habari yako Ankal michuzi,
mimi ni mmoja wa wawanachama wako hapa lakini leo nimeona vichekwesho vya znz mtu raia wa msumbiji kapewa kadi ya uraia wa zanzibar na juzi tuu kapiga kura ya muzambiq sasa naomba msaada wako uniwekee hii
Mdau Zenji









Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 33 mpaka sasa

  1. Huu ni mkakati wa FRELIMO na CCM
    Si huyu tu kuna wengine wametokea hukoo ati wameandikishwa wamezawa pPemba au Makunduchi, bora awe Msukuma au Mnyamwezi tunaweza kuelewa lakini jamaa ametokea hukooo, hata Kiswahili tabu!

    ReplyDelete
  2. We Mzanzibari ni Mbaguzi sana!!

    Hakuna cha ajabu kuwa na utambulisho wa nchi mbili.. Mimi nina uraia wa USA na pia bado nina documents za Tanzania..

    Hapa Arizona wanaandamana kutaka kufutwa sheria mpya ya Ubaguzi wa wahamiaji, sasa tena na wewe Mzanzibari unaaleta nongwa kuwafukuza wa Africa wenzako, ambao wote mko huko Mavumbini.

    Acha roho mbaya we kijana.. watu wanatafuta maisha then unakuja kuwahanika hadharani kama hivi.

    Elewa umeshamletea shida huyo Babu wa watu.. jutia nafsi yako kwa hilo!!

    ReplyDelete
  3. Hapo tatizo liko wapi? Ndiyo mambo ya Dual citizenship hayo.

    ReplyDelete
  4. nchi hilisha uswa wewe.hujuhi ?

    ReplyDelete
  5. We achakua mnoko znz mnakuona kama kama wapi sijuwi. wakati nyinyi ndio wakimbiaji wakubwa kwenda kwa wenzenu wacheni ubaguzi . nyinyi mbona mejaa msumbiji. tushikamane kuhenzi muungano wetu wajinga wasio upenda mungu hawa rani wafe

    ReplyDelete
  6. wewe mnoko wa Wed Apr 28, 01:29:00 PM hebu kwanza kajifunze kiswahili kabla ya kujigamba kuwa umzalendo wa kweli.

    ReplyDelete
  7. Kila siku nasema, sisi Watanzania tuna roho mbaya sana, roho ya chuki sana, tena sana. Jelosi itatuua.

    Kwanza atuambie kapataje dokumenti za huyu Mzee Matete. Huyu mzee saingine ana haki zote za kupata uraia wa Tanzania na hajaamua kuukana uraia wake kama Watanzania wengi nje na ndani ya nchi.

    Pili, kuna Watanzania wengi tu nimekutana nao Marekani, Canada na Australia ambao wana pasi mbili mpaka tatu.

    Ameniudhi sana huyu Mdau, na utakuta anasota waya sana Bongo, anakula vumbi kila siku ya Mungu. Labda kanyimwa viza sana. Bado, atakonda sana, Mungu atakuonyesha na roho yako ya kishenzi.

    ReplyDelete
  8. mtowa maoni wa Wed Apr 28, 12:54:00 PM hebu tuliza mashetani yako, na wacha kuita watu wabaguzi hapa.

    Hatujali kama una una vitambulisho viwili au vitatu huko uliko. suali liloletwa hapa ni kuhusu tanzania.

    Tanzania BADO haijaruhusu dual citizenship, na huyu mleta hii habari ameuliza tu, hii imekuwaje? huyu jamaa anakuwa amevunja sheria ya nchi.

    Na hata wewe mwenzetu ukituwa hapa tanzania na kutuonyesha pasi zako mbili moja ikiwa ni ya tanzania basi unakuwa mkosa.

    Tunajuwa wapo watanzania wengi wana pasi mbili lakini hawazidodeshi wakifika huku kwani wanajuwa ni makosa. kama huamini njoo likizo na pasi zako zote mbili uone kama hukulala keko unless wajomba zako ni watu maarufu hapa nchini.

    ReplyDelete
  9. Ama kweli tanzania ni tambarare!!! iko wapi data protection hapa? watu wanafanya kazi katika maofisi ya serikali na wana access personal details namna hii na wanaziweka hadharani namna hii?

    ReplyDelete
  10. jamani jamani sasa huyu mleta habari hii ameona cha ajabu ni nini haswa hapo, hivyo vyote ni vitambulisho na sio Passport, mimi ni mtanzania na bado nina passport yangu ya Tanzania ila kwa kuwa ni mkazi wa South Africa ID card yangu ni South Africa. Mbona hili wala halihusiani na Dual Citizenship ni vitu viwili tofauti.

