
Dogi huyo inasemakana alikuwa amefuatana na moja wa mafundi mitambo wa bendi ya Ngoma Africa ktk kusherekea pasaka..lakini alipofika mlangoni gari la manjago lilisimama ghafla na kumchukua Dog domo baya - kwa makosa ya kutokuwa na kinga ya wavu wakuziwia mdomo ili kutowang'ata raia. kosa lingine ni kuwa Dogi Domo baya ni kiumbe asiyetakiwa kujichanganya katika mkusanyiko wa binadamu!
wadaku wanasema kisa iko ni kutokana na kisasi cha mtasha moja ambaye siku za nyuma paka wake alivamia mishikaki ya FFU na kufunguliwa mashtaka na baadhi ya wanamziki wa bendi hiyo, na baadaye kesi hiyo kuingiliwa kati na kufutwa na kiongozi wao Ras Makunja. Mtasha huyo inasemekana ndiye aliewachomea utambi FFU kwa manjagu kuwa kopro Domo baya anajichanganya na binadamu katika mnuso huo wa pasaka!
kopro Dog Domo baya amewekwa katika rumande maalumu ya wanyama,hadi Pasaka itakapoisha,hakuna dhamana.
mpaka tunaenda mitamboni, kamanda wa bendi hiyo Ras makunja hakuweza kupatikana kwani kila saa simu yake ilisema mwenyewe kazima, jaribu tena baadaye. inaelekea kazima simu kwa kukwepa hoja.
Why speaking in parables?
ReplyDeleteSema tu usikike!!
Sasa hii ffu imekuaje????mbona sielewi,mnaenda na mbwa ktk paty?
ReplyDeletetena mbwa wenyewe bull dog kichaa
kama si kuwataka ubaya manjagu.
kamanda Ras makunja sooo ili vipi?mbona ndugu yenu kopro dog domo baya anabaguliwa?ras tunaomba ufafanuzi basi,pia washa simu
ReplyDeletekamanda wa ff ras makunja sasa wewe si hodari wa kuyashikia bango ya wenzio?mbona hili soooooo la ndani ya kikosi chako unalizimia simu??????? mjeshi mwenzenu dogi kichaa kopro dogi domo baya yupo mokononi mwa chombo cha dola??
ReplyDeleteHuo ni unyanyasaji wa kidogi dogi.Mbona dogi domo baya ni poa freshi kabisa na unaona pozi yake?
ReplyDeleteBinadamu mna roho mbaya sisi madogi mnatuonea, kama hamuwezi kuishi naye mlete huku kwetu kila siku twala swala freshi.