WABEBA BOX TUKISEMA WAHANDISI WABONGO HAMNA AKILI NA UWEZO WA KUDESIGN NA KUJENGA FLYOVER ROADS MNAKUJA JUUUUUUUUUU......HEHEH AKILI YA KUONA MIFEREJI HIYO PEMBENI MWA ROAD NI MITEGO MLOJIWEKEA WENYEWE...MAGHOROFA MKIJENGA NYIE SIKU MBILI TU YANAANGUKA...MADARAJA YENU NDO WALA HATA SISEMI................LEO MNAKASIRIKA TUKIWAAMBIA WAZUNGU NDO WANAWEZA JENGA FLYOVER ROADS........WAHANDISI WABONGO AKILI HAMNA MKUBALI MKATAE........


    MBEBA BOX #1

    ReplyDelete
  20. yaani inasikitisha sana! yani hamna comment ila kuwapa pole saanaa familia za wafiwa. mungu ameamua iwe hivyo na awalaze pahali pema. lakini na serekali ya tanzania iko wapi kuvumilia mauji makubwa kama haya? TATIZO HIZO BARABARA KUBWA ZA KWENDA MIJI MINGINE NI LAZIMA ZIWE "DUAL CARRIAGEWAY WITH 2 LANES IN EACH DIRECTIONS"NA SPEED LIMIT IWE 60MPH KWA MAGARI YA TRANSPORT SIO SINGLE LANE NA SPEED YA 120MPH, BILA HIVYO AJALI ZITAKUWEPO SANAA. inasikitisha kuona inchi kama TANZANIA yenye uchumi mkubwa haina hizo barabara. sijui viongozi wanafikiria nini? wakulaumiwa ni serekali! mdau toka bujumbura

    ReplyDelete
  21. POLE KWA WAFIWA NA ROHO ZA MAREHEMU ZILALE PEMA-AMEEN
    KWA MUDA MREFU NAJIULIZA HII MITARO KAMA MITEGO JAPO TULIJENGEWA KWA MSAADA JE WAHANDISI HUSIKA HAWAWEZI KUTOA MAWAZO MAREKEBISHO YAKAFANYIKA?
    YAANI UKIKWEPA AJALI UNAPATA AJALI...WAWEKE KINGO NA JAPO MIFUNIKO
    HASA MAENEO KARIBU NA MIJI! HATA WAENDA KWA MIGUU NI RAHISI KUPOROMOKEA HUKO..INAWEZEKANA HIACE INGECHANJA MBUGA KUOKOA ROHO ZA WATU..TANROAD+MAINJINIA HILI VIPI..?

    ReplyDelete
  22. Kwa kweli suala la usalama ni la kuangalia upya katika hizi barabara. Mimi sijaona nchi ambayo mifereji iko kando wazi kama hii ya barabatrta ya Morogoro. Lakini kama alivyosema mwananchi mmoja hapo juu, TANROADS waamke na viongozi waache tabia ya kupoteza mabilioni ya fedha za walipakodi kwa kukimbizana na safari za nje ya nchi zisizo na tija, wakati wananchi wanapoteza maisha kwa uzembe mdogo sana.

    ReplyDelete
  23. Kufa kwingine kunauma.. hii mbaya.. mi nilikuwa napiga trip za kila siku na vipanya kati ya Maili moja na Ubungo... nikawa nawaza.. humu tulivyokaa.. ikitokea ajali.........
    Hii imeuma..
    Vipanya vipigwe marufuku kabisa.. daladala ya chini iwe ukubwa wa 'DCM'

