Naibu Balozi wetu UK Mh. Chabaka Kilumanga akimkabidhi tunzo Bw. Baraka Msiilwa kwa kutambua mvchango wake katika burudani kupitia African Stars Entertainment wamiliki wa Twanga Pepeta ambapo yeye ndiye mwanzilishi na Mwenyekiti Mtendaji wake. Hafla ilifanyika mara baada ya Diaspora 2 jijini London na iliandaliwa na New Deal Africa

Mh. Kilumanga akimkabidhi tunzo Bw. Mohamed Dewji kwa kutambua mchango wake katika jamii. Bw. Dewji ni msafirisha bidhaa mashuhuri UK
ankal akipokea tunzo yake kwa kutambua mchango wa libeneke la Globu ya Jamii

ankal akipozi na Sporah Njau ambaye naye alipokea
tunzo kwa juhudi zake katika kipindi cha Sporah Show
Mengi kuhusu New Deal Africa

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. watoa tuzo mmekosa shukuran, kuna taasisi nyingi zinatoa mchango mmeziacha.

    badala yake mnawapa watu tuzo ambao bila kudharau mchango wao, wamekuwa machoni na masikioni kwa muda usiozidi mwaka mmoja.

    anyway, hatujui vigezo mlivyotumia. sioni kwanini apewe Sporah aliyekuja juzi, wakati kuna old school mmekuwa mkiwatumikisha miaka nenda.

    ReplyDelete
  2. Kweli kabisa nakubaliana na mtoa maoni hapo juu. Haya mambo ya kujikomba na kibongo bongo mmmmmmmmmmmm kazi kweli kweli

    ReplyDelete
  3. Huyo Mr Baraka Msilwa kwa kweli anastahili tuzo kama hizo , manake mbali na kuwa Accountant by proffessional kwa muda mrefu ameweza kutumia muda wake mwingi pia katika kukuza sanaa ya burudani tokea enzi za Bendi za M.K GROUP ikiwa pale Bandari Grill, New Afica Hotel wakijulikana kama ngoma za magorofani, M.K Beats wana Tukunyema, M.K Sounds ya kina NYOSHI ELSADAT wa FM Academia, ELLYSTONE ANGAI,King Dodoo na kisha kuanzisha hiyo African Stars Band"Twangapepeta" inayotamba mpaka sasa. Tumemsikia siku nyingi na mpaka leo bado yupo katika game

    ReplyDelete
  4. Jamani wivu acheni, Mbona hii Sporah Show ipo kwa miaka kadhaa.
    Ndugu zangu jaribuni kuapreciate.
    WELL DONE SPORAH, YOU DID IT.

    ReplyDelete
  5. HONGERA MZEE WA ANKARA, NA PIA HONGERA SANA DADA SPORAH HASA KUPATA AWARD AT YOUNG AGE.. MAMA KWA JUHUDI ZAKO UTAZIKUSANYA AWARD NYINGI SAANA, KEEP IT UP.
    IVI JAMANI NANI KAWADANGANYA KUPATA AWARD NI LAZIMA USOTE KWA MIAKA 10?
    EBU ACHENI UJINGA NA MJARIBU KUWASAPORT WATANZANIA WENZETU
    ACHENI ROHO ZA KOROSHO HUYU DADA ANATUWAKILISHA, NAINABIDI TUKUBALI MAANA HUO NDIO UKWELI WENYEWE.
    HONGERA SANA DADA SPORAH, TUNAKUTAKIA KILA LA KHERI NA UZIDI KUWINI MORE AWARD.

    ReplyDelete
  6. Wivuuuuuuuuuuu
    hongereni jamani

    ReplyDelete
  7. Jamani kwa kweli huyo Baraka Msiilwa ambaye hii juzi juzi tumemuona akishiriki kikamilifu kwenye Diaspora 2 mjini London ni kiunganishi kizuri kati ya sisi Wa DIASPORA na huko nyumbani Bongo. Mchango wake,na muenekano wake kwenye community ya Wa Diaspora unafaa kuenziwa na kuigwa na sisi wengine. Above all, Akiwa anaishi na kusoma UK wakati wake hakusahau Ku invest nyumbani.

    ReplyDelete
  8. ni TUNZO au TUZO?naomba msaada.

    ReplyDelete
  9. Well done Sporah, We love you girl.
    KEEP IT UP.

    ReplyDelete
  10. hongereni wote mliopata tuzo. Ni tuzo Mchuzi siyo TUNZO

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...