Wadau kunradhi. Leo tumemzika nyanya yetu mpenzi kwenye makaburi ya Nonde, nje kidogo ya jiji la Mbeya. Zifuatazo ni taswira za mazishi hayo (ni nyingi kiasi kwa sababu maalumu) ya nyanya yetu aliyefariki siku nne zilizopoita akiwa na umri wa miaka 92. Ni siku ngumu kwangu ankal binafsi na wanafamilia. Najua wengi wadau mnajiuliza niaje? Huyu nyanya wetu kipenzi ni dada wa nyanya yangu mzaa mama ambaye ni mzawa wa huku Mbeya. Yeye alikuwa Mkatoliki swafi wakati nyanya yangu alikuwa Muislamu kama alivyoturithisha siye wajukuu zake. Huyu nyanya aliolewa na babu mwenye asili ya Ushelisheli.
Nyanya yetu kipenzi akiwa hataki kukaa sawa kwenye taswira hii
Ibada katika Kanisa la Mtakatifu Antoni wa Padua jijini Mbeya
Ma-ankal na wakwe zetu kina Isaak na Edwin Kassanga
Ankal Tony Swai akisoma somo la kwanza
sehemu ya waombolezaji wakiwa kanisani
wakati wa ibada
ndugu, jamaa na marafiki ibadani
ndugu na jamaa
madada
ankal na dada wa ankal
mbele shati jeupe ni mwakilishi wa Vodacom kanda ya kusini
Dada Helena akihakikisha kila kitu kinaenda sawa. Nyanya yetu kipenzi tumemzika ndani ya kaburi la mumewe aliyefariki miaka 25 ilopita kwa matakwa yake marehemu
mwili wa nyanya yetu kipenzi ukishushwa kaburini
mazishini anaanza dada helena kuweka udongo
dada Victoria aishiye Ndola, Zambia, na mumewe wafuatia
ankal moses anayeishi Stockholm, Sweden, afuatia
ankal Francis wa Tanga anafuatia
ni zamu ya ankal Tony
ni zamu ya Da' Eliza
Isaack kassanga ambaye ni mkwe aweka udongo kaburini Padri anayetuongoza akibariki msalaba
kitukuu kaburini
Padri anayetuongoza akiweka shada
Da'Viki na mumewe
ni zamu ya ankal na Ndonya, dadaye
kaka Ismail
ankal Tony
Da'Eliza
Mwenyekiti wa mtaa
ndugu, jamaa na marafiki
Dua baada ya mazishi






































Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 25 mpaka sasa

  1. Poleni na msiba. Mungu amuweke panapostahili

    ReplyDelete
  2. Bwana alitowa na bwana ametwaa.....Poleni sana. Anyway, naona Anko mnafanana sana mko kama Wabrazil/Wakorea mnafanana kama vidole.Poleni sana.

    ReplyDelete
  3. TvzkicartoonApril 11, 2010

    Poleni sana Ankal na wana familia Mwenyeezi Mungu atawapa subira InshaAllah, na amweke Marehemu mahala pema Amin.
    Ilobaki Mumwombee nyanya apumzike kwa amani na mumshukuru Mwenyeezi Mungu mmekuwa na nyanya yenu mpaka vitukuu wamemwona ni jambo la kushukuru sana!

    ReplyDelete
  4. Kaka Michuzi poleni kwa msiba huu mzito. Menyezi Mungu awape Nguvu kwa kipindi hiki kigumu awatie moyo faraja na amani. Sisi wote ni wasafiri hapa duniani na heri ya Bibi Yetu ameishi katika kumpendeza Mwenyezi Mungu maana amepitiliza hata ile miaka iliyoandikwa kwenye Biblia miaka SABINI na yeye kagonga tisini na mbili.Hakuna sababu ya kulia tunachotakiwa kufanya ni kusherehekea Maisha ya Bibi wakati wa uhai wake naamini katuachia mambo mengi mema na mazuri yatakayo tuongoza sisi wajukuu kwa muda mrefu ujao. ASANTE

    ReplyDelete
  5. Ankal,

    Poleni sana kwa kuondokewa na Nyanya. Ametimiza wajibu wake hapa duniani, na Mungu amemrejesha kwenye makao ya milele. Tunashukuru kwamba Mungu amewawezesha kusafiri salama hadi kuwahi mazishi. Mimi ni Mkatoliki; nimeguswa sana na ibada ya mazishi ulivyoionesha hapa, ikijumlisha watu wa dini mbali mbali. Mungu awafariji kutokana na msiba huu, na ampokee Nyanya katika pumziko la milele. Amina.