    ReplyDelete
  11. DARAJA LA UMOJA UNAFIKIRI KAZI YAKE NI NINI? KAMA SIO KUONGANISHA WATU

    ReplyDelete
  12. Dual citizenship
    ndo maanake
    halijaaribika jambo hapo

    ReplyDelete
  13. nahisi alietuma na kuweka ukweli huu ni sawa kabisa, kwani dual citizen in Tanzania imekubalika? wangapi wakaazi wa zenji wamekosa kitambulisho hicho wakati ni muhimu kwao, hao wahamiaji ndio wanaokosesha haki wenzao.
    BIG UP kwea kutuonesha ukweli.
    Mdau India

    ReplyDelete
  14. Mbona mmekimbilia kuconclude kuwa ni mtu wa Msumbiji mwenye kadi ya Zanzibar? Mwajuaje kama ni Mzanzibari mwenye kadi ya kupigia kura ya Msumbiji? Mnajuaje kama alikuwa anaishi Msumbiji lakini ameamua kurudi nyumbani Zanzibar? Wabongo acheni unoko na roho za kwanini! Kama maisha yako hayaendi sawa embu zidisha sala, sio kuharibia wengine. Kwanza hapo mmemvunjia haki yake ya kimsingi ya kuhifadhiwa uutu wake na usiri wake. Mmeingilia mambo ya watu ya binafsi. Kama kweli anakosa ingebidi taratibu husika zifatwe na si kumlipua mbaba wa watu.

    ReplyDelete
  15. watu wanatoa maoni wakiwa na jazba..maana ya kitambulish cha mzanzibar...ni kuwajua wazanzibar na wasiokuwa wazanzibar...sio lazima kuwa kwa sababu zanzibar iko Africa ndio kila mwafrica atakuwa mzanzibar....nakuwa na kitambulisho hicho lazima uwe na sifa za kuwa mzanzibar..kama ilivyo kenya....nasio kumwita mtoa habari kuwa mbaguzi kama ni ubaguzi waliunza serikali ya mapinduzi zanzibar

    ReplyDelete
  16. HATI YA ZANZIBAR IMETOLEWA 2005 NA YA MSUMBIJI 2009. LABDA AMEPATA URAIA WA MSUMBIJI AKAMAAMUA KUBAKI NA KUMBUKUMBU YAKE. KAMA UNAONA AMEKOSEA ILIKUWA NI KUMPELEKA KWENYE SHERIA NA SIYO KUMUHUKUMU HAPA. INAWEEZEKANA ANA HAKI KABISA AU KUNA MAPAUNGUFU KWENYE SHERIA ZA SEHEMU MOJAWAPO.

    ReplyDelete
  17. Nyie mwaongelea tu habari ya dual citizenship....ebu tazameni hiyo tarehe ya kuzaliwa...mbona zinapishana????ingekuwa ni tarehe t,tungesemawamekosea hiyo 0,lakini mwezi january na december wapi na wapi bwana??? hapa iko namna

    ReplyDelete
  18. huyo ni mzanzinari, hati ya msumbiji ni visa iliyobandikwa kwenye passport yake na hiuo nyingine ni kadi ya kura. sasa hapo huoni kuwa ni vitu viwili tofauti?

    ReplyDelete
  19. Suala linakuja angalieni mahala palipoandikwa sehemu ya kuzaliwa katika hati zote mbili!
    Huu ni ughushi na haswa twajua kuwa waletwa wageni Zanzibar kupiga kura kudhulumu wananchi..Hatukatai umoja na muungano, hivi ni vitu asili hata kabla ya Muungano ulioletwa na Mwl.Nyere na Karume umoja wetu na Muungano wetu ulikuwepo kwa karne nyingi mno na watu walioana na kuzaana ila mambo haya?!Dual citzenship haipo Tanzania, labda tuseme jamaa alinunua Uraia Msumbiji na akanunua sehemu ya kuzaliwa na akanunua jina na wazazi !!Hilo litafahamika.
    Tunaomba salama kwa nchi zetu mbili hizi majinamizi yatoke na mapepo wabaya watoke, dhulma idhihirike

