
Wanamichezo 40 kutoka Ikulu ya Zanzibar, leo, Ijumaa, Aprili 2, 2010, wametembelea Ikulu ya Dar es Salaam ambako wamekutana na kupiga picha ya pamoja na Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Wanamichezo hao wako Dar es Salaam kushiriki katika michezo ya Pasaka kati yao ya wanamichezo wa Ikulu ya Dar es Salaam, iliyopangwa kufanyika kesho, Jumamosi, Aprili 3, 2010, kwenye Viwanja vya Chuo Kikuu Kishiriki cha DUCE, Chang’ombe.
Timu za Ikulu hizo mbili zitachuana katika michezo ya soka, netiboli, kuvuta kamba, na kukimbia ndani ya magunia.
Akiwakaribisha Ikulu ya Dar Es Salaam, Mkurugenzi wa Huduma za Ikulu, Bwana Frank Mganga ameielezea ziara ya wanamichezo hao kama ziara ya kihistoria.
“Haijahi kutokea tokea tangu mwaka 1964 wakati Tanganyika na Zanzibar zilipoungana ikaandaliwa ziara kama hii,” Bwana Mganga amewaambia wanamichezo hao ambao wamelikwa Dar Es Salaam na wenzao wa Ikulu ya Dar es Salaam.
Amesema kuwa ziara hiyo imelenga kukuza na kuimarisha uhusiano kati ya Ikulu hizo mbili na pia kuimarisha Muungano wa Tanzania.
“Ni kwa kutambua umuhimu wa ziara hiyo, ndiyo maana Rais wa Zanzibar, Mheshimiwa Amani Abeid Karume, ametoa ndege kuweza kuwaleteeni nyinyi hapa Dar es Salaam,” amesema Mganga.
Wanamichezo hao wamewasili Dar Es Salaam katika makundi mawili. Kundi la kwanza lililetwa jana kwa ndege maalum iliyokodishwa na Rais Karume, na kundi la pili limewasili leo asubuhi kwa meli.
Mmm Mbona hizo sura karibu zote ni ngeni machoni mwetu ?
ReplyDeleteMiraji Taufiki
....michu namimi nataka nikutane na JK afu usinibanie foto yangu kwenye blogu ya jamii... si unajua na mimi nataka kugombania jimbo la naniihiii....
ReplyDelete