
JK akipokea ujumbe kutoka kwa Rais wa Misri Hosni Mubarak wa Misri toka kwa Mhe.Profesa Mohamed Nasr El-Deem Allam ambaye ni Waziri wa maji na Umwagiliaji wa Misri ikulu jijini Dar leo asubuhi. Picha na mdau Freddy Maro wa Ikulu
Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, leo, Ijumaa, Aprili 2, 2010, amepokea ujumbe maalum kutoka kwa Rais Hosni Mubarak wa Misri.
Ujumbe huo maalum kutoka kwa Rais Mubarak umewasilishwa kwa Rais Kikwete na mjumbe maalum wa kiongozi huyo wa Misri, Mheshimiwa Muhamed Nasra Eldinallam, ambaye ni Waziri wa Maji na Umwagiliaji wa Misri katika shughuli fupi iliyofanyika Ikulu, Dar Es Salaam.
Ujumbe huo maalum unahusu jinsi Tanzania na Misri zinavyoweza kuongeza ushirikiano katika uendeshaji wa Bonde la Mto Nile.
Akipokea ujumbe huo kutoka kwa Mheshimiwa Eldinallam, Rais Kikwete amemshukuru Rais Mubarak kwa kumtumia ujumbe huo na kumtakia afya njema kiongozi huyo wa Misri ambaye karibuni alipelekwa Ujerumani kwa matibabu.
“Namshukuru sana Rais Mubarak kwa ujumbe wake maalum. Mapendekezo yake kwenye ujumbe huu ni mapendekezo mazuri na makini, tutakaa kama Serikali baada ya Sikukuu ya Pasaka, tutayajadili na tunawatumia majibu mazuri,” amesema Rais Kikwete baada ya kuwa amesoma ujumbe huo maalum wa Rais Mubarak.
Ameongeza Rais Kikwete: “Namwombea Mheshimiwa Mubarak apone haraka. Namtakia afya njema. Ameifanyia mengi mazuri Misri na ameifanyia mengi mazuri Afrika.”
Kumbe JK naye hajui etiquettes za kusalimiana, hutakiwi kuangalia chini au pembeni when shaking hands, u are supposed to look the person into the eye and your handshake should be ''firm'' especially in an official event like this....hii pia ni muhimu when tossing, look the person into the eyes...
ReplyDeleteWewe unaangalia etiquette wakati JK anaangalia bahasha huku akiwaza kamaa ndio wanatangaza vita au vipi? Issue ya maji between sisi na Misri si lelemama
ReplyDeleteNaomba Kumjibu anonymous wa kwanza kwa heshima zote."To look the person into the eye" hayo ni mambo ya Magharibi bwana. There is something beautiful about shyness, even though in some cultures (like the west)is not considered a virtue. Shy people have long shadows, where they keep much of their beauty hidden from intruder's eyes. Shy people remind us of the mystery of life that cannot be simply explained or expressed with a simple "eye contact".
ReplyDeleteNawasilisha!
Mlokole, DC
hivi raisi hana-dress code?
ReplyDeleteHilo jaketi haliendani ki-ofisialo!
ReplyDeletewamisri washenzi hawataki tutumie maji ya ziwa victoria ktk shughuli za maendeleo ili hali wao wanayafaidi maji yatokayo ziwa hilo
ReplyDeleteAlikua anasoma hiyo barua kuona imekuja na kiasi gani? "MISAAADA"
ReplyDelete