    ReplyDelete
  20. (A) Kitambulisho cha Mzanzibari ni cha mwanzo so hana kosa (B)Kuwa na kitambulisho, sio uraia kwani Mbona kuna raia hawana? kwa tunavofahamu Hicho ni kitambulisho cha ukaazi na si cha uraia,Sheria inasema uwe umekaa Zanzibar kwa muda wa miaka 3-5 so hata kama ana uraia mwengine basi kwa kuwa katimiza haki ya ukaazi ana haki ya kuwa nacho.(C)Hicho cha Msumbiji mbona hakina hata Jina lake na mwezi wa kuzaliwa kina tofauti na cha zanzibar.Pia picha inaonesha ya kubandikwa tu,huyu aloweka hii mada ni mnafiki na muongo tu anapandikiza chuki tu-Mbona Uk ukiwa mwanafunzi tu unapiga kura? kwa kuwa ushatimiza haki ya ukaazi tayari na yeye ameshatimiza haki ya ukaazi.MWISHO MICHUZI HUWA NAKUPA USHAURI KILA SIKU Nimekutumia document nilifuta majina kuhifadhi data za mtu na hujaiweka Itakuaje uruhusu data za mtu hadharani kwa nini msifute majina na TAREHE MKAWACHA PICHA TU? Na hao wadau wanaosema mambo ya muungano hapa hatuzungumzii Muungano sio Mimi pia ni Mzanzibari ndugu zangu wamepiga kura lakini baba etu hajapiga kura sasa hapo hushangai?

    ReplyDelete
  21. huyu mtu kwa hali halisi inaonesha ni raia wa msumbiji kwani ana pasipoti ya msumbiji ya mwaka 2009, mimi nahisi amebadili uraia wake na kuwa wa msumbiji awali alikuwa mzanzibari "kitambulisho cha mzanzibari 2005" na si foreigner ID card. sasa kama anadai yeye ni mzanzibari hayo ni makosa kisheria hatuna dual citizenship.
    ni kama jambo dogo lkn ni kubwa maana hapa ndipo yanapokuja malalamiko ya kupandikiza wapiga kura mamluki na hatimaye umwagaji damu.
    privacy: hizi ni screen shots kutoka mzalendo.net ukiangalia pembeni mwa picha utaona.

    ReplyDelete
  22. watu kama hawa inabidi tuwafanyie ile kitu tulomfanyia mmasai kule kiwengwa.
    Kama kuna myamwezi hapa alokimbilia ZANZIBAR kuchafua hali ya hewa huko basi ajuwe sasa kuwa Vijana wa kizanzibari wako macho.tutafirafira wote hawa.
    jitayarisheni!

    ReplyDelete
  23. Poleni wooote....
    NImekubaliana na mdau mmoja hapo juu... I.D card ni tofauti na uraia kama residence permit pia si uraia.
    Ni kadi ya utambulisho tu, ni nchi nyingi wanatoa I.D kadi ili iwe rahisi kumtambua mtu. Hususan nchi za wenzetu, Kwa hapa UK since 2008 home office wamekua wakiwapa woote wanao renew visa zao ID card, na chaajabu raia wao hawanazo na wanazipiga vita.

    Kwa hiyo mleta mjadala, hiyo ni Kadi ya kumtambulisha tu! ama Tanzania wanatoa kwa raia tu na si kwa wageni? Labda wenyekujua watuambie......
    WHO IS ENTITLED TO GET AN I.D CARD IN TANZANIA? IS IT ANY RESIDENT? I MEAN ANYONE RESIDING IN THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA? OR ONLY THE CITIZENS OF TANZANIA?
    MPO HAPO? Hivo vitambulisho ni vya Raia? ama mkazi?

    ReplyDelete
  24. WEWE ULIYE HILETA HII HABARI LAZIMA UWE MNOKO SANA WEWE ULIWEZAJE KUPATA DOCUMENTS ZA HUYU BABU NA KUZI POST UKU!! we lazima utakuwa kibaka ulimmendea babu kalala nini ?

    ReplyDelete
  25. Tatizo linakuja pale ambapo mzaliwa wa Pemba anapoambiwa kwamba hawezi kupata kadi ya utambulisho mpaka apeleke cheti cha kuzaliwa na vitambulisho kibao, hata kama Sheha ana uhakika wa uzawa wake.

    Lakini huyu ambae sio mzawa kabisaa yeye anapeta tu, je hiyo ni haki?

    ReplyDelete
  26. Baba UbayaApril 28, 2010

    mbona inasema ni I.D na sio passport?yaonekana hakuna utata kwani I.D haimaanishi wewe ni raia wa nchi hiyo.tena walau yeye serikali inatambua kwamba kuna mgeni na anaishi kihalali.

    ReplyDelete
  27. Watanzania ndio maana nchi inauzwa watu wakiwa macho. Nyie mnaomsema huyu whistleblower wote kama hamnazo. Mnaojifanya mna pasi mbili nawaza kuwa kweli mmezipata kihalali au? Tanzania bado haina dual citizeship sasa nyie kuwa na mbili ni vipi? Mbona mimi nilisurender yangu iweje nyie hamkuambiwa kusurender pasi zenu kwa vile nchi yetu haina dual citizenship na muwe nazo mpaka leo?

