Picha na Habari
na Dixon Busagaga
wa Globu ya Jamii, Moshi.
KAMPUNI ya Bonite ya mjini Moshi inayojishughulisha na utengenezaji wa vinywaji baridi jamii ya Coca Cola leo imezindua promosheni maalum itakayojulikana kama ''Kwea Pipa na Ushinde''
Promosheni hiyo itawezesha watanzania 200 kushuhudia fainali za Kombe la Dunia zitakazofanyika Afrika Kusini hapo mwezi juni mwaka huu .
Washindi watakaopatikana kutokana na bahati nasibu hiyo, watashuhudia mechi ya Brazil na Ureno mchezo utakaochezwa Juni 26 katika mji wa Durban , Afrika Kusini.
Akizindua promosheni hiyo, kwa kufunga penalti katika hafla fupi iliyofanyika kwenye kiwanda hicho mjini Moshi mkuu wa wilaya ya Moshi Musa Samizi alisema hatua hiyo itasaidia kuendeleza soka Tanzania .
Alisema kuanzishwa kwa promosheni hiyo kutaisaidia nchi kw akuwa watakaoenda kwenye fainali hizo watasaidia kupeperusha bendera ya Tanzania hasa katika sekta ya Utalii ambapo itaiweka nchi katika ramani nzuri ya dunia.
Washindi hao watakaokwenda Afrika Kusini, watagharamiwa kila kitu tiketi ya kwenda na kurudi, chakula, malazi pamoja na usafiri wa ndani

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...