Hasheem Thabeet enzi zake katika tizi wakati akichezea Vijana City Bulls kwenye kiwanja cha Zanaki jijini Dar. Hivi sasa anaendelea vyema huko Marekani na kupata habari zake za karibuni

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. Yaani ile 'link' ndio inazungumzia maendeleo ya Thabeet??? Mbona wakati anafanya vizuri tulikuwa kimya??

    Sasa hivi timu yake inasuasua; nadhani wameshaanza kuangalia msimu ujao! Lakini wiki kama tatu zilizopita dogo alikuwa kwenye form:

    http://vijanafm.blogspot.com/2010/03/tusimsahau-hasheem-jamani.html

    ReplyDelete
  2. Coach BAHATI MGUNDAApril 14, 2010

    mkuu Picha hiyo na maelezo yametofautiana, Hasheem alikuja zanaki siku hiyo akiwa na timu yake ya OUTSIDERs na inaonyesha wakati wakifanya warm up kabla ya mchezo wao na timu ya vijana "City Bulls" ambapo Vijana ilishinda!! lol Wadau msije anza kuona kama Timu YA VIJANA inataka kutumia mafanikio ya Hasheem kujipatia umaarufu!!! kwa picha isiyokuwa na habari sahihi.
    Coach BAHATI MGUNDA

    ReplyDelete
  3. UYO DOGO WA APO NYUMA NAE ANAWEZA KUJA SEMA NSHACHEZA NA JAMAAA KIKAPU, JAMAA WA NBA ASA NDO MJUE NA MI NI MKALI.

    ReplyDelete
  4. Aliyeniacha taabani ni huyo dogo nyuma ya hashim. Ebana vikono vya huyo dogo lazima vilikuwa kama robo ya ukubwa wa mpira lakini dogo hakujali wala kusijisikia tofauti na njemba nyingine.

    ReplyDelete
  5. Mhh jamani hasheem thabeet hajawahi kuchezea Vijana na hata ukiangalia hapo kwenye wachezaji ni(KUANZIA MBELE)DOWN,LLOYD,MALALE,CLAUDIO,ALLY,ALBERTO,HASHEEM NA KATOTO(labda ndio nchezaji wa vijana....... hao wengine woote walikuwa UDSM OUTSIDERS, baadhi wameshahama ila HASHEEM AMECHEZEA UDSM OUTSIDERS watu waache kukuza majina yao kupitia mtu jamani dah................. tutakubali club nyingine lini watanzania au ni raha kila siku ni JKT, VIJANA NA SAVIO???? Huu si mpira wa simba na yanga na masupa staa wao ulaya ni BASKET BALL....I WISH HASHEEM ALL THE BEST AND ALL OTHER BASKET BALL PLAYERS IN THE COUNTRY......BASKET BALL OYEEEEEEEEEE.

    ReplyDelete
  6. Watu wengi hawapendi kusema ukweli juu ya uchezaji wa Hasheem. Mimi kwa kweli sifurahishwi hata kidogo na uchezaji wake. Na hata wachezaji wenzake nadhani wanalitambua hilo. Utakuta mara nyingi Hasheem anazunguka tu uwanjani na ni mara chache sana anapasiwa mpira, hata pale anapokuwa kwenye "rangi". Au kazi anayofanya mara nyingi ni kuanzisha mpira baada ya kikapu kuingia upande wao. Hasheem hawezi kabisa kudrible kwa kukimbia na mpira.Ni mrefu lakini sijaona hata siku moja akirusha mpira wa point tatu. Kwa urefu wake angekuwa ni mali sana kama angekuwa na uwezo wa kupiga point 3. Kwa ujumla anapocheza utamuonea huruma, ni kama wenzake hawamwamini kabisa na mpira. Jamaa bado anasafari ndefu. Anatakiwa ajifue zaidi katika mambo yatayoweza kumfanya abakie NBA kwa muda mrefu. Mdau USA.

    ReplyDelete
  7. Mdau ma senta wengi si kazi ya kudribo, ndio mana kuna hao ma-guards. Pia center wengi sio wazuri kurusha point 3 kwa ivo usimlaumu Hasheem kwa hilo, ma senta wanatakiwa wawe wakali wa kupasi na kwene post na screen plays.

    ReplyDelete
  8. Dogo mkali kweli huyo Nyuma anawacha kwanza Vibonde vitangulie Kurusha Hahahaahah. Mungu atamsaidia atapata kuwa naye mfano kufuata wana Jamaa yetu Hasheem Thabeet. Baba Ubaya.

    ReplyDelete
  9. Senta hana kazi ya kudribo, kuna magadi ndio wanafanya kazi hiyo. Senta anatakiwa kutisha chini ya kikapu kwa madanki kama Dwight Howard, Andrew Bynum, kwa kucheza na board kama Tim Duncan, kwa kuchezesha kutoka chini ya kikapu kama Shaq, kubloku kama Dikembe Mutombo, na kunasa mipira ya ribaundi kama Pau Gasol. Timu inamtegemea Thabeet aje kuwa nyota wa kubloku.
    Kwenye hiyo picha wa pili kulia sio Mohamed Rajab aka Athuman Machuppa?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...