
Kwa Kushirikiana na SickKids Hospital ya Toronto, natafuta watoto wagonjwa, chini ya miaka 14 ambao wanahitaji operation moja ili wapone na kwamba matibabu hayo hayapatikani Tanzania. Matibabu yote ni bure hospitali; na gharama za kuishi huku kwa mtoto na baba au mama najitolea mimi.
Tunaweza kuanza maongezi sasa na tukaonana nikija March. Pia napenda kuwajulisha kwamba Serikali ya Canada, kupitia CIDA, imetangaza kutoa misaada zaidi kwa Tanzania na Ghana kwa mambo ya afya. Nina imani serikali ya Tanzania imejulishwa tayari.
Kama una ndugu yako, jirani yako au mtoto unamjua, tafadhali wasilisha report ya Daktari pamoja na maombi kwa anuani hapo chini:-
Mabula Sabula
Executive Vice President
Dillon-Kaijuka Associates, Inc.
108 S. Joliet St.,
Joliet, IL. 60436
USA Investment & Development Services
Tel: +1312-376-8106
E- Fax: +1206-337-1688
Skypename:mabsab
Canada: Tel: +1416-546-6542
Cell: +1647-281-6474
or
Au wasilisha kwangu najua jinsi ya kumfikishia
Ndugu Mabula.
Tel: +255 713 666616
au Zilete Chuo Cha Diploamasia,
Kurasini – Dar Es Salaam,
ulizia
Ndugu Pius Mikongoti
NB: Ndugu Mabula ni Mtanzania na alikuwa hapa nchini siku chache zilizopita, Naomba tutumie nafasi hii kwa wale wanaowajua watoto wote wenye matatizo ilimradi wako chini ya miaka 14. Asanteni.
Duh! Ni bahati iliyoje kwa watanzania wenzangu. ni vema tukatumia nafasi hii adimu. Mungu amjaalie huyu ndugu aliyetukumbuka na sisi huku kwa matibabu.
ReplyDeleteKampuni ya investment na masuala ya misaada mbona kama haiendani?Isije kuwa ni mambo ya kujinufaisha
ReplyDeleteNgekewa iliyoje....ila wabongo nawajua,watoto wote wagonjwa watakuwa chini ya umri wa miaka 14 ili wapate matibabu ya bure ha ha ha ha ha...bongo jua kali bwana...
ReplyDelete