Hivi kweli serikali imeshindwa kabisa kabisa hata kuwa na Domain jamani, kwanini email address za watu wa serikali ni za yahoo, hotmail au gmail??
Hivi elimu hawana ya kuwa kitengo kama cha serikali kutumia free address ni aibu hata kwetu sisi wenye ufahamu wa mtandao , tunaonekana ushauri wetu kwa serikali ni hakuna!!
Embu ankal fanya kila jambo tuwahimize wakubwa huko kufanya mara moja hili la email address. Iweje wawe na website ya taifa washindwe kuwa na email za .go.tz ?

Natumaini ankal michuzi utalituma hili kwa walengwa hata basi tulijadili na tulitekeleze, mimi ni mtu wa action zaidi kuliko hizi bla bla bla huwa siziwezi kabisa. Yaani inakera mpaka basi.
Mdau Barabara ya Ocean Rodi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 23 mpaka sasa

  1. TATIZO NI WATU KUDHARAU CHAO. WANAFIKIRI YAHOO NI BORA KULIKO .GO.TZ
    TUTAENDELEA KUWA HIVI KAMA HATUTAWEZA KUWA NA WATU WANAOWEZA KULETA MABADILIKO. WENGINE 'IT SKILLS' ZAO NDIO HIVYO TENA!!! KWA HIYO USISHANGAE!!!

    ReplyDelete
  2. Mdau hizo email address unazozungumzia ni za offcial au ni za binafsi? Maana nijuavyo mimi kila office ya serikali ambayo ina website tayari ina official domain ambayo huishia na .go.tz. Kwa mfano utaona wizara ya utumishi wanatumia estabs.go.tz,baraza la mitihani wanatumia necta.go.tz,wizara ya elimu wanatumia moe.go.tz etc. Kwahiyo domain zipo, unless niwe sijakuelewa hoja yako. Isipokuwa watumishi wengi wa serikali wanakawaida ya kuwa na email addresses zaidi ya moja kutokana na sababu totafuti. Address moja ni official (ambayo huwa hawapendi kuitumia kwa mambo ya binafsi) na address ya mambo ya binasfi (yahoo,hotmail, gmail, etc.) ambayo lengo lake nikuendelea kutumika hata nje ya ofisi husika. kwa bahati mbaya au nzuri hiyo ya private huwa inajulikana sana na hivyo kujikuta wanaitumia mpaka kwenye communication ambazo ni offcial

    Mdau wa Mbezi mwisho

    ReplyDelete
  3. Ndugu Mdau

    Ni kweli ni aibu kwa wafanyakazi wa Serikali au Taasisi za Serikali kutumia yahoo na wenzake kwa official communication.

    Ila mdogo wangu ukitumia hizo za kiserikali halafu server ikafa na wewe ndio umekwisha - taarifa zako zote zimekwenda.

    Ndio maana huwa wanatumia yahoo mails ijapokuwa nao siku hizi Wanigeria wamezikamata kweli kweli

    ReplyDelete
  4. KILIMO KWANZA BWANAAAAAAAAAAAAAAA

    ReplyDelete
  5. Kwanza kabisa naomba kutupa shutuma zangu kwa waziri wa Sayansi na teknologia, yeye ndio anatakiwa kwanza kuwa kioo sasa kama na yeye halioni hili kwa kweli hatufai na pia ni aibu kwa wakuu wengine wa nchi, eti rais ukitaka kutuma maoni unamtumia kny yahoo address, kwanini?? Tumeambiwa serikali ina website, na kwa ufahamu wangu kuwa ukiwa na website unaweza pia kupata a number of email accounts kny hiyo domain, sasa kwanini haijafanywa hivyo?? Hivi ankal michuzi na jamii nzima kwa ujumla hii ni uzembe wa serikali au hakuna wa kushauri hili jambo kwa umakini na sidhani kama lina gharama la kihivyo...IWEJJE taasisi kama BOT iwe na email address za taasisi yake kwanini isiwe kwa wizara husika tatizo ni nini hasa?? Hivi gharama ni kiasi gani kwani??nani anakazi ya kuupdate hiyo website ya serikali kwnaini asihimize hili??tusibaki kwenye ulaji tuu PROF amka sasa la sivyo wapishe watu wanaoweza angalau kuanza na hili na kulifutia taifa aibu ya kijinga kama hii...

    Nadiriki kusema wazi Tanzania iko kama sio step mija nyuma au mbili na technology ya ulimwengu huu wa sasa iweje hili hatulioni?? au ndio kila linalowezekana kutupwa tanzania basi linatupwa...

