Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Khamis Mgeja akikabidhi kwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete mchango wa jumla ya Tshs.1,482,200/- kutoka kwa jumuiya ya umoja wa vijana mkoa wa Shinyanga kwaajili ya fomu ya ugombea urais ya Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete.Makabidhiano hayo yalifanyika jana jioni ikulu jijini Dar es Salaam na kushudiwa na viongozi wote wa CCM mkoa wa Shinyanga.Kulia ni Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Shinyanga Stephen Julius Masele amnaye pia alisoma ujumbe maalumu wa vijana wa mkoa wa Shinyanga.
viongozi wa CCM Mkoa wa Shinyanga wakiwa katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete ikulu jijini Dar es Salaam jana jioni.

(picha na Freddy Maro).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 20 mpaka sasa

  1. amakweli mpendazoe amedanganywa,onaa jamaa wa mkoa wake wanavyofurahi,wanakuja wanauhakika wa kiti kimoja zaidi kumpa mtu wao.

    ReplyDelete
  2. Does that help? i think as Tanzanians we need to change a bit. it would be very helpful if UVCCM - Shinganga would send a message to President informing him some of the problems and challenges are facing wananchi paricularly those who are staying at Shinganga. through that it would be possible for them to boost a thousand time the election manifesto of CCM rather than giving the president few cash. wananchi are suffering, if you visit rural areas its when you can really see those problems. Our president need to know that so that he can get ready once again to be more focused on the really problems rather than being illusional. I hate youth doing staff like that which are less helpful. I believe we can change and help our leaders be more focused. Youth used to do that soon after Independence, they were setting agendas but now we are moving without any agenda. Are we power mongers or just kuchumia tumboni?

    ReplyDelete
  3. UTAMADUNI WA KUCHANGIA WATU MASIKINI WAPELEKE WATOTO WAO SHULE HATUNA. INASIKITISHA SANA HUU UBINAFSI TULIO NAO!

    ReplyDelete
  4. Ujumbe mzito wa wajumbe wengi toka shinganya hadi dar imegharimu zaidi ya hizo walizoenda kumkabidhi Kikwete. Hapo wanauchumi mwaliona? Haiingii akilili mwangu idadi hiyo kwenda Ikulu kukabidhi eti Sh milioni moja na matumizi ya safari na kujikimu dara imezidi idadi hiyo ya pesa walizomkabishi. Labda nirudi daradaji kurudia somo la hisabati na uchumi

    ReplyDelete
  5. Kaka Michuzi naomba unisaidie hesabu kidogo, maana mimi nilifeli darasa la nne.

    Kulingana na habari uliyotupostia leo umesema kwamba shughuli hii imehudhuriwa na viongozi wote wa CCM wa mkoa wa Shinyanga. Hapo pichani kuna mtu 21, toa Rais unabaki na mtu 20. Okay, tuanze na hesabu sasa.

    Nauli Shinyanga - Dar - Shinyanga ni kiasi gani? Mi nakadiria elfu 50 one way... So, elfu 50 x 2 x mtu 15 = 1,500,000

    Kwa viongozi 20 (okay, sema wako 15 kwamba hao wengine 5 walikua wafanyakazi wa Ikulu).. Allowances kwa hao viongozi wakiwa safarini.. tuseme walikua nje ya Shinyanga kikazi kwa siku 3 (ingawa watakua wamekaa nje ya Shinyanga kwa zaidi ya siku hizo 3) ; Kwahiyo -- tukadirie wanalipwa elfu 20 kwa siku (najua wanalipwa zaidi ya hizo).. okay, elfu 20 x siku 3 x 15 = 900,000

    Kutakua na gharama nyingine nyingi tu ambazo sitaki kuzitaja hapa; Ila ebu tufanye hesabu ya haraka haraka kujumlisha izo gharama mbili.

    1,500,000 + 900,000 = 2,400,000

    Okay, turudi nyuma kwenye kilichowapeleka bongo hawa viongozi wetu... Umetuambia wameenda kupeleka mchango wa vijana wa Shinyanga ambao ni 1,482,200.

    Okay, ebu tuone puzzle hii:

    Viongozi wametumia 2,400,000 kama gharama ya kupeleka mchango wa vijana ambao ni 1,400,000.

    2,400,000 - 1,400,000 = 1,000,000

    Nafikiri wamefanya jambo zuri sana..... Makofi jamani na vigeregere..

    Huoni tunazidi pata majibu zaidi ni kwanini Tanzania yetu ni masikini almost 50 years after independence?

    ReplyDelete
  6. Oh mi sikujua kama Ikulu ya Bongo unaweza kuingia umevaa kanda mbili.. Naona jaamaa kapiga sandles..


    Kweli Bongo tambarare....

    ReplyDelete
  7. heart attack kwa viongozi hawa zipo hatarini.

