Daktari wa kituo cha Afya cha Dk. Hameer kilichoko maeneo ya Faya jijini Dar, Dk. Sombi Charles akimpatia matibabu ya awali Mwenyekiti wa Chama Cha Jamii (CCJ), Mh. Richard Kiyabo baada ya kuugua ghafla na kukimbizwa katika kituo hicho kutokana na maumivu ya shingo pamoja na kifua kubana jioni hii. Mwenyekiti wa Chama Cha Jamii (CCJ), Mh. Richard Kiyabo
akijieleza kwa ripota wa Globu ya Jamii
Mwenyekiti wa Chama Cha Jamii (CCJ), Mh. Richard Kiyabo
akihudumiwa hospitali hapo

Picha na Habari
na Francis Dande
wa Globu ya Jamii
HALI ya afya ya Mwenyekiti wa Chama cha Jamii (CCJ), Mh. Richard Kiyabo imebadilika ghafla na kukimbizwa katika kituo cha Afya cha Dk. Hameer kilichopo maeneo ya Faya jijini Dar leo.

Akizungumzika hali yake huku akiwa kitandani Mwenyekiti huyo alisema kuwa afya yake ilianza kudhohofika leo na kukimbizwa katika kituo hicho majira ya saa tisa alasiri kutokana na kupata maumivu makali ya shingo pamoja na kifua kubana.

Aidha alisema kuwa hali hiyo inatokana na kuvamiwa na watu wanne majira ya saa tatu asubuhi na kisha kumkaba shingo na kumpora mkoba wake uliokuwa na kiasi cha sh. laki tano, Laptop pamoja na reja iliyokuwa na orodha ya majina ya wanachama wa chama hicho kwa upande wa Zanzibar.

Alisema kuwa kabla ya tukio la uporaji halijafanyika watu hao walimtisha na kisha kumtolea vitambulisho vilivyokuwa vikionyesha kuwa ni wafanyakazi wa Idara ya Usalama wa taifa. “Niliwaaambia kuwa kama nina makosa wanipeleka katika vyombo vya sheria lakini walizidi kunikaba”.

Mwenyekiti huyo amesema kuwa tukio hilo analihusisha na hujuma za kisiasa kutokana na mazingira yake na kuliomba jeshi la polisi kulinda raia wake na kufanya uchunguzi wa kina kujua waliohusika na tukio hilo ili sheria ifuate mkondo wake.

Katika hali isiyokuwa ya kawaida Mwenyekiti huyo alisema kuwa: "Hata kama nikifa leo watanzania wasimtafute katika makaburi yaliyopakwa rangi nzuri ila wamtafute kwenye mioyo ya watanzania wanyonge milioni 40 walio mijini na vijijini, hali si nzuri sina hela hata mchana sijala,” alisema Mwenyekiti huyo na kuongeza kuwa watanzania wamchangie katika gharama za matibabu ambazo ni kubwa.

Daktari wa zamu Dk. Sombi Charles aliyekuwa akisaidiana na Dk. Nassor alisema kuwa katika kumfanyia uchunguzi wao walibaini kuwepo kwa matatizo katika shingo na kifua kutokana na kupata mgandamizo wa kitu chenye ncha butu kwenye shingo na kumsababishia matitizo katika mishipa ya fahamu.

“Hivi sasa tumempatia matibabu ya awali ili kupunguza maumivu aliyokuwa nayo wakati tukimsubiri mtaalamu wa mishipa ya fahamu (aliyemtaja kwa jina moja la Dk. Othman) afike ili kumfanyia uchunguzi wa kina ili kutoa tiba sahihi kwa mgonjwa.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 17 mpaka sasa

  1. kyeleuuuhwiii! ati "BRANCHIOLNEVER" ni nini hicho?kilatini? ni daktari huyo kweli au is this a belated april fools prank. Jamani jamiiforums iko wapi? tunakosa uhondo ati!!! Be back soon

    ReplyDelete
  2. Usanii mtupu. Nawapongeza CCJ kwa kupata PR officer anayejua kazi yake, na mwenyekiti alifuzu mafunzo ya sanaa.