    Na kama mnasema hii ni ID card mbona imeandikwa raia Mtanzania?

    Kama hizi card ni kujulikana kuwa ni Mtanzania halali au niza kumwezesha mtu kuvote ni watu wangapi watapewa ili wasaidie wengine kupata kura zisizo za kihalali? Kweli ni lazima kila kitu kiwekwe nje na ijulikane alipataje hiyo card. Na aliyempa au waliompa lazima wawajibishwe. Ni magaidi wangapi watatumia pasi zetu kufanya mambo ya ajabu nje ya nchi kama tusipokua waangalifu?

    Mahali alipoipata huyu mtu hizo documents hapa sio issue....hiyo itakuja baadaye

    ReplyDelete
  28. Tarehe za kuzaliwa tu ndio zimebadilishwa...

    What a country!!!!!

    Waelimishwe hao wanaovitoa hivi vitambulisho. Si ajabu huyu mtu kaenda mwenyewe kwenye office za vitambulisho kaonyesha pasi yake ya msumbiji na bado kapewa card....

    Tutafika kweli????

    ReplyDelete
  29. Ms B. RugarabamuApril 29, 2010

    duh hicho kiswahili cha baadhi ya wadau mie hoi..
    huwa najiuliza sana hv hili somo la kiswahili si linafundishwa kuanzia shule za msingi?na mbn watu wengi hawawezi kuandika kiufasaha?au hawa watu walikuwa wazito darasani na si wasomaji wa vitabu?
    teh teh teh!
    Jamani wazanzibar wabaguzi kweli hasa wapemba sijui kwanini..?huyo mzee matete si ndugu yenu kabisa kuanzia jina mpk sura jamani?
    muacheni mzee wa watu ni mhangaikaji anahamahama kutafuta maisha,sio ww mdau unaekaa kufuatilia maisha ya watu hayakusaidii,hayo mambo waachie wenyewe mafisadi wenye nchi,hata ukijifanya una mapenzi na nchi yako utaendelea kutaabika na rasilimali kufaidi wachache,
    unamchongea mlalahoi mwenzio ili wampe kashkashi ili we upate nini?
    hii nchi ina wenyewe ,so we piga kimya cheki utaishije we na familia yako,,period!

    ReplyDelete
  30. tuache yoote kuna watu wametoa maoni mtu wa nne na wa tano mbona kiswahili chenu kibovu na ninyi raia kweli wa jamhuri yetu hii au feki?

    ReplyDelete
  31. Nadhani uwelewa wetu wa kumjua nani Mzanibar ni mdogo lakini sheria ya Zanzibar inasema kwamba wabara wote wanaotaka kuishi Zanzibar sharti wakae Zanzibar kwa miaka 15 mfululizo ndio wapeleke maombi yao ya kutaka kutambuliwa kama wao ni wazanzibar kwa Waziri wa Nchi Tawala za Mikoa na Vikosi vya SMZ.Hapo akiridhika nawe ndio unakua Mzanibar na utastahili kupata haki zote wanazostahili Wazanibar kama vile Kumiliki ardhi ambapo kwa sasa wabara wanaruhusika kumiliki si zaidi ya ekari tatu,lakini ukiwa mzanibar unauwezo wa kumiliki hata ardhi ya Zanzibar yoye hamna kikomo,haki nyengine ni kama ile ya kuchagua na kuchaguliwa.
    Lakini kwa mgeni kama huyo ni lazima aombe Uraia kwanza wa Tanzania baada ya kupata uraia itamlazimu akae Zanzibar kwa miaka 15 mfululizo kisha aombe kwa waziri husika akikubaliwa ndio atakua sasa ni Mzanzibar na ndio atastahili kupata hicho kitambulisho cha Uzanzibar ukaazi.
    Ama kwa hili idara ya vitambulisho imechemka kwani ilitakiwa kama sheria inavyoeleza ni kwamba ili kuthubitika kama wewe una sifa ya kupewa kitambulisho cha ukaazi basi ni lazima upeleke cheti chako halisi cha kuzaliwa na wala sio copy.

    ReplyDelete
  32. oya mmekula kwanza ama mnaongea tu ???

    ReplyDelete
  33. wazanzibar kwa ulalamishi mmezidi..
    sasa huyo anatakiwa alalamikiwe na wazanzibar au wamozambique?
    mbn kilichoanza kutolewa ni cha zenji?
    ina maana cha msumbiji kapata juzijuzi tu,wao ndo wangelalamika kwamba kapewa cha msumbiji ilhali ni mzenji.2005 na 2009 ipi ilianza?
    Tumewachoka na mpewe kinchi chenu tupumue,maona dili wakati huku bara ndo kila kitu kwenu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...