Afisa wa Kilimo Wilaya ya Ludewa Mkoani Iringa STANLEY SAPULA akimuonesha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. ALI MOHAMED SHEIN kilimo cha kisasa cha kahawa bora inayolimwa kwenye kituo cha kitalu cha kahawa katika kijiji cha Manyanya Wilayani Ludewa, Wakati alipotembelea kituo hicho leo kwa ajili ya kuangalia maendeleo ya kitalu hicho. Makamu wa Rais yupo Mkoani Iringa kukaguwa na kuzinduwa miradi ya maendeleo. wa kwanza kulia Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. MOHAMED ABDULAZIZI.
Afisa wa kilimo Wilaya ya Ludewa Mkoani Iringa STANLEY SAPULA kulia, akimuonesha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.ALI MOHAMED SHEIN moja ya aina ya miche ya Kahawa inayoandaliwa katika kitalu cha Manyanya Wilayani Ludewa, wakati alipotembelea katika Kitalu hicho leo. wa pili kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. MOHAMED ABDULAZIZI.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzanua Dk. ALI MOHAMED SHEIN, akiondowa kitambaa kuzinduwa rasmi mradi wa huduma ya Nishati ya Umeme wa TANESCO unaotumia nguvu za majenereta kwa ajili ya Wananchi wa Wilaya ya Ludewa leo, Jumla ya shilingi 6.3 Bilioni zimetumika hadi kukamilika kwa mradi huo. Makamu wa Rais yupo Mkoani Iringa kwa ziara ya siku sita kukaguwa na kuzinduwa miradi ya maendeleo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. ALI MOHAMED SHEIN, akihutubia Wananchi wa kijiji cha Ludewa katika mkutano wa Hadhara uliofanyika leo katika ukumbi wa mikutano Ludewa. Makamu wa Rais yupo Mkoani Iringa kwa ziara ya Siku sita kukaguwa na kuzinduwa miradi ya maendeleo.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Education and Vocational Training deputy minister Mwantumu Mahiza has expressed profound shock after she was informed that over 300 girls dropped out of school in Tanga Region last year alone due to pregnancies.

    The statistics were revealed to her at a meeting with education officers and secondary school headmasters held here on Friday.

    “This number is too big …It’s sad to hear that some of my teachers are also involved in impregnating these pupils…this is a great sin …I am an activist and all these are happening in my region. It’s a big shame and I won’t accept it,” said the irked deputy minister, without going into details on actions she would take in response.

    Meanwhile, Mahiza has directed the headmasters through the Tanzania Heads of Secondary Schools Association to desist from discussing own interests in meetings and instead they should concentrate on discussing on ways to raise the quality of education in the region, which is apparently going down.

    According to last year’s Form Four results, a total of 4,723 candidates scored zero division in the region and those who ended up with the lowest division IV were 6,024. There was no Tanga school on the list of ten best schools in the country.

    Mahiza said teachers in the region should assess themselves basing on students’ performance in national examinations and give a conclusion whether they were committed to their work.

    She blamed some leaders in the education sector for putting at fore personal interests by collecting inflated fees, selling the joining instruction forms at high price and collecting contributions from parents, but in return fail to give the students quality education.

    “Some of you here are still collecting school fees and selling the joining instruction forms. I have evidence on that,” Mahiza said, warning the teachers to stop the illegal business, or else disciplinary measures would be instituted against them.

    ReplyDelete
  2. Mzee Ludewa ni wilaya sio kijijiiiiiiiii

    ReplyDelete
  3. Candid ScopeMarch 16, 2010

    Hapa sijakupata mwandishi wa habari. Kijiji cha Lunyanya au Manyanya?
    Kuna kijiji cha Lunyanya karibu na Ludewa wilayani Ludewa na kuna kijiji cha Manyanya karibu na Madunda katika tarafa ya Mawengi wilayani Ludewa. Jaribu kutoa ufafanuzi mwandishi wetu hapa

    ReplyDelete
  4. yote miyeyusho tu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...