    RAIS, tunaomba uwe mkali nchi inaangamia hii, tuache siasa tufanye kazi jamani,,,,hivi mkisafiri nchi za wenzetu hamsikii uchungu jamani yaani hakuna la kujifuunza huko na kuweza kulifanya hapa kwetu, kwa mfano mimi nauchungu sana bwana RAIS kama huwa unasoamaga hii blog au wanaoweza kumpelekea ujumbe huu,,
    Inakuwaje tuwe na wilaya 3 na zote zina hospitali za wilaya iweje kila jambo linapelekwa muhimbili tuu kwanini muhimbili isibaki refferal hospital tuu, mgonjwa asiwe anajiendea tuu muhimbia mpaka apate reference kutoka district hosp. kwa kujua kweli tatizo la mgonjwa limeshindikana kweli then muhimbili wanashughulikia, ingewapa nafasi hata hizi District hosp kufanya kazi zao kwa umakini na ushindani zaidi. nnayo mengi ila tuanze na hili la emails then tuje na hili la muhimbili,,,,,,, Tumuinge KAGAME kama hatuwezi kuonga nchi za ulaya na USA.

    ReplyDelete
  6. Kwa Mdau aliyeleta Mada,

    Wewe mwenye ufahamu umeamua kukaa Ulaya kupiga Box. Sasa huoni kama ni ulimbukeni kuwalalamikia Wakulima waliopo Tanzania kuwa hawajui IT.!!

    Nenda kawafundishe.

    ReplyDelete
  7. mdau wa mbezi mwisho,, kama ni official iweje kny business card za official zisomeke za yahoo na hotmail au gmail???
    hawako serious??

    ReplyDelete
  8. Tunazisikia hizo ziara za nje kila kukicha. Na wanaona mengi ya maendeleo huko wanakotembela. Nadhali wanaishia kushangaa tu!!

    Nimeshasikia misafara mingi ikiambata na wajumbe mbalimbali, lakini hadi leo sijabahatika hata kusikia (sembuse kuona) kuwa hili mnalosikia/ona ni kutokana na jumbe tuliokwenda Marekani, Denmark, nk. Wanaishia shopping tu hao.

    Yaani yote wanayoyaona huko hakuna hata moja la kufanyia mazoezi tukavuka kutokata hatua moja hadi nyingine jamani?!!!

    Eeh, haya bwanaaaaaa. Kilimo kwanzaaaa bwanaaaaa!!1

    ReplyDelete
  9. Mimi nadhani mtoa hoja na asilimia kubwa ya wanaonchangia hii mada hawajui wanaloliongea, mngekuwa mnafanya uchunguzi au kuuliza wenzenu kwanza kabla ya kutoa comments, kila wizara ina domain yake, na wanatumia official emails. Sasa kama nyinyi mkipewa email za watu,ni kuwatumia emails za kuwa piga mizinga na kuwatapeli, unadhani waataacha kuwapa email zao personal? Hawawezi kuwapa official emails zao, then muwe mnawatumia upuuzi.

    Nawewe mdau uliyezungumzia swala la muhimbili, hivi mpaka leo ulikuwa hujui kama muhimbili ni referal hosp, rudi shule.

    Jamani watanzania wenzangu nadhani wakati umefika wa kukaa na kuacha kulaumu serikali wakati wote, hata kwa mambo ya kipuuzi, tuwe tunaangalia mambo ya msingi.

    ReplyDelete
  10. tue mar 23 02:00:00pm

    Nilitegemea unajua kusoma , kumbe unajua kuandika tuu..
    Soma vizuri na uelewe ndio uweze kucomment sio unajijia na njaa zako unacomment.

    mdau alisema anasikitika kuona wilaya zote 3 zina hosp, kwanini kila jambo linapelekwa muhimbili tuu, alitegemea kuona muhimbili kuwa ni really refferal hosp, mgonjwa kwenda muhimbili uwe kweli umepewa reference kwenda huko from either temeke,amana,mwananyamala hosp ili kuziwezesha hata hizo hosp za wilaya kufanya kazi kwa umakini na endapo inashindikana ndio aende muhimbili.. ifikirie hiyo kwa mapana ndio utaelewa , na huo ni mfano mdogo , wale wa mikoani wakipewa reference waende wapi AMANA, au TEMEKe acha sisa chafu wewe jifunze kusoma na kutafakari ndio uelewe mambo.

    Na kuhusu yahoo mails kabla ya mdau kuweka hilo amefanya uchunguzi wa kina mpka mabalozi wetu nchi za nje wanatumia yahoo huoni kama ni ulimbukeni huo,,, sio swala la kuomba pesa , kama ungekuwa hivyo si asingetoa business card ya kazini kwake yenye address hizo za yahoo na logo ya TAIFA..

    TAFAKARIIIIIII kama haupo nchi usikukuruke na kuandika unakaona watu wanasoma na kufurahia unachoandika...
    seriousness inahitajika kwenye maswala ya kimsingi.....