    ReplyDelete
  3. umaarufu unatafutwa kwa njia nyingi pamoja na ulaji pia.Mw/kiti anatembeaje na pesa za chama? Hakuna M/hazina?

    Kama ni zake bank ni za nini?

    usanii bongo no. 1.

    ReplyDelete
  4. duuu, yawezakuwa ni kamera ya mionzi (Colimber Series MD1 24mHz) imetumika na wapiga picha wa sisieem. woooch auuut!

    ReplyDelete
  5. Wobongo tumelewa u-ccm hata ifanye umafia kiasi gani tunaendelea kuiona ndio mkombozi. ukishangaa wanakushangaa kwa nini unashangaa. watu wanataka kuongeza sauti mbadala sisi tunawaona ni maadui badala ya kuwapatia moyo wa kuendelea kupaza sauti. tumeganda

    ReplyDelete
  6. Anon wa Sat Apr 03, 08:59:00 PM

    Kula tano. But usihofu ukiona CCM wanafanya umafia ujue maji yaanza kufika shingoni sooner or later they'll be out of power vinginevyo waiingize nchi pasipo stahili kwa king'ang'anizi chao. Ukweli ni kuwa uongozi wa nchi kwa sisi wabongo ni opportunity pekee ya kutokea, usijekuta na hao CCJ wakishika nchi yatakuwa yaleyale ya kung'ang'ania ndiyo maana CCM wanaogopa kuwekwa kwe minority status.

    Ila kwa maendeleo ya nchi tunahitaji CATALYST za kuwafanya wavivu walio kwenye madaraka angalau kukukuruka waonekana wanafanya kitu vinginevyo watalala suingizi wa PONO.

    ReplyDelete
  7. yamekua haya tena?
    yani kuna maharamia hii nchi!!
    ila iko soku yenu i tell you

    mungu akutie nguvu sana mpendwa mwenyekiti

    ReplyDelete
  8. Watanzania ni rahisi kweli kudanganyika. Hivi hao CCJ si litakuwa tawi tu la CCM? Si hao walikuwa huko CCM na wakiunga mkono sera zote za kifisadi na kufaidika nazo miaka nenda rudi? Leo hii tunategemea waje watukomboe, inawezekana vipi na wao hawajatubu wala kuomba msamaha kwa dhuluma walizotufanyia? Bado wanatafuta umaarufu kupitia ujinga wetu na sanaa za maonyesho za wazi?!!

    ReplyDelete
  9. Mdau, Bloomsbury, LondonApril 04, 2010

    Kama kweli shingo imemuuma na kifua kimembana huyo 'daktari' ametoka wapi kusema ni brachial nerve? Na hiyo brachial nerve inapatikana wapi? Ha ha! Watu wengine bwana, wanadhani waTZ wote wa kudanganywa. Hamna nerve kama hiyo, na kama ulimaanisha brachial plexus, ungekuta anamaumivu au kukosa hisia kwenye mkono, si kubanwa pumzi. Nashauri yeyote aliye karibu na huyu mwenyeketi amshauri aende Muhimbili, hususan MOI inawezekana amebana mishipa inayoenda kwenye msuli mkuu wa kupumulia, yaani diaphragm, kwenye vyanzo vyake shingoni.

    Maelezo marefu lakini nadhani ujumbe umefika.

    ReplyDelete
  10. Mimi sio Dr lakini hizo kama dalili za heart attack...Mtu mwenyewe mwembamba...lakini ni huku kula mavyakula yenye kuengeza cholestrial sana....