    ReplyDelete
  24. MIMI NASHANGAA SANA ,PESA ZA UTALII,BANDARINI, AIRPORT UTALII, ZIKOWAPI NA VIONGOZI WAKOWAPI NA MAWAZIRI WANAOSHIKA NAFASI ZA USALAMA MAENDELEO YA MJI WAKOWAPIIIIII!?? NA NDUGUZETU NDIO KAMA HIVI WANA POTEZA ROHO KWA UZEMBE WA WATU WACHACHE WANAOKULA PESA ZETU KWA KUJAZA MATUMBOYAO,HII HAINGI AKILINI KUONA MFEREJI /MSINGI KAMA ULE HAUNA HATA KUZIBWA JUU UPO OPEN HATA HUKUTI ALAMA YOYOTE ITAKAYO KUHATARISHA KAMA KUNA MFEREJI/MSINGI MBELE,TUNASOMA MPAKA AJALI ITOKEE ,KWELI KESHO NDEGE IWAKEMOTO AIPORT TUTAWEZA KUOKOA MAISHA NDUGU ZETU ,HAYA NIYALE KAMA YALIOTOKEA ZIWA VICTORIA MELI KUZAMA NA KUITWA WAOKOZI KUTOKA SOUTH AFRICA AYSEE INANACHOSHA SANA NA,VIONGOZI MPOOO,BASI BORA KUNUNUWA SPEED CAMERA,NA MOVING CAMERA ZA BARABARANI,KUWE NA TRAFICK LIGHT KILA MAILL FULANI,NAMENGI TU KULIKO KUNUNUA MTAMBO WA MILIONI KWA KUANGALIA NDEGE ANGANI

    ReplyDelete
  25. Nakubaliana na commentz kadhaa za wa2 walioandika aerlier ya kwamba Maroli yatafutiwe njia yao, pili Mwenye kipanya inaelekea alikuwa anawai nyomi nyomi la nyiongeza. Wakubwa wa nchi mshasafiri nchi nyingi na mmejionea bara bara za wenze2 zipoje. Je mnashindwa kufanya kila bara bara kuu mikoani ziwe mbili au tatu. kwenda mbili kurudi mbili na za mikoani vipande vingine muwe munwaweka mikeka mitatu. Ajali nyingi za Tz zinatokea sababu ya wa2 wanataka kuover take na bara bara yenyewe lane moja pia awangalii mbele kuna nini. Tatizo kubwa ni bara bara, kama 2ngekuwa na bara bara mbili mbili nahisi ajali zingekuwa ndogo sana. N,way MUNGU awaweke wa2 waliopoteza maisha ktk ajali hii mahari pazuri, amin. Mola wape makazi mema pepon, amin
    Kigogo Boy

    ReplyDelete
  26. niliangusha chozi,,,yani wamekufa vibaya hawa?sikuelewa dereva alikua anawai nini uyo wa lori na uyo dereva wa kipanya wana jeuri sana utakuta na yy alikua anataka apite speed!!wewe unaona m-lori unakuja spidi ya kufa mtu afu na iyo MITUTA 2 ilipo apo na wewe unajiendea tuuu spidi,ukipisha unapungukiwa nini akili izi???
    usishindane na mwenye lori au daladala maana kifo kipo mbele tu their r so rough!

    wanamaombi tupaitie damu ya Yesu mahali hapo maana kuna ajali sana,damu ikimwagika ujue kuna laana apo mahali ikiwezekana twendeni kabisa apo tupateke tuvunje roho chafu na mahali pengine pia,,,TUOMBE

    ee mwenyezi watie nguvu familia za marehemu wote

    ReplyDelete
  27. Mimi kuna komenti moja juzi nimetoa kuwa, hao vipngozi na wajumbe wote wanaoambatana nao katika ziara zote wanazokwenda nje ya nchi wakifika kule hawaendi kujifunza kitu chchote. Wanakwenda kushangaa shangaa tu kule na hatimaye kuishia kufanya shopping kubwa.
    Ni nani aliwahi kupraktizi kile alichojifunza au kuona kwenye ziara? Anyooshe mkono atuonyeshe!!

    Jana tumeona picha za watu wameambatana na waziri mkuu mheshimiwa Mizengo Pinda wakishangaa kuona vitu, mashine mbalimbali kule Japan. Mitambo inapanda mpunga yenyewe ndani hakuna mtu. Imesetiwa tu. Jamaa Pinda mwenyewe alishika kidevu kushangaa, itakuwa wajumbe wake? Na tuone kama kuna kitakacholetwa cha kuingwa toka katika ziara ile!!

    Mimi nawaambia tutaishia kupiga miluzi mingi sana na hakuna hata mmoja utakaotuletea ufumbuzi wa maendeleo. Kwanza tu wavivu wa ubunifu na kujituma, pili tu watu wachoyo, tunataka kujinufaisha binafsi, na sio umma.