    ReplyDelete
  11. UZEMBE WA MAMLAKA ZA JIJI LA LUKUVI.
    NI AIBU NA KERO PAMOJA NA HASARA KWA UJUMLA YA WAHUSIKA WA JIJI KUTOKUSHUGHULIKIA KERO YA FOLENI YA JIJI HILI LA DAR.

    FOLENI HIZI HULETA KATIKA UCHUMI NA MAISHA KWA UJULWA NEGATIVE MULTIPLE EFFECTS ZIFUATAZO:

    MOJA:
    WATU KUCHELWA KUFIKA MAKAZINI MA MAJUMBANI; HIVYO KUPOTEZA NGUVU KAZI KWA KIASI KIKUBWA; KWANI MUDA MWINGI HUUPOTEZA KWENYE FOLENI, NA PIA KUWAKOSESHA NA KUPATA HUDUMA MBALIMBALI; KWANI WATOA HUDUMA HIZO WANAKUWA KWENYE FOLENI

    PILI:
    WATU WAFIKAPO MAJUMBANI HUWA WAMECHOKA HIVYO KUTOWAJIBIKA IPASAVYO KWENYE OTHER SOCIAL ACTIVITIES.

    TATU:
    MATUMIZI YA MAFUTA HUONGEZEKA; HIVYO KULAZIMISHA UNNECESSARY IMPORTATION YA MAFUTA; HII HUSABABISHA DEMAND YA FOREX KUONGEZEKA NA AMTOKEO YAKE ADHARI INAKUJA KUFANYA EXCHANGE RATE KUPATA; KWANI SISI HATU-EXPORT SANA HIVYO FOREX CHACHE ZILIZOPO ZINZFUKUZIWA NA HELA NYING ZA MADAFU.

    NNE:
    KWA SABABU ZA HAPO JUU; KUNAKUWA NA INLFATION ISIYOKUWA YA LAZIMA.

    KWA KUTOKUWA MAKINI NA SWALA LA FOLENI TU TUNAJIKUTA TUNANUNUA MAISHA MAGUMU BILA YA KUPENDA.

    SIYO KILA PAHALI TUNAHITAJI RASILIMALI HELA NYINGI ILI KUTATUA MATATIZO YETU KAMA YA BARABARA; WAKATI MWINGINE UBUNIFU NA UFUATILIAJI WA MAMBO UNAWEZA KUTUONDOLEA KWA KIASI KIKUBWA MATATIZO YANAYOTUZUNGUKA.

    MFANO PALE BP KUELEKEA KILWA ROAD; HUWA KUNA FOLENI KUBWA ISIYO YA LAZIMA; KWANI KAMA SEHEMU INAPOKATIZA RELI IKIREKEBISHWA NA KUFANYA MAGARI YAPITE KWA SPEED BILA YA KUKWEPA MASHIMO YALIOPO; BARABARA ILE INGELETA UNAFU KWA KIASI KIKUBWA; NA GHARAMA YA KUREKEBISHA ENEO LILE NI DHAHIRI NI NDOGO SANA IKILINGANISHA NA USUMBUFU UNAOWAPATA WATUMIAJI WA NJIA ILE.

    SERIKALI YETU IJARIBU KUBINAFSISHA BAADHI YA MAENEO AMBAYO WAMESHINDWA KU-DELIVER LIKIWEMO HILI LA MANAGMENT YA MABARABARA; ILI WANANJI WAONE MAANA YA KODI WANAZOTOZWA AMBAZO NAZO HAZINA SURA NZURI KABISAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAA

    ReplyDelete
  12. Mtoa mada,asante kwa kuliona hili..jambo la msingi sana..bado wabongo hatujazingatia mambo mengi muhimu yahusianayo na ICT.. kwa mfano, utashangaa hata vyombo muhimu kama TBC na technolojia zao zote hawana website..kuna mdau mmoja amekupinga hapo juu..nadhani na yeye hajui umuhimu wa ulichoongelea, tegemea wengi wa aina hiyo..anabadili mada..tubadilike jamani

    ReplyDelete
  13. Jiji letu la Dar es salaam halina website!!!. Jamani professionals wa web design tafadhalini jitoleeni kututengenezea website for our beautiful city! VOLUNTEER PLEASE.

    ReplyDelete
  14. Mdau Tue Mar 23,03:28:00PM,Asante kwa uchambuzi wako unaona mbali kwa kweli lile suala la kufikiria MUDA kuwa MALI kwa sasa halipo nadhani Michuzi ataichukua hii kama changamoto na kuiweka kwenye blogu kama mada inayojitegemea,ila pia we ni funid sana wa SWANGLISH ni vyema lakini nadhani ukipata wasaa wa kuyaweka misamiati hiyo kwa kiswahili fasha ITANOGEZA ZAIDI Asante
    MZAZI.

