JK akipokea ujumbe kutoka kwa Rais wa Misri Hosni Mubarak wa Misri toka kwa Mhe.Profesa Mohamed Nasr El-Deem Allam ambaye ni Waziri wa maji na Umwagiliaji wa Misri ikulu jijini Dar leo asubuhi. Picha na mdau Freddy Maro wa Ikulu

Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, leo, Ijumaa, Aprili 2, 2010, amepokea ujumbe maalum kutoka kwa Rais Hosni Mubarak wa Misri.

Ujumbe huo maalum kutoka kwa Rais Mubarak umewasilishwa kwa Rais Kikwete na mjumbe maalum wa kiongozi huyo wa Misri, Mheshimiwa Muhamed Nasra Eldinallam, ambaye ni Waziri wa Maji na Umwagiliaji wa Misri katika shughuli fupi iliyofanyika Ikulu, Dar Es Salaam.

Ujumbe huo maalum unahusu jinsi Tanzania na Misri zinavyoweza kuongeza ushirikiano katika uendeshaji wa Bonde la Mto Nile.

Akipokea ujumbe huo kutoka kwa Mheshimiwa Eldinallam, Rais Kikwete amemshukuru Rais Mubarak kwa kumtumia ujumbe huo na kumtakia afya njema kiongozi huyo wa Misri ambaye karibuni alipelekwa Ujerumani kwa matibabu.

“Namshukuru sana Rais Mubarak kwa ujumbe wake maalum. Mapendekezo yake kwenye ujumbe huu ni mapendekezo mazuri na makini, tutakaa kama Serikali baada ya Sikukuu ya Pasaka, tutayajadili na tunawatumia majibu mazuri,” amesema Rais Kikwete baada ya kuwa amesoma ujumbe huo maalum wa Rais Mubarak.

Ameongeza Rais Kikwete: “Namwombea Mheshimiwa Mubarak apone haraka. Namtakia afya njema. Ameifanyia mengi mazuri Misri na ameifanyia mengi mazuri Afrika.”

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Kumbe JK naye hajui etiquettes za kusalimiana, hutakiwi kuangalia chini au pembeni when shaking hands, u are supposed to look the person into the eye and your handshake should be ''firm'' especially in an official event like this....hii pia ni muhimu when tossing, look the person into the eyes...

    ReplyDelete
  2. Wewe unaangalia etiquette wakati JK anaangalia bahasha huku akiwaza kamaa ndio wanatangaza vita au vipi? Issue ya maji between sisi na Misri si lelemama

    ReplyDelete
  3. Naomba Kumjibu anonymous wa kwanza kwa heshima zote."To look the person into the eye" hayo ni mambo ya Magharibi bwana. There is something beautiful about shyness, even though in some cultures (like the west)is not considered a virtue. Shy people have long shadows, where they keep much of their beauty hidden from intruder's eyes. Shy people remind us of the mystery of life that cannot be simply explained or expressed with a simple "eye contact".
    Nawasilisha!
    Mlokole, DC

    ReplyDelete
  4. hivi raisi hana-dress code?

    ReplyDelete
  5. Hilo jaketi haliendani ki-ofisialo!

    ReplyDelete
  6. wamisri washenzi hawataki tutumie maji ya ziwa victoria ktk shughuli za maendeleo ili hali wao wanayafaidi maji yatokayo ziwa hilo

    ReplyDelete
  7. Alikua anasoma hiyo barua kuona imekuja na kiasi gani? "MISAAADA"

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...