    ReplyDelete
  6. pole ankal kwa kuondokewa na nyanya yenu kipenzi, Mungu ampumzishe kwa amani, amen

    ReplyDelete
  7. POLENI SANA ANKALI NA FAMILIA YAKO YOTE SIS TULIMPENDA LAKINI MUNGU ALIMPENDA ZAIDI,JINA LA BWANA LIBARIKIWE,NA MUNGU AMLAZE MAHARI PEMA PEPONI AMEN

    ReplyDelete
  8. ANKAL MICHU, POLE SANA KWA MSIBA WA NYANYA. MUNGU AILAZE PAHALA PEMA ROHO YAKE, AMINA. MWITA, LONDON

    ReplyDelete
  9. poleni sana kwa msiba

    ReplyDelete
  10. poleni sana

    ReplyDelete
  11. Michuzi umekosea kusema uislam umerithishwa .
    Dini mheshimiwa hairisishwi.

    ReplyDelete
  12. Ankal alikuwa na dhumuni la kuonyesha jinsi dini mbili zinavyoweza kuinteract na mambo yote yakaenda shwari, naona wadau waliotoa comments hapa hakuna hata mmoja aliyeliona hilo!!! Thats from My understanding especially when wrote that he uploaded many pics for a special reason!!!
    Nanjilinji!!!

    ReplyDelete
  13. Poleni sana Ankal kwa kuondokewa na kipenzi.sasa nauliza mbona nyanya anaonekana mzungu kwa umbali?yupo kama africast..halafu hata jina lake...

    ReplyDelete
  14. Poleni sana. Ikija suala la kurejesha namba kwa Muumba, hapo sisi binadamu hatuna ujanja tena. Tunaomba Muumba ampokee katika ufalme wake.
    Nimefurahishwa na sherehe ya mazishi. Ankal mmedumisha mila za kiTanzania: ninajua kuwa mna uwezo lakini hamkutenganisha waombolezaji kati ya wenye suti za ulaya na khanga kama mtindo ambao umeanza kuibuka jijini dar kutokana na ulimbukeni. mmeruhusu watu wote wachanganyikane bila kuwagawa katika matabaka ya walio nacho na wasio nacho na wote kwa pamoja wanatimiza azma ya kumwombea marehemu. nikiri kuwa ninachukukia ulimbukeni (ambao kwetu hapa umechochewa na ufisadi).
    Mungu ampokee katika ufalme wake!

    ReplyDelete
  15. Unkal pole sana kwa kuondokewa na Nyanya yako. kazi ya mola haina makosa. Lakini swali la ufahamu ankal, umesema amezikwa ndani ya kaburi la mumewe? Inaamana wakati wanatengeneza kaburi la Nyanya ilibidi mwili (mifupa) samahani ya Mumewe iwekwe vizuri humo humo ndani ili Bibi naye alale ubavuni mwa mumewe?? Haya ni mapenzi makubwa sana

    ReplyDelete
  16. poleni sana wafiwa wote, pole ankal pole sana ila jamani naomba kuuliza mbona sijawahi kumuona or kumsikia japo kwa kutajwa tu mke wa ankal? Nilitegemea sana ankal angekuwa na mkewe kwenye msiba huu mzito kwa ankal, naomba jibu kwa yeyote ajuae tafadhali.

    ReplyDelete
  17. Poleni sana Mungu amuweke mahali pema peponi, Amin

    ReplyDelete
  18. Poleni sana ankal.

    Mwenyezi Mungu awape subira.

    (US Blogger)

    ReplyDelete
  19. MsemakweliApril 11, 2010

    Poleni uncle na familia.

    ReplyDelete
  20. Kaka Michuzi pole sana kwa kufiwa na Nyanya. Mungu ailaze pema roho yake peponi.

    ReplyDelete
  21. pole kaka hila na suggestion sizani kama ni vyema kuweka picha za makaburini na mwili ya marehemu kwenye blog too much pictures ,zina tisha. pole lakini

    ReplyDelete
  22. Rafiki yangu,

    Poleni sana. Bwana Awe Nasi. Amen.

    Fidelis.

    ReplyDelete
  23. Poleni sana.
    Mungu ailaze roho yake pema peponi na awape nyote nguvu.

    ReplyDelete
  24. Asalaam alaykhum ankal

    poleni sana na msiba mola aiweke mahala pema peponi roho ya mpendwa nyanya yenu amiin.

    Chef Issa

    ReplyDelete
  25. pole ankal kwa msiba. ndagha kyala.amen.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...