Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na baadhi ya chipukizi wa CCM muda mfupi baada ya kuwasili katika viwanja vya Karimjee ambapo aliongoza kikao cha Halmashauri kuu ya taifa ya CCM (NEC).
Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Zanzibar Amani Abeid Karume na Katibu mkuu wa CCM Bwana Yusuf Makamba wakiingia katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam leo tayari kuanza kwa kikao cha Halmashauri kuu ya taifa ya CCM (NEC).
Baadhi ya wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) wakiwa katika kikao chao leo katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam.
(Picha na Freddy Maro)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. pamoja na ufahamu wangu kwamba ccm sio gwanda la kijani lakini wenzangu mmegundua kwamba rais karume huwa havai gwanda la kijani hata kwenye shughuli za chama?

    ReplyDelete
  2. MKUU NIPE CHEO CHA WAZIRI ASIYEKUWA NA WIZARA MAALUMU UONE NCHI ITAKAVYO NYOOKA KWA MWAKA MMOJA TU!!!

    MKEREKETWA MKUU WA CCM, mi siyo wale wabeba mabox wazushi tu!!!

    we Ankal unabania sana story zangu sasa hii nayo ibanie tuone kama utapata VISA ya kuruka UKerewe

    ReplyDelete
  3. eti ni kwa nini Karume huwa si mara nyingi kuvaa nguo za ccm (kijani au njano) anapokuwa katika shuhuli za ccm?

    ReplyDelete
  4. Mimi kwa kweli nashindwa kuelewa na niliwahi kumuuliza Ankal hili swali lakini akakauka naomba nirudie tena sijui atatoa haya maoni?!

    JE MWENYEKITI WA CCM NI RAISI JAKAYA MRISHO KIKWETE AU NI BWANA JAKAYA MRISHO KIKWETE?!

    Mzawa

    ReplyDelete
  5. Mh. Karume simuoni na kijani siku hizi, ama ndio mambo ya CCJ hayo.

    ReplyDelete
  6. Benki ya Dunia yaikopesha Tanzania mabilioni ya umeme

    Na Mwandishi wetu

    Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Dunia (WB), imeidhinisha Dola za Marekani milioni 25 sawa na zaidi ya Sh. bilioni 33 kwa ajili kuikopesha Serikali ya Tanzania kwa ajili ya kusaidia kutekeleza miradi ya umeme katika maeneo ya vijijini.

    Kadhalika, Benki ya Dunia kupitia Taasisi ya Maendeleo ya Kimataifa (IDA) imetoa msaada wa Dola za Marekani 105 sawa na zaidi Sh. bilioni 140.

    Kabla ya kutolewa kwa fedha hizo, Shirika la Mazingira Duniani lilitoa msaada wa Dola za Marekani milioni 6.5 sawa na zaidi ya Sh. milioni 81 kwa ajili ya kusaidia mradi huo mwaka 2007.

    Mradi huo umelenga kuboresha huduma za umeme katika vituo vya mikoa ya Dar es Salaam, Arusha, na Kilimanjaro na kuimarisha upatikanaji wa umeme nchini.

    Miradi hiyo ya umeme inalenga kuboresha upatikanaji wa umeme mbadala maeneo ya vijijini.

    Benki hiyo ilisema kuwa miradi hiyo inasaidiwa ili kuimarisha Wakala wa Umeme Vijijini ili kuwasaidia wawekezaji wa ndani kwa ajili kusaidia upatikanaji wa nishati maeneo ya vijijini.

    Miradi 80 imebainishwa ambapo kati ya hiyo 22 itapewa kipaumbele ambayo itaweza kuzalisha megawati 78.

    Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia katika nchi za Tanzania, Uganda na Burundi, John Murray Mclntire, alisema fedha zilizotolewa kwa ajili ya miradi hiyo kutasaidia kushusha bei ya nishati hiyo.

    Aidha, alisema fedha hizo zitasaidia kumaliza tatizo la umeme, kuboresha usalama wake pamoja na kuondokana na utumiaji wamafuta katika kuzalisha nishati hiyo.

    Aliongeza kuwa Tanzania inakabiliwa na matatizo ya umeme kwa kuwa vyanzo vya nishati hiyo vinategemewa kutoka katika maji ambayo hata hivyo sio ya uhakika na hukauka wakati wa ukame.

    Kati ya mwaka 2009 hadi 2010, miradi ya umeme imepatiwa jumla ya Dola za Marekani milioni 275, sekta ya miundombinu Dola za milioni 634.5, na maendeleo ya jamii ikiwemo afya na elimu Dola milioni 557.

    ReplyDelete
  7. Mavazi ni lugha. Mhe Karume ni muungwana sana anajaribu kupunguza ukereketwa usio na tija. Pamoja na kwamba ni mwana-CCM na makamu mwenyekiti, yeye wakati wote ni rais wa wazanzibari - waCCM na wasio WaCCM. Ninafikiri hicho ndicho anachojaribu kusisitiza. Kama angekuwa Rais wa Muungano tungeweza kumshawishi apitishe sheria ya kupiga marufuku vyama vya siasa kuwa na sare na bendera (mamabo ambayo yamepitwa na wakati. haya yalifaa wakati watu walipokuwa hawajui kusoma na kuandika)
    Pia mhe Karume ni nadra sana kumuona katika misuti ya tai kama huyu wa kwetu bara. Ninafikiri Karume si mlimbukeni, na hilo linajitokeza katika mavazi - ambayo kwa lugha ya kisosholojia ni ngozi ya kijamii (social skin).

    ReplyDelete
  8. Kwani na huyo askari nyuma ya JK nae CCM? Mbona nae ana kijani?????

    Ankal angalia simba mikumi usije ukaliwa tukaja kulia kwa kumkosa Ankal nambali wani duniani na kushindwa kuendeleza libeneke la globu.

    ReplyDelete
  9. Result OrientedApril 09, 2010

    Watu wanapokea PhD bila majoho itakuwa sherere za Chama?

    ReplyDelete
  10. Michuzi tutafutie jibu la swali hili. Watu wengi humu na siku zilizopita tumeshaliuliza sana.

    KWA NINI KARUME HATAKAGI KUVAA MAGWANDA YA CHAMA HATA AKIWA KWENYE VIKAO VYA CHAMA?

    ReplyDelete
  11. suali la karume kuvaa magwanda ya ccm linazidi kuulizwa kila kikicha na kila mmoja atakuja na idea yake.

    Lakini anaejuwa ukweli wa mambo ni mwenyewe karume, asipoulizwa na kujibu tulobaki tutakuwa na dhana zetu tu.

    Hata hivyo, naamini kuwa viongozi huwa hawanunui haya mavazi, (sio kama wanachama walala hoi). Mavazi haya wao hupewa in advance na wanaosimamia hafla wakishirikiana na PR wa viongozi husika. Kwa hivyo basi ipo posibiliti kuwa karume hapatiwi haya magwanda in advance, mind you yeye ni mrefu sana labda hakuna CCm hawaagizi size yake.

    ReplyDelete
  12. Karume naonesha kuwa anamaliza muda wake na hataongezewa tena. Ndio maana havai kijani

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...