    ReplyDelete
  8. Michuzi nimekuwekea mchanganuo wa hesabu za matumizi ya hawa jamaa kuja dar vs pesa waliyoileta lakini umeubania. Au unataka niseme MICHUZI MTU MZURI SANA ndio uibandike comment yangu?

    ha ha ha.... Michuzi bwana kwa kuyeyusha watu, duh.

    ReplyDelete
  9. CCM bwana hawezi kuachana na mambo ya uswahili!
    Huo mchango ni kisingizio,haya ni madongo kwa Mpendazoe, na tutaendelea kuona vituko vingi, na Mhe Rais anavipa baraka zake!
    Haya angewaachia akina Makamba!
    Kweli kutwaliwa na mkwere ni kazi, aachi jadi yake!
    ninajua Ankal hii hutaiweka lakini message sent, wafikishie huko Ikulu.

    ReplyDelete
  10. Yote njaa
    ni ccm hap propaganda zao
    wamewalipia hata nauli ili kujibu kombora la mpendazoe.
    Lakini wana shinyanga hatudanganywi na hizo propaganda
    ccm mwaka huu shinyanga hamna chenu
    utajiri wote wa madini shinyanga eti mkoa wetu ni wa kwanza kwa umasikini tanzania

    ReplyDelete
  11. Anyway, walikuwa Dar kwenye mkutano wa CCM uliofanyika juzi mlimani city na wakatumia ujio huo kwenda ikulu kujielezea kama CCM itashinda au vipi.Maana huyu Mpendazoe anatokea huko.
    Il kama jamaa aliposema hapo juu pamoja na hayo gharama za kujikimu ni kubwa kuliko mchango, bora wangesomesha watoto 10 day sec school ya serikali kwa mwaka mmoja hapo SHY.

    ReplyDelete
  12. MSAADA TUTANI

    kamichu, hilo shati la raisi wetu tafadhali niambie linakopatikana au kama unaweza kuniombea tafadhali manake katoka najua na mume wangu atatoka hivyo hivyo.

    ReplyDelete
  13. I dont understand.... what is the contribution for? is JK trying to win back the office? If so I good for him (i wish i was him). what about you bro michuzi?

    RIP - Mwalim

    ReplyDelete
  14. Raisi Kikwete hajui kwa nini Tanzania ni maskini. Tukio na mchanganuo huo hapo juu unaweza kumsaidia kujibu swali hili.

    ReplyDelete
  15. Naona kuna baadhi ya wachangiaji hapa hawajajua dhana ya kumchangia Rais hiyo inaitwa kumuunga mkono na kutaka agombee tena nafasi ya urais kupitia CCM,pia haina maana Mh.Jakaya Kikwete hana uwezo wa shs 1mn kwa hiyo ,pia ikumbukwe kulikuwa na semina ya viongozi wa ccm jiji Dar es alaam kutoka nchi nzima hao viongozi walikuwa Dar kwa shughuli hiyo ndipo wakatumia fursa hiyo kwenda Ikuku kumpatia Mh Kikwete hizo fedha!SIo kama walisafiri rasmi kutoka Shinyanga kwenda Dar kwenda kumkabidhi Rais hizo fedha

    ReplyDelete
  16. Wewe mchangiaji wa Pili una dandia Treni kwa mbele!Umesoma maelezo ya picha vizuri?Kuwa pamoja na kumkabidhi Rais fedha hizo Mwenyekiti wa Vijana wa Mkoa wa Shinyanga alisoma ujumbe maalum wa vijana ulijua walisoma ujumbe gani?
    Wengine wanasema kama kuna ruhusiwa ikulu kuingia na kanda mbili je huenda huyo aliye vaa sandals ana matatizo ya fungus hawezi vaa viatu vingine?Jamani punguzeni kupinga kila kitu this is too much!!!

    ReplyDelete
  17. hii nchi ni shida tupu, wanasema huo ni ujumbe wa UVCCM shinyanga. ndugu zangu mbona mimi namuona kijana mmoja tu hapo na wengine wote ni wazee. Da Tanzania ni zaidi ya kichwa cha Mwendawazimu

    ReplyDelete
  18. Nyie mlioweka mahesabu ya kiuchumi kuna mtu kawambia ya kuwa hao viongozi wa CCM mkoa wa Shinyanga wanafanya biashara ya kununua na kuuza form za wagombea Urais?Mpaka muwapigie hasara na faida za kupeleka hizo fedha?

    Walichokifanya hao wana CCM wa Shinyanga ni kuonyesha "Political support"kwa Kikwete!

    ReplyDelete
  19. Hebu watanzania tujaribu kujali afya zetu, hebu cheki huyo jamaa, eti ni mwenyekiti wa vijana lakini amezeeka kuliko hata kikwete, fanya mazoezi bwana, kama vipi endesha mabaisikeli huko shinyanga

    ReplyDelete
  20. Ni vizuri kukipiga tafu chama unachokipenda, lakini je vipi kuhusu kuvuta maji hapo SHY?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...