Mwenyekiti wa UVCCM Yusuf Masauni akimkaribisha Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika viwanja vya CCM Maisara mjini Zanzibar jana jioni ambapo aliyapokea maandamano ya vijana na kuwahutubia. Leo ni Siku rasmi ya Karume na ni mapumziko nchi nzima Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete Mwenyekiti wa Jumuiya ya umoja wa Vijana CCM Yusuf Masauni(wapili kushoto), Makamu mwenyekiti wa jumuiya hiyo Bwana Beno Malisa(kushoto), na katibu mkuu wa jumuiya ya umoja wa Vijana CCM Bwana Martin Shigela wakiyapokea maandamano ya vijana wa CCM katika viwanja vya CCM Maisara Zanzibar jana jioni.Rais Jakaya Kikwete ambaye ndiye aliyekuwa mgeni Rasmi katika maandamano hayo aliwahutubia vijana hao.
Rais Jakaya mrisho Kikwete, Rais Amani Abeid Karume wa Zanzibar(kulia) na Mwenyekiti wa jumuiya ya umojawa Vijana wa CCM Bwana Yusuf Masauni wakati wa mapokezi ya maandamano ya umoja wa vijana wa CCM mjini Zanzibar jana jioni.
vijana wa jumuiya ya Umoja wa vijana wa CCM, UVCCM wakipita mbele ya Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete wakati wa maandamano ya kumuenzi muasisi wa mapinduzi ya Zanzibar Hayati Mzee Abedi amani Karume yaliyofanyika katika viwanja vya CCm Maisara, Zanzibar jana jioni
vijana wananchama wa UVCCM wakishangilia hotuba ya Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete aliyoitoa wakati wa kilele cha maandamano yaliyoandaliwa na jumuiya hiyo mjini Zanzibar kumuenzi muasisi wa mapinduzi ya zanzibar marehemu Mzee Abeid Amani Karume.
vijana wa jumuiya ya Umoja wa vijana wa CCM, UVCCM wakipita mbele ya Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete wakati wa maandamano ya kumuenzi muasisi wa mapinduzi ya Zanzibar Hayati Mzee Abedi amani Karume yaliyofanyika katika viwanja vya CCm Maisara, Zanzibar jana jioni.
Mjane wa Muasisi wa mapinduzi ya Zanzibar Mama Fatma Karume pamoja na mke wa Rais wa Zanzibar Mama Shadya Karume wakati wa dua ya kumuombea Marehemu Mzee Abeid Amani Karume iliyosomwa wakati wa kilele cha maandamano ya UVCCM kumuenzi muasisi huyo jana mjini Zanzibar.
Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwahutubia vijana wa UVCCM walioshiriki katika maandamano ya kumuenzi Marehemu Mzee Abeid Amani Karume mjini Zanzibar







Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. Hilo ni tukio la kitaifa au la CCM?
    CCM acheni utani, kama mnataka kudumisha muungano na umoja wa waTanzania inabidi muheshimu mipaka kati ya chama na taifa. Kwa hiyo wanachama wa CUF hawaruhusiwi kumuenzi Mzee Karumue?

    ReplyDelete
  2. Mdau umeongea ukweli viongozi wa serikali TZ waache kuchanganya mambo!!
    Mfumo wa vyama vingi ni muhimu kutofautisha shughuli za SIASA NA SERIKALI.
    Tuelewe kwamba WALIPA KODI ni wa vyama vyote, hivyo sio busara kuweka mbele shughuli za chama kimoja kwa kutumia kodi za wanachama wa vyama vingine.
    Kingine siasa ziweke kipa umbele kuimarisha uchumi na haswa kumuinua mlala hoi, na kukubali kukosolowa na kuwajibika kwa walioko madarakani, ili kuwe na ushindani katika kuleta maendeleo.

    ReplyDelete
  3. yusuf masauni ni ushahidi mwingine kuwa watu wanapata vyeo ccm kwa kuvaa majoho ya wazazi wao. Tanzania nzima tunaona kila leo watoto wa viongozi nao wanatumia link zao kuwabeba watoto wao, si ajabu tanzania tupo tulipo leo.

    ReplyDelete
  4. fungueni macho nyie,kwani hamjasoma habari,ni ccm wameandaa dua maalum kwa mzee karume,na hapo kikwete kaenda kama mwenyekiti wa ccm na sio rais.kwa hiyo na cuf wangeweza kumuenzi karume na lipumba kuwa mgeni rasmi.

