Waziri wa Fedha na Uchumi Mustafa Mkulo akijaribu mmoja ya baiskeli alizokabidhiwa hivi karibuni na Rais Kikwete kwa ajili ya kuwasaidia waathirika wa mafuriko wa Kilosa. Baiskeli hizo na misaada mingine ilitolewa na Serikali ya China .

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Jakaya Mrisho Kikwete ametoa msaada wa vifaa mbalimbali kwa ajili ya waathirika wa mafuriko ya wilayani Kilosa, mkoani Morogoro.

Vifaa vilivyokabidhiwa hivi karibuni Ikulu jijini Dar es salaam na Naibu Katibu wa Rais Ndugu Shabani Gurumo kwa niaba ya Rais Kikwete kwa Waziri wa Fedha na Uchumi Mh. Mustafa Mkulo.

Vifaa vilivyotolewa na Rais Kikwete ni pamoja na pikipiki,
baiskeli na Viatu kwa jinsia zote.

Akipokea vifaa hivyo kwa niaba ya waathirika wa mafuriko wa Kilosa ,Waziri wa Fedha na Uchumi Mh. Mkulo alisema kuwa vifaa kama vile baiskeli na pikipiki zitapelekwa kwa Maafisa Elimu , Waratibu wa Elimu na Chuo cha Vijana cha Ilonga.

Aliongeza kuwa wengine watakaopata msaada huo ni Chuo cha Utafiti, Shule za Sekondari na Chuo cha Ualimu.

Aidha , Mh.Mkulo alisema kuwa misaada hiyo imekuja wakati muafaka nakuwa itasaidia kupunguza tatizo la usafiri na kuongeza kuwa atahakikisha inawafikia walengwa mapema iwezekanavyo.

Waziri Mkulo alisema kuwa, vifaa hivyo ni msaada kutoka Serikali ya China kwa Mhe.Rais Kikwete na ambapo yeye aliamua kuvitoa kwa waathirika wa mafuriko ya Kilosa.

Rais Kikwete aliamua kutoa msaada huo baada ya kuwatembelea mapema mwezi wa pili mwaka huu na kujionea jinsi mafuriko yalivyoathiri eneo hilo na ndipo aliahidi kujitahidi kuwatafutia vifaa mbalimbali ili viwasaidie kuanza maisha mapya.


IMETOLEWA NA MSEMAJI MKUU
WIZARA YA FEDHA NA UCHUMI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...