    ....wachekigi afya zao jamani tusije tukawapoteza...tunahitaji sauti nyingi TZ sana

    ReplyDelete
  11. NautiakasiApril 04, 2010

    We mdau, Bloomsbury ndo mwenye matatizo..unajifanya "much-know" kumbe hujui kitu. Sasa brachial plexus nini? Naona unazunguka tu lakini kitu ni hicho hicho. Tatizo wewe umekariri. Basi kwa kukusaidia tu daktar yuko sahihi, alichokifanya ni mention tatizo lilipo moja kwa moja bila ya kutumia terminology zisizo lazima. Sababu ukisema branchial plexus ni mpangalio wa nevers fibre katika brachia which means ni "brachial nerves" Nenda kasome uelewe, sio kukariri!

    ReplyDelete
  12. ....na kwa bahati tu wapiga picha walikuwepo hapo hospitali wakati akifikishwa kwa matibabu, hii sio publicity hat akidogo, yeah wright.

    na toka lini daktari akaruhusu wapiga picha wakati akimkagua mgonjwa? iko wapi privacy? jawabu ni paragraph yangu ya mwanzo.

    ReplyDelete
  13. mnaobishana juu ya utaalamu wa daktari, naomba niwasaidie ni hospitali ndogo hiyo lakini they are very smart kwa huduma zao, mtu yeyote ambae ameshawahi kupata huduma hapo atakubali. Really, they have good doctors, facilities and their hospitality is wonderful! Jamaa asiwe na wasiwasi afya itatengemaa, labda kuwe na mkono wa mtu.

    ReplyDelete
  14. Bi Reaka RafikApril 04, 2010

    Hii ni karne ya 21.
    Hapa ndio mtagundua kuwa uelewa wa watu umekuwa mkubwa sana.

    Hii haina tofauti na lile puto feki (balloon hoax) kwa ajili ya 'reality show'


    Michuzi hii haiminywi. Ambaye haelewi aniulize nimfafanulie.

    ReplyDelete
  15. Afadhali umemsahisha ndugu yangu. Jamani tangu darasa tano tutasoma "Brachial Nerve" sasa leo hii mtu anaibuka from no where to somewhere nakuongea upupwe.Ati anajifanya mtu wa Muhimbili, Muhimbili kitu gani, ondoka huko uende kutibia Chekeni Mwasonga ndiyo size yako.Kuna kasimba mbaya sana hapa Bongo kuwa mgonjwa ambaye hajatibiwa Muhimbili amekuwa Mis-managed, hii kitu mbaya sana.Kwani umuhimu wa Ankal kuanzisha Medical debate humu ndani ili watu waweze kuelewa japo Basic Medical Knowledge tu.

    Ni hayo tu wapendwa.

    ReplyDelete
  16. Kwa kumsaidia tu huyo mjuaji wetu ni kuwa plexus maana yake ni network, hii ndiyo maana halisi ya neno plexus.Huyo Dr amekuwa specific kwenye mahelezo yake ili kila mtu aweze kuelewa hata kama sio medical personel.

    ReplyDelete
  17. mr,michuzi.najua wewe unafanya kazi serkali.napenda kusema,usiwe unabania maoni ya watu mbalimbali.maana siku ya hukumu nawewe utahesabiwa kama unahatia na mijdhambi inayofanya na serkali na pia wahisani wako CCM.
    nachokuomba ni hiv;hichi chombo ni chako ni mali yako lakni ujue kwamba hiki chombo ni sauti ya uma.ni kuambie tu,watu wengi wanasoma comment hapa.na ninachoweza kusema,kuna ukweli mwigni unaoongelewa happa.katika blog yako
    hivyo,basi blog yako isiwe ni kwajiili ya kukumbatia upande moja wa shilingi na kusahau wapi umetoka.
    nasema hivi kutokana na kwamba nimeona mara nyingi umekuwa ukiania comments za msingi na ambazo moja wetu hata mkubwa akisoma.mambo yatabadilika kuona kwamba kuna sauti na sauti ni watu.
    kuhusu huyu jamaa naamini ni watu wa serkanili ndo wanaotaka kuingilia huu mchakato mnzima,
    ni nani alisema kuna democracia hapa bongo?
    anyways,nathani umeelewa somo!
    usinglie uwazi na fursa ya watu wako katika hii blog kutoa maoni yao.
    ni mimi

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...