    Kwa mtaji huu, hatuendelei. Mnatdanganya tu kuwa KILIMO KWANZA kumbe ni njia ya kula mitaji yetu. Tumewagundua, HATUDANGANYIKI.

    ReplyDelete
  28. vitu vingine jamani hata kutoa mawazo unashindwa, vitu vingine lazima tukubali tuu kuwa kuna nguvu za giza na kazi za shetani kwa nyakati hizi zinatawala sana, maeneo kama yale yanaitwa Black spot ni vituo vya shetani kabisa kwa ajili ya kutaka Damu, sasa basi kwa wale waombaji waendelee kuomba kwasababu hali inatisha sana, ukitaka kuangalia kwa macho ya kawaida huwezi kuona ila inabiodi kuomba sana hizi ni nyakati ngumu ambazo shetani anajaribu kuvuna kwa nguvu, Mungu atusaidie sana ndugu.

    ReplyDelete
  29. vitu vingine jamani hata kutoa mawazo unashindwa, vitu vingine lazima tukubali tuu kuwa kuna nguvu za giza na kazi za shetani kwa nyakati hizi zinatawala sana, maeneo kama yale yanaitwa Black spot ni vituo vya shetani kabisa kwa ajili ya kutaka Damu, sasa basi kwa wale waombaji waendelee kuomba kwasababu hali inatisha sana, ukitaka kuangalia kwa macho ya kawaida huwezi kuona ila inabiodi kuomba sana hizi ni nyakati ngumu ambazo shetani anajaribu kuvuna kwa nguvu, Mungu atusaidie sana ndugu.

    ReplyDelete
  30. JAMANI SI KULIKUWA NA SHERIA YA MALORI KUSAFIRI USIKU TU? INA MAANA ILIFUTWA? KAMA ILIFUTWA SERIKALI RUDISHENI ILE SHERIA. HII ITASAIDIA KUPESHA VIFO VYA WANANCHI WASIOKUWA NA HATIA. HII MILORI IKIPATA AJALI INAANGUKA YENYEWE. SIO SASA LIKIANGUKA TU LINALALIA KIPANYA CHA WATU KINAKUWA CHAPATI KABISA.

    ReplyDelete
  31. nasikia dereva wa lori alikuwa amesinzia..akastukia upo nje ya barabara,akawa hana jinsi

    ReplyDelete
  32. Watanzania tumelogwa sio bure, hivi kweli kila jambo linaloamuliwa na hawa viongozi wetu tunaliafiki na kuliona sahihi kweli, kweli, kweli kabisaaaaaaa?????? Tanroad pamoja na wizara husika kama kweli mlikaa na kuafiki hiyo nyie mnayoita mifereji mikubwa lakini mimi ninaona ni MIHANDAKI iliyo pembeni ya barabara ya morogoro ndio solution ya kupitisha maji mengi kama sio mnataka kufanya uwe mfereji wa makaburi ya watu? (hata kaburi lina mfuniko) Kwa nini kusiwe na vifuniko juu? au huo msaada wa kujenga huo mfereji ulikuwa na masharti ya kutokuweka vifuniko?
    Kuna kipindi mabreak down yalivutavuta magari yaliyokuwa yanapaki vibaya jiji la Dar maeneo ya mjini yakawa yanaharibu magari ya watu lakini hilo zoezi lilisitishwa kutokana na gari la kiongozi mmoja wa serikali kuvutwa gari lake na kuharibiwa vibaya.
    Sasa wakazi tunaotumia barabara ya Morogoro ambapo pembeni kuna hiyo MIHANDAKI tusubiri kiongozi mmoja yamkute (siwaombei) ndio mambo yatarekebishwa, hiyo ndio hali halisi ya nchi yetu.
    Mimi nawapa pole wale wote waliofiwa na wapendwa wao.