    ReplyDelete
  5. mdau wa Wed Apr 07, 12:27:00 PM, usishangae sana, haya tumeshayazoea haya. ukiwa mtoto wa mkubwa hata uwe na criminal record inayojulikana kimataifa bado hukosi nofu.

    ReplyDelete
  6. Mbona huyu Amani Karume hakuvaa kijani ya CCM?

    ReplyDelete
  7. kaka nakupongeza kwa kazi nzuri ya kutuletea habari moto moto za huko nyumbani.

    nawapongeza wana ccm kwa kumkumbuka mzee hayati karume ila nadhani suala la kuwakumbuka na kuthamini mchango wa wanaoifanyia CCM kazi usiwe kwa viongozi wa juu tu.

    mimi nilikuwa SUA miaka ya 2006-2008 wanafunzi wa SUA hawakuwa na ofisi ya tawi la CCM pale chuoni. mwenyekiti wa tawi la CCM wanafunzi wakati huo alihamasisha michango akafanikiwsha ujenzi wa tawi la CCM SUA ambazzo hadi leo zinatumika.

    jamaa alipomaliza shule alirudi kazini kwake wizara ya mifugo. mwezi januari nimerudi nyumbani nimemkuta yuko kwenye desk lile lile ambalo alipangiwa kabla hajapata shahada na jamaa ameamua kuendelea na kujiendeleza kimasomo baada ya kuona serikali ya CCM aliyokuwa anajivunia na kuitumikia imemuweka pembeni.

    huo ni mfano mmoja ila kuna vijana wengi ambao wanatoa michango mingi na mikubwa kwa chama ambao hawtambuliki. napendekeza pongezi na kukumbukwa huku kusiishie kwa wakubwa tu.

    ReplyDelete
  8. Nakuunga mkono anonymous wa apr 07 01;49;00PM. WANA CCM NDIYO HOST WA SHUGHULI NA MKUMBUKE KARUME ALIKUWA MWANA CCM WAKATI ANAKUFA. INGAWA ALIKUWA RAIS LAKINI NI WA CCM HAKUNA ALIYEKATAZWA KUMUENZI KIONGOZI YEYOTE YULE! HEMBU WATANZANIA TUJIFUNZE KUCHAMBUA MAMBO KWA KUFUATA HISTORIA YA NCHI YETU NA SIYO KUKASHIFU KILA KITU CHA CCM. KUNA WATU WANA ALLERGY NA RANGI ZA CCM! WAKION KIJANI TUU BASI KILA KITU KIBAYA. CCM JUUUUUUUUU! KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI.

    ReplyDelete
  9. kwani ni lazima ukikitumikia chama upate madaraka serikalini? hilo ni suala la kiutendaji serikalini sio CCM wala CCJ serikali yoyote itakayofuatilia nguvukazi yake haiwezi kufanya jambo kama hilo. toeni siasa katika kazi.

    ReplyDelete
  10. imeandikwa CCM itajengwa na wenye moyo sasa akishajenga mnataka iwaje. hiyo ni sadaka. huyo jamaa lazima hajatoka katika familia bora alidhani kwa juhudi zake wangemuona hiyo ilikuwa CCM ya Zamani sio sasa.

    ReplyDelete
  11. wewe annon 10:25pm acha uongo wakati rais Karume anauwawa kulikuwa hakuna ccm,ila palikuwe ASP NA TANU

    ReplyDelete
  12. wewe anon wa Wed Apr 07, 10:25:00 PM nenda kadanganye watoto wenzako barazani. karume amefariki 1972 na hapakuwepo na ccm.

    na kusema kweli kama angelikuwa hai mpaka leo basi sidhani kama ccm ingelizaliwa. Wazanzibari tunakumbuka sawa sawa alipokuwa akisema kuhusu muungano "muungano mwisho chumbe pia "muungano ni kama joho ukichoka unavua" kwa maneno hayo hatudhani kama angelikubali kuunganisha vyama.

    Pia tunakumbuka tulivyokuwa tukisema kila siku wakati wa assembly maskulini Marehemu mzee abedi amani karume ameuawa na amezikwa; lakini kilichokufa na kuzikwa ni kiwiliwili chake tu, member, mawazo na busara zake zipo pale pale na zitadumishwa milele

    Sadly alhaj aboud jumbe na wenzake walishondwa kutimiza ahadi hii.

    ReplyDelete
  13. panasomwa dua na ni mmoja tu aloinuwa mikono, his wife, walobaki hata habari hawana including his daughter in law.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...