Kamanda wa Kikosi cha Mbwa na Farasi nchini , ASP Egyne Emmanuel , akitoa shukurani kwa niaba ya Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini ( IGP) Said Mwema kwa baadhi ya wataalamu wa mradi wa APOPO ( hawapo pichani ) wa SUA, Aprili 14 mwaka huu mara baada kukabidhiwa mbwa sita waliofuzwa utaalamu wa kutambua milipuko na mabomu yaliyofichwa
Mmoja wa Mtaalamu wa Mbwa kutoka Mradi wa Apopo uliopo chini ya Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo ( SUA), Patrick Mbuna akicheza na mbwa mwenye jina la Deby ambaye amepatiwa mafunzo maalumu ya kutambua milipuko na mabomu yaliyofichwa kabla ya mbwa sita waliofundishwa mbinu hizona Mradi huo kukabidhiwa kwa Jeshi la Polisi nchini Aprili 14, mwaka huu Chuoni hapo.
Mtalaamu Mwandamizi wa ufundishaji mbwa kutambua mabomu wa Chuo Kikuu cha Sokine cha Kilimo ( SUA) kutoka Mradi wa APOPO, Fidelis John ( aliyeshika kamba ya mbwa) akimwingiza kwenye chombo maalumu cha kusafirishia mbwa waliofudishwa mbinu za kutambua milipuko na mabomu yaliyofichwa ikiwa ni makabidhiano ya mbwa sita kwa Jeshi la Polisi , Aprili 14 mwaka huu na Mradi huo uliopo chini ya SUA.
(Picha na John Nditi)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. NEXT TIME USIMUWEKE MBWA KWENYE GARI LILILOZIBWA HIVYO HASA KATIKA NCHI KAMA TANZANIA YENYE JOTO ANAWEZA KUFA HASA UKIZINGATIA SYSTEM YAKE YA SWEATING. HUWA ANATOWA JASHO KUPITIA ULIMI WAKE. MASS YA MWILI WAKE NI KUBWA SANA KUTEGEMEA ULIMI TU SO NI RAHISI KU-SUFFOCATE NA KUFA, BEBA MBWA KWENYE GARI OPEN

    ReplyDelete
  2. Sidhani kama kuna haja ya kuwa na mbwa wa kutegua mabomu yapi kwanza wawapeleke afghanistan sie tunahitaji mbwa wa kukamata vibka na majambazi ambao wamekuwa kero kubwa ktk nchi yetu, watu hawakai kwa raha , hununui kitu roho ikatulia kila kukicha majambazi nchi gani sasa hii, amani hakuna kabisa,,,, Apopo please fundisheni mbwa kukamata hao wahusika jamani

    ReplyDelete
  3. Mambwa mazuri kweli hayo....Nadhani ni German Shepherds hayo ...very nice dogs...I hope yatatunzwa vizuri....

    ReplyDelete
  4. Anon wa 1 na 2 haiitaji tochi hiyo.

    ReplyDelete
  5. Prpf: PETER NALITOLELAApril 17, 2010

    HAO MUMBWA BWANA NI MAKINI SANA. WAMESOMA NA MAJINIAS KAMA MICHUZI, NABII YOHANA MASHAKA NA KANUMBA. HAO NDIO MA JINIAS WA TANZANIA PAMOJA NA RIDHIWANI MTOTO WA MUENENE. HAO MBWA WANELEWA KIINGEREZA NA KISWAHILI KWA MAANA MUZUMBE WALIKUWA WANAFUNDISHWA LUGHA ZOTE BWANA. KWA HIYO TUNAOMBA YALE MABOMU YA MBAGALA WAYANUSE WASIJE YAKATEGUKA TENA.

    ReplyDelete
  6. Kipara kinachompiga naniliu wakoApril 17, 2010

    Ngoja nikumbuke utotoni. Eeh bwana dogi la mzungu ni kubwa kuliko dogi la kiswahili? Ha ha ha ha ha.

    ReplyDelete
  7. Jamani SUA tunaomba mtu fundishie mbwa wa kuwaweka viwanja vya ndege vya kimataifa kwa ajili ya kuwatambua mafisadi [waeshimiwa] wanapo safiri mamtoni ili waumbuke .

    ReplyDelete
  8. wategue mabomu yapi wakati sikuhizi watuwakiiba Benki hawayategi wanayarusha tu.
    Chakula chenyewe cha kuwalisha kipo?Nyama hiyo hiyo ya mbwa koplo nanii pale anaipiga kaponi ,mbwa watakula pumba hao mpka wabaki mifupa mitupu kama mbwa wetu wa uswahilini,
    ha ha haa

    ReplyDelete
  9. kwani nchi iko katika vita ? mngewafundisha jinsi ya kuwatambua wabeba unga wapelekwe a-port ingesaidia sana manake akikunusa kama una ishu inakula kwako

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...