    ReplyDelete
  33. Nasikia kiligongwa kwanza, kikaburuzwa.. afu kikalaliwa.. pengine ingekuwa DCM watu wangejaribu kuruka/kuchoropoka kabla hakijalaliwa kabisa (nafasi kubwa zaidi)

    ReplyDelete
  34. INNA LILAH WAINAILAIHI RAJIUN.
    MBELE YAO, NYUMA YETU. HAKUNA KITACHOBAKI. M'MUNGU AZIWEKE ROHO ZA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI, AMEN.

    ReplyDelete
  35. Serikali ifanye chini juu huu Mtindo wa barabara moja urekebishwe kabisa kuanzia 2010, umepitwa na wakati, kwa mji mkubwa kama dar es salaam,,katika afrika miji yote mikubwa kwa mfano cairo kuna barabara mbili, hiyo njia inaepusha ajali kwa muda wote...ushauri mwigine,,malori yasitembee mchana,,, yaanze kutembe usiku kuanzia saa nne mpaka 3.a.m....

    kwa mfano kutoka morogoro kwenda dar miji ukutana,,,

    Amen, nawapa pole wafiwa,,kwa kifo kichungu kilichowakabili marehemu. inauma....

    Lucy

    ReplyDelete
  36. kweli ajali haina kinga. by mwanyika

    ReplyDelete
  37. MoID imetoa tangazo la tender ya kukagua kila gari angalau mara mbili kwa mwaka kwa kila gari!
    Zoezi likiendeshwa vyema na wakikagua magari na leseni nafikiri ajali zitapungua mno! Maana mtu unanunua gari halijawahi kukaguliwa wala nini mpaka unamuuzia mwenzio naye anadunda nalo!
    Hiyo barabara ili-design-niwa na wazungu sasa kuanza kulia na wahandisi wa bongo haisaidii ni kama kulia na madaktari kutoka na ongezeko la vichaa mtaani!

    ReplyDelete
  38. Vipanya vinachomekea sana , sasa lori hilo kubwa tena likiwa na mzigo ni vigumu sana kusimama kwa breki ya ghafla , bora vipanya vyote vipgwe marufuku , viende LUGOBA huko sio mjini hapa , na kuhusu mifereji mipana ni usalama wa wapita njia pembeni na nyumba zilizo pembeni mwa barabara , unadhani hapo kusingekuwa na mfereji mpana kama huu hiyo gari ingesimamia chumbani kwa mtu na kama sio chooni uwani . THINK ABOUT IT

    ReplyDelete
  39. Swala ni kwamba hebu cc watanzania tubadilishe huu wimbo manake wahusika hawataki kuubadilisha!Hivi mimi nikianza kushawishi kwamba katika ajali mbaya kama hizi muhusika mkuu wa usalama barabarani ajiuzulu nitakuwa nimekosea?Ajiuzulu ili kupate mawazo na uongozi mpya utakaoleta ufumbuzi badala ya visingizio visivyokwisha!Kwa madereva wazembe wanapewa na nani hizo leseni?Mimi sijasikia eti dereva aliyesababisha ajali hakuwa na leseni!Hebu tuanze kuwa serious.

    ReplyDelete
  40. ndugu mdanganyika walaumu TANROADS kwa Lipi? Je kungekuwa na Fly over kama ulaya si ingekuwa balaa Tanganyika hii mana ungekuta gari zinapaa kama ndege. Jaribu kufikiri chanzo cha ajali nini kabla ya shutuma. Matuta yale yaliombwa na wapiga kura wadanganyika wakidhani watapunguza vifo vya waendao kwa miguu!Kumbe wapi bwana wamedanganyika!Tafuta suluhu ya matatizo ni madreva kuwa na busara kidogo tu.

    ReplyDelete
  41. Mzee wa DCM nimekusoma ndugu yangu.

    ReplyDelete
  42. WALIKUWA NA PROJECT WAKUWEKA SPEED CAMERA..WALIVYOKUWA WAJINGA WANAWEKA MJINI...MISONGOMANO YA MAGARI mijini kuna ulazima gani.


    speed camera ziwekwe njia za nje ya jiji....ni project isiokuwa na pingamizi.

    nchi za wenzetu kifo kimoja kama hichi ni issue kubwa...

    kila kitu tuchukulie serious.sio measure lazima ipitishwe bungeni.