    ReplyDelete
  15. Jamani hivi wabongo wote mliosoma IT huku majuu mko wapi. Wazungu wenzetu wanafanya volunteer jobs tena Afrika! Sasa sisi kwa nini tupo selfish kiasi hicho. Yaani IT specialist wa ki-bongo akitua bongo kwa vacation yake na kwenda kushusha darasa kwa waziri mkuu au waziri wa miundo mbinu au sijui science na teknolojia kuwa anaweza kusaidia katika IT setting ya serikali sidhani kama mtu atakataa. MAANA INABIDI WOTE TUJITAHIDI KUIJENGA NCHI YETU NA KUPELEKA HABARI NZURI ZA MAENDELEO TULIZOBAHATIKA KUZIONA NCHI ZILIZOENDELEA!

    ReplyDelete
  16. HIYO NDIO BONGO BWANA . WANASEMA TAMBARARE. KWA IDAI YA WATU WALIO NA DEGREE , MASTERS, PHD NA KAZALIKA BASI BONGO ILITAKIWA IWE NA MOTOR WAY KIBAO NA MATECKNOLOGY KIBAO.BUT NI MAJOHO TU NA KARATASI NO REALITY. INGEKUWA VIZURI WATUMIE WATU WENYE EXPERIENCE KUAJIRI NA SIO KUAMINI SANA MADEGREEE JAPO NI MUHIMU NAYO NCHI HAIJENGWI KWA MAKARATASI TU BALI NI UFANYAJI BORA WA KAZI.

    ReplyDelete
  17. @ Mar 23, 09:45:00 AM, wengi huku tuna degree za IT na tulitaka sana turudi kutumikia taifa japo taifa halikutusaidia wakati tunasaka maisha

    Kilichonikwamisha kurudi home baada ya kuona hizi kazi zikitangaza kuwa zinatafuta mtu ...Umri usizidi miaka 30. Mimi ninilivyoona hivyo nilijua nitaenda kuaibika home bure...Nikatafuta mshiko huku huku mungu si mchoyo. Huku hawajali umri wanajali nini unajua. Ninamiaka 31 naona huko mimi sihitajiki tena.

    ReplyDelete
  18. tatizo mitandao yetu nyumbani ipo slow sana..........utachukua dakika 15 ku-load page na ikiwa na attachment ndio inagoma kabisa kufunguka. kwanini wasitumie yahoo kwa fasta fasta!

    ReplyDelete
  19. Aibuuu! hata Dr Manyuki anawashinda kwa email yake Emai....:manyuki@drmanyuki.com

    ReplyDelete
  20. Ni wakati muafaka kwa hoja hii kwani kituo husika cha kusajili majina ya vijoa au domain names kiitwacho tzNIC sasa hivi kinaendesha promotion kwa kushirikiana na Clouds FM kuhamasisha watanzania kusajili majina hayo. Mchango wake ni mkubwa kwani mbali na kupata utambulisho unaoendana na sifa za nchi yetu pia utachangia kupunguza gharama za mawasiliano (internet traffic localization). Watanzania tuchangamkie.
    Kuhusu viongozi kutumia yahoo, gmail nk basi wawe makini kutenganisha mawasiliano ya kikazi na kibinafsi na kuhusu biz cards zao si vibaya wakiwa na za aina mbili.

    ReplyDelete
  21. Hakika hii ni hoja ya haja laki Upande wa pili wa shilingi je? - SMEs/viwanda na kampuni ndogo ndogo na asasi nyingine zisizo za kiserikali, mashule, nk pia tusajili majina haya tusijeshtuka na kukuta hata majina yetu asili yameshachukuliwa na wageni. Sajili jina la biashara yako ili huduma zako zionekane ulimwenguni na si Tanzania tu!!! Mtaarifu na mwenzako.

    ReplyDelete
  22. ACHA KELELE WEWE PIGA BOKSI DEKI NYUMBA ZOA TAKA, MAMBO YA TZ YAACHE TZ KAMA ULIVYOIACHA NA KWENDA KUPIGA BOX NA UKIRUDI UTAKUTA HIVYO HOVYO AFRICA HATUNA HARAKA WEWE

    ReplyDelete
  23. @WEWE MDAU WA WES MARCH 24 10;55 AM. ACHA USHAMBA , ET AFRICA HATUNA HARAKA . FUMBUKA MACHO, ENDELEA ACHA KUTHINK SMALL THING LARGE. U WISH UNGEPATA VISA UPIGE BOX NAWEWE. NYOOO NA VISHILINGI VYAKO. BOX THEN UNALIPWA IN £££ AU $$$$$. SIO BOX THEN SHILLINGI. AU KUWA MATAPELI NA KUIBIA MASIKINI. RUSHWAAAAAAAA.NA KUSABABISHA VIFO VISIVO NA MSINGI. BE CIVILIZED. SILLY COW.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...