    ReplyDelete
  43. Samahani sana, lakini Tanzania hakuna dawa ya kupunguza hizo ajali zaidi ya kuweka SPEED BUMPS! Madereva wakiiacha kwenda mwendo wa kasi ajali zitapungua. Yaani ajali ilikuwa mbaya mno, hivi wengine waliokuwemo kwenye hiyo daladala watatambulika kweli? Labda kwa nguo walizovaa.

    Mungu alaze roho za waliopoteza maisha yao katika ajali hiyo mahala pema mbinguni. AMEN.

    ReplyDelete
  44. KUNA JAMAA AMESEMA HAPO JUU SHERIA YA MALORI YASAFIRI USIKU,USIKU NDIO NOMA ZAIDI WEWE MANAKE WANAKUA HAWAJALI NA WANAENDESHA ONYO ZAIDI NA MADALADALA PIA YAPO KIBAO NDIYO YATABONDWA VIZURI ZAIDI.

    ReplyDelete
  45. MsemakweliMarch 26, 2010

    kwanza Pole kwa wafiwa.
    Pili, huyo mtoa mawazo wa mwanzo aliyesema Tanroads ndio ya kulalamikia hajui anachosema.
    Ajali hii haina uhusiano kabisa na Tanroads. Tanraods walaumu sehemu nyingine lakini sio katika hii ajali kabisa.
    Angalia chanzo cha ajali: Taarifa inasema dereva wa lori alikuwa ana-overtake akanyimwa njia, akaegemea upande wa kipanya, akakiburuza na kukilalia.
    Leo nitazungumzia hili la mifereji.
    Mifereji ya Tanroads barabara ya Ubungo hadi Kibamba ni ya ulazima. Elewa na umesema kweli kwamba nchi nzingine hiyo mifereji haipo brabara kuu. Na sababu ni kwamba barabara kuu zao zilipimwa na kujengwa na kupewa ardhi kubwa itakayomwaga maji bila kuelekea katika nyumba za watu na kuleta mafuriko.
    Barabara zetu zote kuu zimevamiwa na nyumba na vimiji karibu kabisa na eneo la barabara. Nikiwa na maana kwamba huwezi jenga barabara hizi kuu na kuziacha zikiwa chanzo cha mafuriko katika vinyumba vilivyo jirani.
    Mfano Kimara to Ubungo elewa hilo ni eneo la miinuko, milima na mabonde, sasa ukijenga barabara njia mbili pia kumbuka umezuia njia asilia ya maji, hivyo lazima uipe njia ya mifereji ili imwage maji yake mwisho wa barabara. Wewe ulitaka wasiweke mifereji ili maji yalete mafuriko katika nyumba za watu kimara hadi ubungo.
    Tatu, wazo lako la kufunika hiyo mifereji kama unvyosema, ni la kusema zaidi ya kufikiria. Ukiangalia gharama za kuziba hiyo mifereji ni sawa na kujenga barabara njia tatu kutoka ubungo kwenda kimara.
    Nne sababu za kuacha wazi hiyo mifereji ni kwamba takataka zinaweza zolewa haraka na kufanya barabara kupitika bila kuleta mafuriko. Wangeweza weka mabomba mifereji (drainage sytem) , lakini tumeona matatizo yake pale mvua ikinyesha Dar mjini, drainage system zote huwa zimejaa taka na kuziba na mwisho huleta mafuriko katikati ya Dar. Njia mbadala na rahisi mifereji wazi.
    Gharama za kujenga kilometa moja tu ya lami ni milioni 500-800 za kitanzania. Piga hesabu kilometa 30 njia mbili ni kiasi gani, halafu laumu Tanroads kwa matatizo ambayo ni ya madereva au sheria za barabarani au polisi wa barabarani.
    Hizi barabara kuu hasa hii ya Ubungo- mlandizi imejengwa kwa ungalifu mkubwa kupita barabara zote za TZ, na wafadhali wakishirikiana na wahandisi wa aina zote wa ujenzi wa barabara wamefuata kila muundo kusaidia na kuhakisha hii barabara inafaa kwa hali ya TZ.
    Pia sikatai wahandisi wote katika sekta ya ujenzi barabara TZ wengi ni bora liende.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...